Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,154
- 2,758
Kama ilivyo kawaida msiba ukiwa kwa jirani, nyie majirani mnaweza kuchangisha michango, kupika chakula, kuchimba kaburi, kula na kunywa na hata kwa wengine kucheza draft au karata
Hata hivyo hali huwa tofauti kabisa kwa wafiwa hasa kama aliyeondoka ndiye alikuwa nguzo ya familia
Oktoba 29, 2025 Taifa lilikumbwa na msiba mzito lakini viongozi waligoma kuomboleza
Wakati wafiwa/wananchi wanaomboleza watawala walikuwa busy wanagonga glass za mvinyo na wisky huku wakipiga story na kupongeza kwa hili na lile
Hawakufanya hayo kwa bahati mbaya bali ni kwasababu msiba haukuwahusu wao. Wao hawakuwa wafiwa ndiomaana hawakuwa na machungu. Walichukulia kawaida
Bahati mbaya walisahau jambo moja la msingi kwamba wao si majirani bali ni watawala wa eneo kuliko tokea msiba. Kiongozi anaposhindwa kuomboleza na wanaoomboleza ipo siku heshima yake itashushwa na anaowaongoza
Kiongozi anapojitenga na watu wake wakati wa shida hawezi kupata heshima kamwe
Ukiangalia mambo yanavyoenda kuna juhudi kubwa sana za kutaka kuzima zimwi la oktoba 29 lisizungumzwe, life kifo cha kawaida lakini wafiwa wamegoma kumrishwa.
Wafiwa/wananchi wameamua kusema kama mlivyotuacha tuomboleze peke yetu tangu mwanzo tuacheni na sasa
Mjadala wa ACT wazalendo wa juzi ni kama kuna maneno baadhi ya viongozi wa ACT hawakutamani yasemwe lakini Peter Madeleka aliyasema
Ni uzumbukuku uliopitiliza viongozi kusema eti uchaguzi wa 2025 ulikuwa huru na haki wakati huo huo tume yao imekiri kuwa siku ya uchaguzi kulikuwa na vifo zaidi ya 518 (waliibuni namba hii wakidhani ni ndogo)? Hawa aliuawa kwasababu za uchaguzi, unawezaje kusema ulikuwa wa haki? Walikufa wakipigania nini?
Ni uwendawazimu kusema kuwa kura zote zilihesabiwa wakati huo huo unakiri kwamba vituo vya kupigiwa kura vilianza kuvamiwa saa tano asubuhi na wasimamizi kuanza kukimbia huku na kule na kutelekeza masanduku ya kura. Huu ni utindio wa ubongo sio uwendawazimu pekee
Hii ni kukwepa kuwajibika, lakini kifo huwa hakiendi bure. Damu ya mtu haimwagiki bure. Siku yaja na haiko mbali