Zilizala la mwezi Januari na jinsi tunavyoweza kupunguza makali yake

General Akudo

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
560
824
Salaam wana JF,

Daima mwezi Januari ni kipindi kigumu sana kwa mtu mwenye majukumu lakini mara nyingine hata wasio na majukumu hujumuishwa kwa kupigwa mizinga, kukopwa au kusaidia.

Pango la nyumba, kibanda cha biashara, ada za watoto shule, usafiri, sare za shule, michango kibao na nk.

Ushuhuda wangu, 2017 nilifikiri njia ya kupunguza makali ya Januari 2018. nilianza utaratibu wa kuweka AKIBA BENKI, katika mshahara wangu kila mwezi nikaweka standing order kiasi cha 50,000 kiende kwenye akaunti mbili za watoto ambazo hazina makato ya mwezi na hata unapotoa.

Kwa mwaka jumla naweka akiba ya 600,000, hakika niliona unafuu kidogo Januari ya 2018.

Mwaka 2018 niliendelea na zoezi hilo kwa ajili ya januari 2019. Mwaka huu 2019 nikachukua mkopo binafsi benki na kwenye Saccos nikajenga kajengo kwa kujihifadhi, nikifikiri maisha haya unaweza kurest in peace unaacha familia nyumba ya kupanga.

Kwahiyo nilifanikiwa 2019 kujenga kijumba kidogo ambacho hakijaisha kiasi cha kuvutia macho lakini naishi humo hivyo hivyo. Hatua hii imenibana kiasi maisha maana kila mwezi rejesho kubwa kuliko ile kodi nilikopanga sema sio mbaya nalipa pango kwenye nyumba yangu.

Sasa Januari 2020 nadaiwa ada tu na vitu vingine vya hapa na pale. Mkopo Saccos nitamaliza katikati ya mwaka 2020.

Mwaka 2020 malengo yangu ni kufungua biashara ambapo haitakuwa mara ya kwanza maana nishawahi fungua biashara ndogo mara mbili nikafunga kwa sababu mbalimbali, ikiwemo mzunguko wa biashara kuwa mdogo na kukosa uwezo wa kustahimili na biashara kipindi cha mpito.

Ushauri wangu wadau tuwe na utaratibu wa kujiwekea akiba, tusiwe na visingizio wewe anza kuweka Mungu atakusaidia.

Mkopo wa Bodi ya Elimu ya Juu ukiisha nitaongeza kiasi cha akiba kufikia 100,000 kila mwezi lengo kupunguza hekaheka Januari maana ni hatari.

Hasara humfika mwenye mabezo
 
Back
Top Bottom