MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,184
- 5,432
Habarini wakuu,
Kwa muda mrefu sasa serikali inaonekana kukosa uhuru kwasababu kuna vitu vinavyoitisha tunaweza viita mazimwi.
Serikali imefinyanga zimwi ikaanza kuliimba usiku na mchana hatimaye likawa zimwi linalowatisha hao waliolifinyanga.
Upinzani: Hili laweza kuwa zimwi namba moja, serikali onions mambo yao hayaendi sababu ya uwepo wa wapinzani sehemu muhimu wanakonywea kahawa kama mbeya,arusha,dar,mwanza na kwingineko.
Bunge: Ingewezekana kulifuta Basi lingefutwa ila njia rahisi ikawa kuliziba mubashara na kumremote spika wa bunge asiwe huru.
Vyombo vya habari: Ukisikia risasi hatari basi ni kalamu. Waandishi wengi wamelazimishwa kulamba viatu vya serikali kwa kuwa walionekana kuwa na sura ya zimwi hatari kwa nchi kupitia maandishi yao.
Wataalam mbalimbali:
Tunapoongelea wataalamu ni watu wenye uweledi uliotukuka ktk fani walizosomea. Mfano madaktari, walimu, mainjinia, wanasheria na wengineo. Wanapousema ukweli kwa mujibu wa taaluma zao wameonekana ni kikwazo kwa serikali. Wataalamu wetu wakitumiwa na nchi nyingine hzo nchi zinafaidika sana kuliko sisi. Ajabu sisi hao wataalamu wanajuta kuzaliwa tz kila uchwao wana kesi na serikali eti wanaitisha serikali wakati wamefinyangwa na serikali hii hii.
Njaa: Hili zimwi ndiyo chanzo cha uharibifu mwingi, watu wameacha kutenda haki kwa kuogopa njaa. Hakimu au jaji anaelekezwa namna ya kutoa haki na mtu ambaye kwanza haelewi taaluma hiyo, aibu. Haya yanafanyika kwingi. Wakati wa ajali ya mv bukoba waziri aliwaelekeza mainjinia watoboe meli utadhani hata low of floatation anazijua mwisho akaongeza idadi ya wafu. Hizo zote ni njaa.
Serikali hii itafanikiwa kwa kasi ya ajabu pale tu itakapoacha kuogopa mazimwi iliyoyafinyanyanga yenyewe ikiwa ni pamoja na kukubali hoja za msingi bila kujali aliyetoa hoja hiyo ni nani. Leo serikali inaogopa hata ndoto za watu wakati farao aliponesha taifa kupitia ndoto. Leo lema anaogopwa kuliko alshabaab, leo lissu anazuiwa kugombea cheo utadhani wao siyo wapiga kura wamkatae ili yaishe na aaibike,Leo magazeti yanafungwa kwa sababu tu hayajamsifia pilato wetu.
Serikali ijitafakari mapema vinginevyo ipo siku mkuu wa nchi atakataa kulala ikulu kwa kisingizio mazimwi yanamkaba usiku. Hofu ni kubwa maana serikali inatembea na orodha kubwa ya majina ya wary inayowaogopa kuliko vipaumbele vyao vya maendeleo.