Zimamoto show ya madawa kulevya sasa basi, turudi kwenye anguko la uchumi wetu

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,027
Hakuna mzalendo halisi wa nchi hii anayepinga vita dhidi ya madawa ya kulevya. Nasema boldly hakuna!

Ni vita iliyotakiwa ianze kupiganwa miongo kadhaa iliyopita lakini kwa sababu zisizoeleweka au kuelezeka hakuna cha maana kilichofanyika muda wote huu hadi hapa majuzi baadhi ya wanasiasa walipoamua kuianzisha kwa mtindo wa zimamoto.

Sote tunajua kuwa approach yoyote ya zimamoto huwa haina tija endelevu - hata propagators wa approach hii pia wanalitambua sana hilo. Kwa maana hiyo, wanapoamua kuitumia njia wanayojua fika kuwa haina tija, tafsiri rahisi ni kuwa lazima kuna ulterior motives behind it. Kwa haya yaliyotokea hivi karibuni kuhusiana na style iliyotumika kwenye vita hii, kuna nadharia nyingi zimeibuka kuzieleza hizo "ulterior motives". Sina haja ya kuzirudia hapa kwani siyo lengo la kuanzisha hii thread.

Nchi yetu inapita katika kipindi ambacho hali ya uchumi ni tete. The problem is real, brethren. Hili pia halina ulazima wa kulijadili kwani ni ukweli ambao ni dhahiri kwa sisi sote. Kwenye micro level, pesa mtaani hakuna na familia nyingi zinaishi kimungumungu. Kwenye macro level, miradi mingi muhimu ya serekali ime-stall, huku sekta ya fedha ikiendelea kusinyaa. Mifano ipo na mingi imeongelewa kwenye media mbalimbali.

Going forward?

Nashauri mihimili ifuatayo, kwa kutumia platform zao, ijikite sasa katika kuihanikiza serekali ili ichukue hatua za makusudi ku-reverse trend ambayo inaweza kupelekea anguko la jumla (ultimate meltdown) la uchumi wetu:

1. Bunge:
Chombo hiki kiunde haraka tume maalumu ya kibunge. Tume hii, baada ya kufanya consultation na magwiji na wadau wengine kwenye eneo la uchumi, iwasilishe mapendekezo ya kuirudisha serekali kwenye mstari. Suala la serekali kuyapokea mapendekezo au la lisiwe kikwazo kwani bunge litakuwa limetekeleza wajibu wake vizuri kwa ajili ya mustakabali wa nchi. Sina shaka majina yao yataandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

2. Media (print & electronic):
Kwa nguvu ile ile (ama zaidi) iliyotumika kwenye "zimamoto show" ya madawa ya kulevya, sasa zijielekeze kwenye ku-cover (microscopically & forensically) uhalisia wa madhira yatokanayo na hali tete ya uchumi iliyopo. Ninapotumia expressions za "microscopically & forensically" nina maana kupata na kutoa taarifa zilizotafitiwa na si vinginevyo.

Tukusoe lakini pia tutoe suluhu.

Karibuni.
 
Chama twawala wangekuwa wana uwezo hata kidogo kufikiri hili ingekuwa poa sana

Back
Top Bottom