Zingatia hili

Zingatia hili

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Posts
9,252
Reaction score
6,211
Hii ni muhimu kwa wadada ambao hawajaolewa na wanapenda maisha ya ndoa

-Usiolewe sababu rafiki zako wote wameolewa.
-Usiolewe sababu class mates zako wote wameolewa na wanawatoto.
-Usiolewe sababu umemaliza chuo, unaishi mwenyewe na unakazi nzuri.
-Usiolewe sababu kila mtu kanisani anakuuliza pilau tutakula lini.
-Usiolewe sababu wazazi wanataka kumuona mkwe na wajukuu.
-Usiolewe sababu wazazi na wewe mmechoka kuchanga sasa mnataka kuchangiwa.
-Usiolewe ili uonekane umeolewa.
-Usiolewe kwa sababu umepata ujauzito.
-Usiolewe sababu unaogopa kuzeeka ukiwa mwenyewe.
-Usiolewe sababu unaona umri unakwenda.
Ndoa sio jumuia, ndoa sio destination, ndoa sio zawadi kwa wazazi, ndoa sio social status, ndoa sio watoto, ndoa sio kuondoa nuksi..
Olewa kwa sababu ni wakati wa Mungu wewe kuolewa, umempata mtu sahihi mnayependana kwa dhati, umeridhia kutoka moyoni bila kuwa influenced na kitu chochote.
Ni bora uendelee kuishi mwenyewe kuliko kuingia kwenye ndoa ya majuto. Mngojee Bwana na hakika hatakuacha wala hajakusaha

​
 
wakati wa Bwana ndio wakati upi huo?
 
Ni wakati ambapo unaona kila unayemkamia akuoe anakupa kibuti cha shingo hapo lazima Sir God atafutwe kokote alipo,c unajua raia wema hatumtafuti Sir God mpaka muda wa dk za nyongeza mkuu:faint:

Hahaha hizi sentensi nimezipenda bure eti hadi dakika za nyongeza.........Swala la ndoa si swala rahisi bila uwepo wa Mungu. Watu waliokota mabomu badala ya wenzi wa ndoa na matokeo yake mabomu yaliwalipukia ndani ya nyumba wanabaki wanajuta milele. Mungu pekee.
 
Badili ya kuweka hizo guidelines kwanini watu wasibadilike kifikra ambazo zimetawala jamii kuwa kama wewe ni mwanamke lazima uolewe @ certain age. Kufanya hivyo mnamuweka mwanamke kwenye 'hard time', sio wote huwa wanajaliwa kupata wenza wawatakao could be any reason.

Mimi naomba acheni kuwanyanyapaa na kila mmoja ajue lake ikiwa kitu hakikuhusu...............hasa ukiwa unaaamini mke bora na mume bora anatoka kwa mungu then let it happen naturally.
 
Ni wakati ambapo unaona kila unayemkamia akuoe anakupa kibuti cha shingo hapo lazima Sir God atafutwe kokote alipo,c unajua raia wema hatumtafuti Sir God mpaka muda wa dk za nyongeza mkuu:faint:
Hii nayo ni kweli
 
Badili ya kuweka hizo guidelines kwanini watu wasibadilike kifikra ambazo zimetawala jamii kuwa kama wewe ni mwanamke lazima uolewe @ certain age. Kufanya hivyo mnamuweka mwanamke kwenye 'hard time', sio wote huwa wanajaliwa kupata wenza wawatakao could be any reason.

Mimi naomba acheni kuwanyanyapaa na kila mmoja ajue lake ikiwa kitu hakikuhusu...............hasa ukiwa unaaamini mke bora na mume bora anatoka kwa mungu then let it happen naturally.

madamX umesema vema kabisa, jamii ibadilishe mtazamo vinginevyo mtoa mada ametoa ushauri mzuri sana
 
Last edited by a moderator:
Badili ya kuweka hizo guidelines kwanini watu wasibadilike kifikra ambazo zimetawala jamii kuwa kama wewe ni mwanamke lazima uolewe @ certain age. Kufanya hivyo mnamuweka mwanamke kwenye 'hard time', sio wote huwa wanajaliwa kupata wenza wawatakao could be any reason.

Mimi naomba acheni kuwanyanyapaa na kila mmoja ajue lake ikiwa kitu hakikuhusu...............hasa ukiwa unaaamini mke bora na mume bora anatoka kwa mungu then let it happen naturally.

hahha usemalo ni kweli sio lazima kuolewa ila tatizo ni kwamba mwanamme haolewi lakini anajaza mabf kibao. kama hujapata wakukuoa basi bana miguu yako
 
Lol...unaangushiwa kama furushi toka juu.....

Nadhani Mungu anachofanya ni kutoa fursa au kuandaa mazingira ya watarajiwa kukutana, suala ya kumwaga mbungi "kutongozana" hilo labakia kuwa la wahusika...sasa fursa hii ndio sisi wanadamu twaitumia vibaya
 
Ogopa mazingira kama baa au kilabuni............itakuwa imeandaliwa na shetani
 
Back
Top Bottom