Zimbabwe yashutumiwa kukiuka haki za binadamu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Vikundi vya haki za binadamu nchini Zimbabwe vinasema serikali imekuwa ikikiuka haki za kimsingi za watu tangu kuanza kwa ugonjwa wa COVID-19. Vikundi hivyo viliwasilisha uchunguzi wao katika mkutano wa njia ya mtandao na maafisa katika mji mkuu Alhamisi.

Katika mkutano huo, vikundi vya haki viliwasilisha ripoti wanayoiita Athari za COVID-19 juu ya Haki za Kijamii na Kiuchumi. Ripoti hiyo inaelezea jinsi serikali ya Zimbabwe ilivyokiuka haki za binadamu tangu kufungwa kwa shughuli za kiuchumi kutokana na COVID-19 kuanzia Machi 2020.

Calvin Fambirai, mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Madaktari wa Haki za Binadamu wa Zimbabwe, alikuwa mmoja wa wasemaji. Anasema janga la COVID-19 liliangazia pengo la huduma ya matibabu kati ya wenye nacho na wasio nacho nchini humo.

Mara kadhaa, madaktari na wauguzi wa Zimbabwe wamegoma, wakidai vifaa vya kutosha vya kinga na mishahara bora wakati wa janga la corona.

Naome Chakanya, mtafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Kazi na Maendeleo ya Uchumi ya Zimbabwe, alisema serikali lazima iongeze mishahara ya wafanyakazi wake wote ili kuwahamasisha.

Serikali ilitangaza kufilisika kila wafanyakazi wake walipoomba kuangaliwa upya kwa mishahara yao. Watumishi wa serikali nchini Zimbabwe hupata chini ya dola 200 kwa mwezi. Mishahara ya wafanyakazi iliongezeka hadi angalau dola 500 kwa mwezi kupita kiwango cha umaskini.

Siku ya Alhamisi pia, Sibongile Mauye wa Tume ya Jinsia Zimbabwe alisema visa vya mimba za utotoni vimeongezeka kwa sababu watoto hawaendi shule na wanabaki majumbani mwao.

Vikundi vya haki nchini Zimbabwe hapo awali vilishutumu serikali kwa kutumia vizuizi vya COVID-19 kukandamiza haki za raia.

Wanaharakati kadhaa walikamatwa kwa mashtaka ya kupuuza kanuni za kubaki majumbani baada ya kuandamana dhidi ya serikali kushindwa kuwasaidia wale walioathiriwa na vikwazo.

Erick Mukutiri, katibu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Zimbabwe, alisema shirika lake linajua malalamiko yaliyotolewa na vikundi vya haki wakati wa kufungwa kwa shughuli za kiuchumi.

Mukutiri aliahidi kutochukua hatua yeyote Alhamisi, akisema tume hiyo inafuatilia hali hiyo.

Zimbabwe ina kesi 38,191 zilizothibitishwa na vifo 1,565, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, kinachofuatilia maambukizi ulimwenguni.

VOA Swahili
 
Rais wao wa sasa hivi unaweza kusema bora Babu tena maana ameenda kununua chopa ya kisasa Urusi kwa ajili ya kampeni kipindi cha Uchaguzi kwa sababu ya bara bara nyingi mbovu ila unaambiwa katumia mamilioni ya dollar kwa ajili ya hiyo chopa...Zimbabwe Kuna shida aisee hatari wauguzi maeneo mengine wanatumia matoroli kama ambulance inaumiza sana kwa kweli Afrika ikipolomoka ila huko Hwange wachina wapo na migodi kama kawaida...
 
Back
Top Bottom