Zimwi lakata kamba, laanza kuwatafuna waliolifuga

Zimwi lakata kamba, laanza kuwatafuna waliolifuga

Mzarau mwiba mguu huota tende.

Sasa wanaota matende, zimwi limeimarika vizuri, usamala wa wafugaji upo mashakani
 
limepita huku kwetu, limeanza kufumua misingi ya nyumba za watu walilolifuga. na limeapa kama halipati mososi kwa wafugaji litakwenda kwa majirani
 
Hahaha zimwi likujualo halikuli likakwisha litawabakiza tu
 
Lkn walikuwa wapi kulidhibiti hawa jamaa??,nasikia sasa limekuwa na manyoya mwili mzima na limeota pembe kama za nyati!!, hata ukiwa umejificha ukiliongelea lina pata taarifa na linatoa mrejesho hapo hapo.

Zimwi hilo linalojinadi ya kwamba litaleta mafuliko/flood ambayo siyo mwenye nyumba wala mwanakijiji yeyote atakaeweza kuyazuia.Mafuliko hayo yata destroy miundombinu yote na kizazi chote kwenye kijiji hicho kitateketea.Ila wale wachache tu watakao msujudu na kumuunga mkono ktk maovu yake watapona na kuishi maisha ya kiflame ktk nchi ya zimwi hilo.
 
Back
Top Bottom