Zingatia haya kulinda afya yako ya mwili

Plaintiff

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
308
203
Kumekuwa na malalamiko humu ndani watu wanapoleta matatizo yao ya kimwili na baadhi ya watu kuanza kuleta mizaha.

Mjadala wangu leo umebase sana kwenye magonjwa yasiyoambukiza kisukari, pressure, Kansa and the likes.

Wakati tunakua huko kijijini hayo magonjwa walikuwa wanasema ni magonjwa ya wenye pesa. Unajua kwanini? Huku afrika mtu mwenye pesa ndio mtu mwenye ulaji mbaya(sehemu kubwa ya chakula chake imejaa animal products). Je huku ndio kula vizuri?

Na shida yetu kubwa inaanzia mahali hapa, mtu anapoamua kufanya chakula kama moja wapo ya starehe yake. Mwili wa mwanadamu haujawahi kuridhika siku ukilijua hili utajiepusha na mambo mengi sana.

Wakati Mungu anaumba dunia alishaweka misingi kwamba binadamu atakula nini na ukisoma mwanzo 1:29-30

Mwanzo 1
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

Hiki ndio kitu Bora ambacho Mwenyezi Mungu aliona kingemfaa mwanadamu hasa ukizingatia mipango yake ilikuwa mwanadamu aishi milele, kuishi kwake milele kungetegemea afya yake ya mwili kwa sehemu kubwa.

Labda nikushauri kitu kimoja, ikiwa Mungu aliliona hili kuwa jema machoni pake, Na kama ambavyo tumekuwa tukishauri kufuata mapenzi ya Mungu kwa maana ni mema, basi kuanzia leo.

1. Chakuka chako na kijae matunda na mbogamboga na product zingine za mimea.
2. Punguza sana product za wanyama na ukiweza kuacha kabisa ziache.
3. Kunya maji mengi.
4. Achana na mambo ya kukoboa nafaka.
5. Mara moja moja jifunze kufunga.

Na Mungu akubariki.
 
Back
Top Bottom