Zimbabwe kuchapisha dola ya Marekani kukabiliana na ukosefu wa pesa

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,188
10,668
4bk145b4925aa02jeu_800C450.jpg


Benki Kuu ya Zimbabwe imetangaza kuwa nchi hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa fedha za kigeni na hivyo itachapisha dola sawa na ile ya Marekani kukabilinaa na hali hiyo.

Katika taarifa, benki kuu hiyo ya Zimbabwe imesema kutumia sarafu za nchi kadhaa kama fedha rasmi za mabadilishano nchini humo ni jambo ambalo halijawa na matokeo mazuri na kwa msingi huo nchi hiyo imeamua kutumia sarafi moja, yaani dola ya Marekani iliyochapishwa nchini humo. Hivi sasa nchini Zimbabwe kunatumika rasmi sarafu za kigeni za Euro, Dollar ya Marekani, Yuan ya China, Pauni ya Uingereza na Rand ya Afrika Kusini. Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mangudya amesema benki hiyo itachapisha dola ambayo itakuwa na thamani sawa na ile ya Marekani lakini iliyochapishwa Zimbabwe.

Mwaka 2000 Zimbabwe ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa na hivyo kupelekea wakuu wa nchi hiyo kuchukua hatua kadhaa kama vile kufuta sarafu ya dola ya Zimbabwe na mahala pake kuchukuliwa na sarafu za kigeni zilizotajwa mwanzoni.

Kwa mujibu wa ripoti ya 'Utajiri wa Afrika Mwaka 2016' ambayo imechapishwa na tovuti ya 'utafiti wa masoko', raia mmoja wa Zimbabwe kwa wastani ana pato la dola 200 kwa mwaka na hivyo kuwafanya Wazimbabwe kuwa kati ya watu masikini zaidi Afrika.

Hali mbaya ya kiuchumi Zimbabwe inajiri huku Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Watoto UNICEF ukitoa taarifa na kuonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na baa la njaa na kwamba iwapo hatua za lazima hazitachukuliwa, basi kutaibuka maafa ya njaa na lishe duni katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Jane Muita, mwakilishi wa UNICEF Zimbabwe anasema nchi hiyo inakabiliwa na hali mbaya zaidi ya lishe duni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita. Amesema hivi sasa watoto 33,000 Wazimbabwe wanakabiliwa na lishe duni. Muita ameongeza kuwa, ingawa serikali na taasisi kadhaa zinajitahidi kutatua mgogoro uliopo, lakini hatua zaidi zinahitaji kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo lililopo.

UNICEF imeongeza kuwa, kupungua mazao ya kilimo mwaka huu kumepelekea Wazimbabwe wengi kukumbwa na njaa na lishe duni.

Mashirika ya kutoa misaada yanasema tukio la El Nino la mwaka huu ni baya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Aidha ukame wa miaka miwili mfululizo ni jambo ambalo limepelekea karibu watoto milioni moja kusini mwa Afrika kukabiliwa na tatizo sugu la lishe duni.

Hivi karibuni Zimbabwe iliomba msaada wa dola bilioni 1.6 kununulia nafaka na bidhaa zingine za chakula. Pamoja na matatizo hayo ya Zimbabwe, tatizo jingine nchini humo ni ufaisadi na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma.

Shirika la kimataifa la kupambana na ufisadi, Transparency International, katika taarifa yake ya mwaka 2015 kuhusu namna ufisadi unavyoathiri vibaya watu Afrika lilisema ufisadi uliopo Afrika ni mkubwa na hauwezi kuvumiliwa tena.

Shirika hilo lilitaja nchi zinazoongoza kwa ufisadi Afrika kuwa ni pamoja na Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Libya, Guinea Bissau, Angola, Burundi na Zimbabwe.

Matatizo ya kiuchumi ya Zimbabwe yalianza mwaka 2000 wakati Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo alipoanzisha mpango wa kurekebisha umiliki wa ardhi . Katika mpango huo serikali iliwapokonya Wazungu ardhi walizokuwa wameziteka wakati wa ukoloni na kuzikabidhi kwa Waafrika wazalendo.

Aghalabu ya ardhi hizo zilikuwa ni ardhi nzuri za kilimo. Kufuatia mpango huo karibu Wazungu 4,000 walitimuliwa Zimbabwe. Tatizo lililofuata ni kuwa, waliopewa umiliki wa ardhi mpya walikuwa hawana ujuzi wa kilimo cha mashamba makubwa na pia hawakuwa na uwezo wa kifedha wa kusimamia mashamba hayo.

Kwa msingi huo Zimbabwe ikaanza kushuhudia ukosefu mkubwa wa mazao ya kilimo hasa nafaka. Tokea wakati huo kilimo cha Zimbabwe kimedidimia na kuibadilisha nchi hiyo kuwa kati ya nchi masikini zaidi Afrika.
 
Nchi inahitaji akili mpya na sera mpya kuweza kufufua uchumi wao,
Kutwa anawatukana wazungu leo anataka kutengeneza pesa ambayo kuanzia Jina la wazungu mpaka thamani anataka iwe kama wazungu, kweli baniani mbaya kiatu chake dawa
 
Nchi inahitaji akili mpya na sera mpya kuweza kufufua uchumi wao,
Kutwa anawatukana wazungu leo anataka kutengeneza pesa ambayo kuanzia Jina la wazungu mpaka thamani anataka iwe kama wazungu, kweli baniani mbaya kiatu chake dawa

Hao ndio viongozi wetu wa Kiafrika.
 
dola ya kimarekani haiwezi kuwa sawa na ya Zimbabwe kwa kuchapisha tuu...Mugabe apumzike tuu
 
Back
Top Bottom