Zingatia mambo haya ili usiibiwe kirahisi

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
229
1. Vitu ambavyo huwezi kuishi bila kuwa navyo kaa navyo muda wote na usithubutu kumuachia mtu akuangalizie.

2. Kama umeingia hotelini, hakikisha baada ya kukaguliwa mizigo yako kama vile vidani, simu au kompyuta na nyaraka muhimu unaweka sehemu salama.

3. Usiwe mzembe ukiwa safarini, hakikisha unakuwa makini na mazingira yanayokuzunguka.

4. Kama unasafirisha mzigo toka nje ya nchi hakikisha unakata “insurance” kwa ajiri ya usalama wa mzigo huo njiani.

5. Kamwe usithubutu kuacha vitu vyako vya thamani ndani ya gari.

6. Kama huwezi tembea na mizigo yako hakikisha unaificha vyema ndani ya gari na usifanye hivyo katika eneo la maegesho wakati watu wakikuona.

7. Weka vitu vyako vyote vya thamani katika begi lako la mkononi ili uwe karibu navyo.

8. Hakikisha muda wote gari yako imefungwa vyema.

9. Kamwe usiache ufunguo kwenye gari iwe mlangoni au sehemu ya kuwashia.

10. Ukinunua kitu hakikisha unapewa stakabadhi kwa kile kitu na iliyoandikwa thamani ya kitu ulichonunua.
 
Hapo namba 6 na 8 wezi wa siku hizi wanamwagia kemikali kwenye vioo vya gari na kuvisambaratisha kisha kuchukua mizigo iliyomo kirahisi kabisa.Na kuhusu namba 7 ukitembea na begi lako mkononi muda wote badala ya kuibiwa utanyang'anywa na kuumizwa kama siyo kutolewa roho. Hii dunia imeharibika.
 
Hapo namba 6 na 8 wezi wa siku hizi wanamwagia kemikali kwenye vioo vya gari na kuvisambaratisha kisha kuchukua mizigo iliyomo kirahisi kabisa.Na kuhusu namba 7 ukitembea na begi lako mkononi muda wote badala ya kuibiwa utanyang'anywa na kuumizwa kama siyo kutolewa roho. Hii dunia imeharibika.
Ni kweli mkuu lakini ukiwa mtu makini itakusaidia san kujihakikishia usalama kiasi fulani,
 
Hizi hazi-apply kwenye utapeli maana huo kwangu ndo naona changamoto kwa wajasiriamali wa mjini.

Umetoa shule nzuri sana.
 
Mimi nimesha surrender kwa wezi wa sasa waibe tu kila kitu ila atakaye thubutu kuniibia kibalua changu huyo nakufa naye...!!
 
Back
Top Bottom