Zingatia hili ni muhimu sana kabla hujaoa

Zingatia hili ni muhimu sana kabla hujaoa

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
522
Habari wanaJF,

Kusema ukweli nimejaribu kufanya uchunguzi mdogo ambao unahusu kijitabia fulani cha wanawake ambacho ni muhimu zaidi kukifikiria na kukifanyia kazi kabla hujaingia katika maamuzi magumu ya kuoa. Mara nyingi ndoa za siku hizi zinaonekana kutodumu kwa muda mrefu kuzidi hata muda wa uchumba.

Watu wanaweza kuwa wachumba kwa miaka mitano, lakini kwenye ndoa ndani ya miaka miwili au mmoja tu wameachana. Kuna matatizo mengi, lakini ninalotaka kuliongelea ni hili ambalo wengi aidha hatujui au tunapuuza. Kisaikolojia, mwanamke ukishamuoa tu, yeye anafikiria kukumiliki katika himaya yake.

Uwe unamfikiria yeye muda wote na niamini mimi, mwanamke akikutilia shaka haswa kuhusu kuchelewa kurudi nyumbani, yeye anachowaza ni kuwa unamsqaliti tu, wachache saaana watafikiria positive, wachache mno. Kama ulikua na tabia zako ulizomuonyesh mwanamke katika uchumba wenu, halafu baada ya ndoa ukabadilika, basi jua kuwa utagombana nae tu.

Wanawake wana tabia ya kujaribu kukuwekea misimamo yao na masharti yao, yaani wana tabia ya kujaribu kuona kama akikwambia kitu flani utachukuliaje. Kumbuka kuwa ukikubali kwa mara ya kwanza, basi huo ndo msimamo wake, ukibadilika mtagombana tu. Kwa mfano anaweza kukwambia, "Naomba isizidi saa 12 uwe hapa nyumbani" halafu ukatii kwa mara ya kwanza, siku ukirudi saa 2 jua kuwa mtagombana tu hata kama saa 2 bado mapema.

Kingine muhimu zaidi, usikosee ukamfanya mwanamke kuwa ndio msemaji wa familia haaaaa..kosa kubwa hili, usifanye! Utapoteza marafiki wengi sana siku zote act kama mzazi kwa wanao na mkeo yani wako vzuri sana katika ushauri hawa mama zetu, lakini "Accept her opinions, but you must have final decisions" ukimpa final decisions ndoa lazima itakushinda.

Namalizia hivii;
Wanawake hawana matatizo, tatizo ni wewe mwanaume umemzoesha vipi.

Sababu kuu mbili za kukosana na mwanamke ni:
1. MAVAZI
Yaani, ukimbania kwenye mavazi na yeye anataka avae apendeze, jua kuwa mtagombana. Hapa ni chanzo cha migogoro mingi saana saana sana na vijana wengi wanaoingia kwenye ndoa hawajui hili.

2. MICHEPUKO
Hii inachekesha kidogo, maana wanawake wengi ukianza kuchepuka tu na yeye anachepuka sasa wewe ukigundua ndo mnagombana na hata kama hatochepuka, lakini mwanamke anapenda sana mume awe wake peke yake. Kama umeamua kuoa, acha kuchepuka utamteka vizuri mwanamke.

Naomba niage

N.B
Niliwahi kuoa ��
 
Kumbe kuna kupangiwa muda wa kurudi home? hii nilikuwa sijaijua bado.
 
Ukioa viruka njia na Watoto wa Pwani lazima hayo yakutokee .. Huwa Hawana Akili za Kujenga Uchumi wa Familia anawaza Kupet pet tu na Kutunza Mume

Mwanamke anawaza Ukichelewa ulikuwa na michepuko...😂.. Mara muda wa Kurudi home...😂
 
Duu, mbona mtihani, ntaweza kweli. Mi sio mchepukani, Ila Hamna kitu ninachokifurahia my time alone, pindi ninapokuwa nimetingwa na mambo mengi. Na hili pia ni chanzo kikubwa cha migogoro. Wanawake wako too emotional afu wanapenda all your time for themselves. Hapa ndo huwa ugomvi wangu na wao unaanzia,
 
Siku hizi hakuna ndoa kwa maana ya ndoa bali kuna watu wawili wa jinsia tofauti waishio pamoja kwa ajili ya kutimiziana haja za miili yao...
 
Tatizo linatokana na siku zote unarud nyumbani sa 12 jioni leo umerudi saa5 usiku bila taarifa mapema ....lazima kiwake tu
 
If you are a woman and your husband is cheating on you its your fault and if your a man and your wife is cheating on you its your fault...
 
Ndoa bwana kila leo kuna somo jipya yealekea ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom