Zimbabwe yauza Tembo wake China

Zimbabwe yauza Tembo wake China

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
16,654
Reaction score
18,800
Zimbabwe inasema inahitaji fedha kukabiliana na uwindaji haramu, lakini mashirika ya kutetea maslahi ya wanyama yameghadhabishwa na hatua hiyo.

Waziri wa mazingira Zimbabwe amesema tembo hao walisafirishwa kwa ndege hadi China kwenye ndege binafsi ya mizigo. Wahifadhi wanyama wanasema tembo wanahitaji uangalifu wa miaka kadhaa kutoka kwa wazazi wake na kwa hivyo kuwatenganisha tembo hao wadogo kutoka jamii zao katika umri mdogo ni kitendo cha ukatili na kitakacho kuwa na athari kubwa kwa wanyama hao.

Tembo hao wataishi katika mbuga ya wanyama karibu na mji uliopo kusini - Guangzhou. Inasemekana kwamba wanyama katika mbuga hiyo wanateswa na kuwekwa katika mzingira mabaya.

Raia wengi wa Zimbabwe wanaona tembo kama wanyama waharibifu wanaoharibu mazao na kuangusha miti.



Source:
bbcswahili
 
Bora tu wakapumzike huko na kula raha kwa Wachina, Waafrika ndivyo tulivyo.
 
Inaonyesha Wazimbabwe bado hawajatambua umuhimu wa kuwahifadhi hawa wanyama waliojaliwa na mwenyezi Mungu.
 
Baada ya miaka 10 utasikia China ndio inaongoza kuwa na tembo wengi Duniani
 
Mmesahau Ndege ya Uarabuni iliyosheheni kila aina ya wanyama toka Tanzania.

Tanzania mnajua ni wanyama wangapi wanasafirishwa kwa njia za magendo kila siku.

Bora wao wameuza kihalali serikali imefaidika.
 
Back
Top Bottom