Zimbabwe: Rais Mnangagwa azindua shamba la bangi

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,992
10,497
1655278318457.png
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amezindua shamba la bangi kwa ajili ya dawa lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 27.

Shamba hilo limewekewa kiwanda cha kisasa cha usindikaji ambacho bangi yake itatumika kama suluhisho la matibabu ya kibaolojia na bidhaa za dawa katika soko la ndani na la kimataifa.

Mradi huu ni kwa ushirikiano na Serikali ya Uswizi kupitia kiwanda cha Swiss Bioceuticals na Serikali ya Zimbabwe.

Rais Mnagangwa amesema kuwa ushirikiano huo unaonyesha imani ya Uswizi katika kuwekeza ndani ya uchumi wa Zimbabwe huku akisema kuwa taifa hilo la Ulaya tayari limeshirikiana na Zimbambwe katika miradi mingine kama vile viwanda, usindikaji wa chakula na ujenzi wa taasisi mbalimbali
 
Mama yenu anapaswa kuiga vitu kama hivi, bangi inavumilia hali mbaya ya hewa, itaongeza ajira, itaongeza pato la kigeni, itafacilitate ujenzi wa viwanda nchini.
 
Ni mradi mzuri sana kiuchumi, majani yanatumika kama mboga na dawa. Hebu bunge lijadili hili jambo kwa makini.
 
Mama yenu anapaswa kuiga vitu kama hivi, bangi inavumilia hali mbaya ya hewa, itaongeza ajira, itaongeza pato la kigeni, itafacilitate ujenzi wa viwanda nchini.
ukiiruhusu kulimwa ruhusu na kuitafuna kupiga msuba🚭🚭
 
Ukiwa unapandisha kutoka Ngorongoro Crater miti ya Bangi na Mirungi imejazana pembezoni mwa barabara ila kutokana na ile steepness ya mpando sio rahisi kusimama na kuchuma
 
Back
Top Bottom