'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'!

ngoja tuwasaidie japo kidogo tu

8 Januari 2012
CHADEMA; Urais utaamriwa kwa mahitaji ya Umma na Sifa za Kiongozi, si uchu au utashi wa watu/mtu binafsi
 
Asante ndugu yangu zito kwa kujibu haraka hoja hii. Kila hoja inayotaka kudhoofisha chama inabidi ijibiwe haraka na kwa uhakika.
 
Na nyie kina Zitto mnakuwa wanafki mno, mnakuwa tu sasa kama ccm yaani mnasubiri mpaka mahoja haya yanatapakaa vinyesi ndipo mnaibuka hovyo na kukanusha kishkajishkaji tu. Ulipaswa kulitolea maelezo hili toka awali lakini uliamua kuliacha kupima upepo eti? Mtaua chama na mauroho yenu....

Pangu Pakavu.
 
[h=6]Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA[/h]
Source Facebook.
 
zitto sikiliza kwa makini ule wimbo wa wanasiasa vigeugeu. Hata ulipotangaza hukutushirikisha vipi hili unatushirikisha? au ni mbinu ya kutaka kutushitukiza na kupima upepo.
 
ulitaka kugombea uenyekiti wa chadema hukufanikiwa pengine ungetuomba ushauri tungekwambia gombea au usigombee. wewe Zitto ni mtata unatangaza nagombea mara keshosigombei kesho kutwa utasema wazee wameniomba nimekubali kugombea.
 
Hii imekata mizizi yote ya fitina na nimeisevu hii kwa ajili ya mwaka 2015, Hongera zitto kwa kukubali kubadilika.
 
utamuungaje mgombea wa chadema wakati hujui atakuwa ni nani? pengine chama kitakupendekeza wewe? basi ungesema nikipendekezwa na chama sitakubali. kauli yako haisemi nafsi yako kama itatokea wewe ndiye mteule wa chama.
 
Roho mbaya inawasumbua hili gazeti na kwa mara ya kwanza nimpongeze Zitto kwa kuthibitisha kua hatogombea Urais 2015 bali atamuunga mkono mgombea wa CDM

pamoja na Msiba mambo mengine yanaendelea, Msiba haujafuta mnyukano huo ila unauweka likizo fupi Zito kusema hivyo ni dalili ya kuona kuwa hawezi kupata nafasi kwenye mnyukano huo ama wamekubaliana kitu..........
 
ulitaka kugombea uenyekiti wa chadema hukufanikiwa pengine ungetuomba ushauri tungekwambia gombea au usigombee. wewe Zitto ni mtata unatangaza nagombea mara keshosigombei kesho kutwa utasema wazee wameniomba nimekubali kugombea.

MAMA POROJO HAYO YA KWELI HUYO KIJANA MJANJA SANA NA ANAWAPUMBAZA WENZAKE, ZITO ANATUMIA MATOKEO YA TAFITI MBALIMBALI NA HIVYO ANAJUA WAZI KUWA YEYE NI MAARUFU KULIKO MWENYEKITI WAKE.NA NDIYO MAANA ALITAKA KUGOMBEA UENYEKITI AKIWA NA UHAKIKA, NA PIA KWA LENGO LA PILI LA KUMDHIBITI PADRI KATIKA KUWANIA KUTEULIWA NA CDM KUGOMBEA URAIS.....................MBOWE HILO ANALIJUA WAZI PIA KUWA YUKO NYUMA YA PAFRI NA KIJANA HUYO KWA UMAARUFU KTK CDM HIVYO NAYE ANAONA NI BORA AKABAKIA KWENYE UBUNGE WAKE NA HATA UMAKAMU M,KITI MAANA YEYE NDOTO YA URAISI HANA NA HAJATHUBUTU NA HATATHUBUTU KUONGEA (sababu.........elimu). ZITOOOOOOOOOO NI KAFULILA/HAMAD RASHIDI WA CDM IKO SIKU ATAWACHACHAFYA TU NYIE TULIENI MUONE MIMI NI RAFIKI YANGU SAANA NAMJUA ANAO MSIMAMO WA NDANI UNAOSOMEKA USONI
 
utamuungaje mgombea wa chadema wakati hujui atakuwa ni nani? pengine chama kitakupendekeza wewe? basi ungesema nikipendekezwa na chama sitakubali. kauli yako haisemi nafsi yako kama itatokea wewe ndiye mteule wa chama.

As a great thinker, you must have fast thinking! Sintagombea urais inamaana hatajitokeza kuchukua form. Atakayejitokeza na kupitishwa na chama basi atamuunga mkono. Hata kama chama kikiona ndiyeatakayekuwa anafaa kulingana na mazingira na mahitaji ya wakati huo basi yeye ndiye atakayebeba ilani na bendera ya chama. Ndio maana ya kumuunga mkono mgombea wa chadema. Au ulitaka maelezo gani ya ziada!?
 
Lisemwalo lipo na kama halipo laja.

Kuweni na subra tu mtaona mengi

'barubaru anashikishwa ukutwa.'
Kwa hiyo hapo Barubaru unataka kutuambia kama hushikishwi ukuta leo utashikishwa kesho kwa sababu imesemwa hivyo???????
 
Magazeti kama ya majira, uhuru, habari leo, mi napendekeza fedha za kuyaendesha haya magazeti wangepewa wanafunzi wa vyuo vikuu ili kupunguza tatizo la mikopo, kwani magazeti haya yanaandika upupu 2 wa kimamluki.
 
utamuungaje mgombea wa chadema wakati hujui atakuwa ni nani? pengine chama kitakupendekeza wewe? basi ungesema nikipendekezwa na chama sitakubali. kauli yako haisemi nafsi yako kama itatokea wewe ndiye mteule wa chama.

Zitto ni mwana chama wa Chadema,tena kiongozi muandamizi ulitaka amuunge mkono mgombea wa CCM?
 
Lisemwalo lipo na kama halipo laja.

Kuweni na subra tu mtaona mengi

Wewe ukishakula mirungi yako na nyama ya nguruwe unakurupuka tu, yeye mwenyewe amesema kuwa hagombei unachong'ang'ania nini?
 
Zito hapa umenena, jaribu kukanusha haya mambo kama kiongozi wa Chama
 
Magazeti kama ya majira, uhuru, habari leo, mi napendekeza fedha za kuyaendesha haya magazeti wangepewa wanafunzi wa vyuo vikuu ili kupunguza tatizo la mikopo, kwani magazeti haya yanaandika upupu 2 wa kimamluki.

Jamba Leo Je?
 
Mkuu kiranga,
Zitto Kuandika kwenye face book yake sentensi ' sitagombea urais 2015, nitamuunga mkono mgombea wa chadema' ni malumbano au ni kuweka ukweli hadharani?

Hongera zitto kwa kuwakatia wabaya wetu mzizi wa fitina, sasa wakatafute hoja nyingine. You are very correct. Big up, mimi najua wewe unachosema ni kweli. Mengine ni speculation.
 
Mimi kitambo tu sisomi gazeti la majira. R.I.P Regia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…