Zimbabwe bila Mugabe inawezekana

Zimbabwe bila Mugabe inawezekana

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,751
Reaction score
17,240
Heri mugabe awarithishe vijana uongozi Wa nchi Yao mapema na yeye abaki kuwa baba Wa taifa na mshauri Wao mkuu Kama walivyofanya Nyerere, Mandela, Moi, Kaunda, chisano, nk. Mugabe hâta akifa Zimbabwe inapaswa kubaki salama bila yeye kuwepo pia. Viongozi Wa Afrika kushirikiana na viongozi wanaong'ang'ania madarakani Kama hawa inalipotezea hadhi bara la Afrika. Kung'ang'ania madarakani, kuwaibia wananchi na kushindwa kutatua kero za wananchi ni mbaya zaidi kuliko viongozi wa Kiafrika kushitakiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC). Mimi nilikuwa miongoni mwa watu waliofurahia Bw. Mugabe kutwaa mashamba ya walowezi na kuyarudisha kwa kwa wananchi waliokosa ardhi, lakini sasa siungi mkono hili la kutaka kuwa rais wa maisha wa Zimbabwe au la kutaka kuacha kiti kwa familia yake. Marafiki wa Zimbabwe na Mugabe mko wapi?

Kama kuna rafiki mzuri Wa Zimbabwe asimame na kumshauri Mugabe ang'atuke na kuwajenga vijana wazoee uongozi chini ya uangalizi Wake. Hii ni pamoja na marais wengine Afrika wanaodhani kuwa bila wao nchi zao haziwezi kuwepo.
 
Viongozi kama Mugabe hawashauriki Mkuu! Anataka kifo ndicho kimtoe! Ingekeuwa vizuri kama the so called first lady wake 49 yrs old, Grace amshauri aachie ngazi tu. Lkn inaweza kuwa ajabu kwani kuacha tabia hii ya kushikiria madaraka as if hakuna wengine. Mkuu inabidi tujifunze kitu fulani kutokana na katabia hako hasa kwa hapa TZ!
 
Back
Top Bottom