ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Balantanda (PhD)!

By virtue of the authority vested in me by JF, I hereby confer upon you the Honorary Degree of Doctor of Music.

Congratulations!

Dr. Balantanda amenikumbusha mbali. Miongoni mwa nyimbo nazopenda sana ni "Ni wewe pekee" wa Nguza Viking/Marquis na Jack wa Nico Zengekala. Nikisikiliza nyimbo hizi nahisi mapigo ya moyo yanabadilika.

Single ya Alikiba, "Usinisemee kama napenda kula" tutaisikiliza kweli?
 
washirika tanzania stars watu njatanjata,super matimila,tancut almasi,mk group,maquiz du zaire,ruaha international na jkt mafinga wana kimulimuli
 
Si wewe tu mkuu wangu,kila mtu akizikumbuka bendi kama Marquis(wana sendema,zembwela n.k),Sambulumaa,Vijana Jazz(pambamoto),Washirika Tanzania Stars(watunjatanjata,njata one),Tancut Almas(wana fimbo lugoda,kinyekinye kisonzo tisa kumi mangala),JKT Mafinga(kimulimuli),JKT Kimbunga stereo,Ngorongoro Heroes Band(sukuma push),Kurugenzi Jazz,Six Manyara,Bima Lee(Magnet tingisha),Super Matimila(Bongo beats,talakaka),Zaita Musica(wana zuke muselebende),MK Group(wana Ngulupa tupatupa dansi),MK Beats(wana tukunyema,wowowo),MK Sound,OSS(wana masantula ngoma mpwita,dukuduku,ndekule,power Iranda,rashikanda wasaa),MCA Internationa(wana munisandesal,Orch. Makassy,Magereza Jazz(Mkote Ngoma),Bicco Stars(wana kindumbwe ndumbwe),Super Rainbow,Bantu Group Band(wana kasimbagu kaabuka),Legho Stars(wana sopabango),Afriso International ya Lovy Longomba na nyingine nyingi lazima utatokwa chozi mkuu,kifo cha bendi hizi ndio kifo cha muziki wetu ule mtamu tulioupenda,haupo tena.......Nyingi kati ya bendi hizi zimekufa na zilizopo zinajikongoja........Natamani kuurudisha wakati nyuma aisee....

Kuhusu Super Stereo Hassan Rehani Bitchuka,kwa sasa yupo Mlimani Park orch wana Sikinde ambako alihamia akitokea Msondo Ngoma....

Dukuduku eeh!!
"Mara ya kwanza umeniomba tucheze,
Muziki wa kwetu siwezi kukataa,
Mara ya pili ukarudia tena,
Sio kwa kucheza ila kunifinya jicho,...

Uliza kwanza, kabla ya kufanya upuuzi wako bwana eeh, mimi nimeishaolewa...
Nimekuja kucheza, nimekuja kufurahisha mwili bwana eeh....

Dr Balantanda, hebu lete lyrics za huo wimbo bwana..,
 
Dr. Balantanda amenikumbusha mbali. Miongoni mwa nyimbo nazopenda sana ni "Ni wewe pekee" wa Nguza Viking/Marquis na Jack wa Nico Zengekala. Nikisikiliza nyimbo hizi nahisi mapigo ya moyo yanabadilika.

Single ya Alikiba, "Usinisemee kama napenda kula" tutaisikiliza kweli?

Aah, Jackie, mtoto wa Nairobi.

Mkuu zile zilikuwa nyimbo bwana.
Sio haya mabongo fleva, vijana wanajaza majina ya wauza chips kwenye wimbo mzima. Ha ha ha.

Kulikuwepo na Orchestra Tomatoma, walikuwa na kibao cha "Mwanaidi" nao walikuwa wametulia, sijui hata walifia wapi.
Juwata nao waliwahi kuwa na kibao kama Ashibae (sina uhakika na spelling) na hasira hasara vilitamba sana miaka ya 84/85.

Hakuna duniani, mizani,
Iwezayo kupima kiwango cha mapenzi yangu na wewe mama,
Ashibae..
 
Dr. Balantanda amenikumbusha mbali. Miongoni mwa nyimbo nazopenda sana ni "Ni wewe pekee" wa Nguza Viking/Marquis na Jack wa Nico Zengekala. Nikisikiliza nyimbo hizi nahisi mapigo ya moyo yanabadilika.

Single ya Alikiba, "Usinisemee kama napenda kula" tutaisikiliza kweli?

Nico Zengekala(R.I.P) pamoja na kilema chake cha upofu alikuwa habari nyingine mkuu,angalia mashairi ya nyimbo hizi utaona maana ya ninachokisema ama ulichokisema wewe hapo juu...

Jackie...


Mtoto Jackiee,mtoto wa Nirobi
Ingawa ni mara ya kwanza mimi nawe Jackiee
Tulipokutana palee Kampala kwenda Nairobi
Tulifurahiana sana kama tuliishi mwaka
Tabia yako njema kweli sitoisahau.

Mtotoo Jackie,mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi ukielekea Nairobi nyumbani eeh
Lakini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh

Mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi,ukielekea Nairobi nyumbani eeh
LAkini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh

Kiitikio:

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau lakini nashindwa
Hasa ni ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Nimejaribu kukusahau lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua eeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau lakini nashindwa
Hasa ni ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Nimejaribu kukusahau lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua eeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Sauti yako nyororo inaniua sana na mwendo wako wa maringo unanikondesha mamaaah,ayoleli mwanamama nakuwinda sana Jackie yeyeyeeeh mwanamamaah aeaeeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Mvumilivu hula mbivu,Jacki yeyeeeh,mvumilivu hula mbivu Jackie yeyeeeh
Jaribu kuvumilia yeeh tutaonana mamaah kama sio Kampala ni Tanzania mamaa
Jackie yeyeyeeh mwanamama aeaeeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU



Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Nitakuja Nairobi eeh nikuone mamaah
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Tutafurahi pamoja mi na wewe mama yeeh
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Jackie yeyeyeeh Maneno sema na yeye
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi

ama kitu Solemba

Solemba solemba solemba aaaaaaaaaah

Sitakuwa nikifika nyumbani kwako,aibu nilopata ni kubwa sana,
Ahadi nilopewa ilivunjwa oooh ooooh hata bila kosa,
Ulinipa ahadi tukutane kwenu,nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi oooh ooh na dharau tele,

Ungenieleza ukweli Solemba,kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi oooh ambayo si ya kweli,
Ungenieleza ukweli Solemba,kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi oooh ambayo si ya kweli,

Bridge

Ulinipa ahadi tukutane kwenu,nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi oooh ooh na dharau tele,
Ungenieleza ukweli Solemba,kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi oooh ambayo si ya kweli,

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Ulinikana mbele za watu ati hunifahamu,
Ndugu zako na marafiki walianza kutoka nje,
Waliponiona ni mimi,walishangaa sana mama,
Mbona hivyo solemba mama eee

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Nilikuuliza mbona ulinitendea hivyo Solemba,
Ulisema mimi hujipendekeza kwako tena sana,
Na kuwa hunipendi,nakusumbua bure mamaa,
Mola yupo Solemba,Eloi yupo mamaa.

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Nilichomwa na jua toka asubuhi,
mpaka saa nane Solemba,Sababu ya kukungoja wewe
Kumbe ulikuwa ndani,unachungulia dirishani,
Huna huruma Solemba,I shall never forget you mamaa,

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Sikutaki tena,sina haja nawe,
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakayembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,nimeshituka solemba.

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Lalala lalala lalala lalalalala
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakayembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,lololo lolololo mama lo

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
 
Aah, Jackie, mtoto wa Nairobi.

Mkuu zile zilikuwa nyimbo bwana.
Sio haya mabongo fleva, vijana wanajaza majina ya wauza chips kwenye wimbo mzima. Ha ha ha.

Kulikuwepo na Orchestra Tomatoma, walikuwa na kibao cha "Mwanaidi" nao walikuwa wametulia, sijui hata walifia wapi.

Mwanaidi-Orch. Tomatoma wana 'tambatamba'

Nimetokea kumpenda binti Mwanaidi

nimeridhishwa na tabia yake
nikaamua tufunge nae pingu za maisha
urithi ulioacha baba niliutumia
ili kuneemesha ukoo wake
nilianza kuuza mifugo
hatimaye shamba
ili kumtosholeza mahitaji yake ehhh

baada ya miezi michache nikapata barua kutoka kwa Mwanaidi
..... .. kuwa yeye hanitaki tena
tena hawezi kuolewa na mimi

(wote)
mimi najuta eh najuta mama
gharama nilizogharamia
ameona bure
sijui la kufanya .. nasikitika oh
sababu yako ....... Mwanaidi x 3
 
Nakumbuka kulikuwa na bendi ya Chezimba ilikuwa inapiga Twiga Hotel samora...wimbo wao maarufu "Kijongoo sina nyumba..."
Then kulikuwa na bendi nyingine ikiitwa Bene Bene, Jambo Stars....Of course Tanzanites na wimbo wao "KIdude"
 
Nakumbuka kulikuwa na bendi ya Chezimba ilikuwa inapiga Twiga Hotel samora...wimbo wao maarufu "Kijongoo sina nyumba..."
Then kulikuwa na bendi nyingine ikiitwa Bene Bene, Jambo Stars....Of course Tanzanites na wimbo wao "KIdude"

Hahaaaaa,umenikumbusha mbali sana mkuu wangu......Chezimbaaaa......Dah,

'Kijogoro sina nyumba ee,nitajenga barabarani,nitajenga nyumba ya mawe ee,ghorofa ndani kwani,nitangoja manowari ee,ikipita barabarani'...

Hivi mkuu una habari kwamba Chezimba ilikuwa ikimilikiwa na Hoteli ya Kilimanjaro?,

Hapa pia kulikuwa na vichwa kama Zahir Ally Zorro na vijana wanaochipukia enzi hizo kama akina Hamis Kayumbu(Amigolas wa Twanga),Ally Choki Lwambo,Mwinjuma Muumini,Adam Bakari 'Sauti ya zege',Charles Mhuto na wengine....

Kwa upande wa Tanzanites wao naona bado wapo japo si kwa chati ile ya kipindi kile,wao kwa sasa wanapiga miziki ya zamani ya kukopi,wanapiga zaidi mahotelini......Nafurahi kuona mkongwe John Mhina anaendelea kukomaa mpaka sasa.....

'Nimeinama nimeinuka nimeokota kidudeeee'..........'Pajero pajero linanichengua'...........Hahahaaaaaaaaaaaaa,zamani ilikuw raha jamani...
 
Pia ilikuwepo bendi ya Tancut Almasi,bendi hii ilikuwa inamilikiwa na kiwanda cha kukata almasi kilichokuwa mkoani Iringa na ilikuwa ni mojawapo ya bendi za mikoani zilizokuwa na makali kweli(kama jirani zao wa JKT Mafinga wana Kimulimuli chini ya Zahir Ally Zorro na Kurugenzi ya Arusha).....Tancut Almasi walikuwa wakitumia mtindo wa Fimbo Lugoda na Kinye kinye Kisonzo,tisa kumi Mangala.......

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Samahani ya uongo,Pili wangu,Butinini,Ngoma za Afrika,Helena mtoto wa Arusha,Masikitiko,Lutandila,Safari siyo kifo na nyingine nyingi tu tamu...

Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Kalala Mbwembwe,Nanah Njige,Nuru Mhina,Kawalee Mutimwana,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Mafumu Bilali 'Bombenga',Shaban Yohana 'Wanted',John Kitime,Akuliake Saleh 'King Maluu',Ray Mlangwa,Mohammed Shaweji,Kibambe Ramadhan,Bakari Buhero,Bdul Mngatwa,Hashim Kassanga na wengine wengi......Bendi hii ilikuwa na hazina ya vipaji kwa kweli.......

Bendi hii ilitamba sana kabla ya kuanza kusambaratika baada ya wanamuziki wake tegemeo akiwemo Kalala Mbwembwe,Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga kuanzisha bendi nyingine hapohapo Iringa ya Ruaha International ambayo ilitamba sana na wimbo wa Lutandila namba 2 Safari (Safari safari safari kweli tabu,naomba kwa Mungu baba nifike salama,safari yangu mieee,safari ya Zimbabweee............ulikuwa wimbo mtamu kweli jamani).....

Bil kuvisahau vibao kama Mama,Tutasele, Mbuguswa na Masafa mrefu...

Hivi mnkumbuka kile kibwagizo cha 'akina mama mwipulikeee,ieeee mwipulikeee........Mbuguswaaaa'
 
Hivi wakuu...........Mbona tunaisahau Bendi ya Sambulumaa?.....Mnawakumbuka hawa jamaa?

Bendi hii ilianzishwa mwaka 1993 na iliundwa na wamuziki wengi wliotoka katika bendi ya Tancut Almas ya Iringa,waasisi wa bendi hii ni pamoja na Kynga Songa,Kasaloo Kyanga,Said Gotagota, Skassy Kasambula,Lister Elia,Nguza Vicking,Freddy Ndala Kasheba,Zahir Ally Zorro,Rahma Shally

Hivi unakumbuka nyimbo kama Kadiri Kansimba,Cleopatra,Dezo dezo,Mama Happy,CCM imekua,Mayombo na vingine vingi.....
 
Kulikuwepo na Orchestra Tomatoma, walikuwa na kibao cha "Mwanaidi" nao walikuwa wametulia, sijui hata walifia wapi.

Nanreen..

Hii bendi ilianza kusuasua baada ya kukimbiwa na wanamuziki wake tegemeo kama akina Kasaloo Kyanga(mtunzi wa wimbo wa Mwanaidi),Kawalee Mutimwana,Abuu Semhando 'Baba Diana/Lukasa'(R.I.P),Skassy Kasambula,Ally Yahaya,Kabaa Balee na wengineo kuondoka ambapo baadhi yao(akiwemo Kasaloo) walienda Arusha kujiunga na bendi ya Kurugenzi ya huko.....Hata hivyo iliibuka upya baada ya kupata wanamuziki wapya kama Francis(Nassir) Lubua, Banza Tax, Mbwana Cox, Saadi Ally Mnara, Adam Bakari 'Sauti ya zege', Huruka Uvuruge na wengine hivyo kufanya bendi hii iibuke upya na kuanza kuwa moto kma ilivyokuwa enzi za akina Kasaloo......
ke
Ukiacha wimbo wa Mwanaidi,wimbo mwingine uliopendwa wa hawa jamaa wa Tomatoma ni wimbo wa Almasi utunzi wake Kasaloo Kyanga(kama sikosei)......
 
Mheshimiwa, kwa kweli nimekukubali.
Najaribu kuukumbuka wimbo wa Almasi, lakini maneno yanakuja halafu yanapotea.

Kulikuwepo na wimbo mwingine naukumbuka, ila nimesahau ulipigwa na nani (labda akina Hemedi Maneti au labda UDA wana bayankata), nafikiri ilikuwa kati ya 80-83.
Baadhi ya maneno yake yalikuwa hivi:

Safiri salama na usalimie wote,
Na ukifika salama nijulishe majibu mapema.

Salaam sana kwa baba, salaam sana kwa mama,
uwaeleze sijambo oh,
Lakini nakonda kwa gubu ya mume.

Jambo dogo kwake kubwa, atasema kutwa nzima,
Na usikuuu hatulali.

Hakina ninachokosa hapa nyumbani.
Kama chakula ninakula mpaka natupa.
Toka vitenge mpaka khanga hazinipiti,
Ila gubu tu la mume.....


Hizo zilikuwa enzi za kusikiliza RTD. Wenyewe tuliridhika na umaskini wetu, tukawa tunafurahia muziki wa dansi.
 
Muziki wa Tanzania hauwezi kukamilika bila kuwataja Msondo Ngoma Music Band.....

Bendi hii ilianzishwa mwaka 1964 na Muungano wa vyama vya wafanyakazi Tanganyika wa wakati huo(NUTA),hii inaweza kuwa ndiyo bendi kongwe zaidi ambayo bado inatamba mpaka sasa kwa nchini Tanzania.Ilianza ikiitwa NUTA Jazz na wanamuziki waanzilishi wanatajwa kuwa ni pamoja na John Simon,Abel Barthazar,Muhidin Maalim Gurumo,Zuberi Makata, Mnenge Ramadhani, Joseph Lusungu, Juma Akida, Ahmed Omari, H.R. Sama,Mohamed Omary, Mabrouk Khalfani,Wilfred Bonifashmed Omary, Mohamed Omary, Epimakus Mkundika, Rashid Abdallah na wengineo......

Bendi hii ilianza mwaka 1964 ikiitwa NUTA Jazz baadaye ikabadilishwa jina na kuitwa JUWATA Jazz Band-JJB (mara baada ya Jumuiya ya wafanyakazi Tanzania kuliweka jina lake katika lugha ya kiswahili na kuwa JUWATA),baadaye tena JUWATA ilibadilishwa jina na kuwa OTTU ambapo ilibidi na bendi ibadilishwe jina na kuwa OTTU Jazz Band,baadaye tena OTTU ilibadilishwa na kuwa TFTU(Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania) ambapo na bendi nayo ilibadilishwa jina na kuwa TFTU Jazz Band(jina hili halikuvutia kabisa ikabidi waruhusiwe kulitumia jina la OTTU),bendi iliendelea kumilikiwa na Shirikisho la vuama huru vya wafanyakazi Tanzania ikitumia jina la OTTU Jazz Band mpaka miaka ya karibuni ambapo Shirikisho hilo lilisema limeshindwa kuiendesha bendi hiyo na kuwapa uhuru wanamuziki wa bendi hiyo wa kuiendesha bendi wenyewe ambapo waliamua kubadili jina na kujiita Msondo Ngoma Music Band almaarufu kama 'Msondo'......Bendi hii imekuwa ikiutumia mtindo wa 'Msondo Ngoma Magoma kitakita' ikiwa ni pamoja na 'kujiita Baba ya muziki'....

Baadhi ya nyimbo zilizotamba za bendi hii tangu ikiitwa NUTA Jazz mpaka sasa ikiitwa Msondo Music Band ni pamoja na Magdalena, Maneno ya Mwalimu, Nipeleke kwa baba, Nimuokoe nani, Viva Flerimo, Maneno ya Wazee Yote Sawa, Rehema Umefeli Shule kwa Kisa Gani, Ashibaye, Bahati, Gloria, Hamida, Sikutarajia kashfa, Mwenzio nateseka, Msondo wa NUTA, Mwana Iddi, Kisomo cha watu wazima, Nakwenda kijijini, Tulia upate mchumba, Nimwokoe nani, Nilikuwa si amini, Asha adabu yako mbaya, Barua nimeipata, Ndugu Zangu Leo Nataka Kuwahadithia, Asha Mbona Wanitesa Dada, Nilipofika Nyumbani kwako Asubuhi, Mbona Hivyo Dada, Bibi, Onyesha Nguvu, Catherina Nilikupend Sana,Mwangele Kanitoa Kwet, Amina Mwacheni Aende, Kaka.....

Nyimbo nyingine ni pamoja na Rudi Mpenzi Zakina, Mwana Acha Wizi, Wazee Wangatuka, Usia wa Baba, Nimekubali Makosa,Nidhamu ya Kazi, Mariam Ninakujibu,Priscilla, Bahati, Kanjelenjele, Siwema, Hasiri Hasara, Solemba, Jackie, Queen Kasse, Penye Penzi Hapakosi Tezi, Belinda, Mama Sanny, Tuma, Ajuza, Mwana Mkiwa, Tupatupa, Binti Maringo, Asha Mwana Seif, Piga ua talaka utatoa, Ndoa ndoana, Mzee wa miiba,Msafiri kakiri, Usia wa baba, Demokrasia ya mapenzi, Nizamu ya kazi na nyingine nyingi tamu za hawa jamaa wa Msondo Ngoma a.k.a JJB Baba ya Muziki,Magoma kitakita.....

Baadhi ya wanamuziki waliowahi kupitia bendi hii tangu ikiwa NUTA Jazz mpaka sasa Msondo Ngoma Music Band ni pamoja na John Simon,Abel Barthazar,Muhidin Maalim Gurumo,Zuberi Makata, Mnenge Ramadhani, Joseph Lusungu, Juma Akida, Ahmed Omari, H.R. Sama,Mohamed Omary, Mabrouk Khalfani,Wilfred Bonifashmed Omary, Mohamed Omary, Epimakus Mkundika, Rashid Abdallah, Ali Kishiwa Mhoja 'TX Moshi William',Hassan Rehani Bitchuka,Shaban Dede 'Kamchape', Hussein Jumbe, Joseph Maina, Athuman Momba, Said Mabera, Suleiman Mbwembwe, Suleiman Mwanyiro 'Computer', Roman Mng'ande 'Romario', Karama Legesu, Ibrahim Kandaya, Juma Katundu,Nico Zengekala 'R.I.P', Shukuru Majaliwa(huyu huwa anachukuliwa mahsusi kuimba nyimbo ya hayati TX Moshi William,yeye ni mwanamuziki wa Mwenge Jazz wana Paselepa).....

Kwa uchache hao ndio Msondo Ngoma Music Band........
 
Vipi kuhusu Dar International Orchestra wana Super Bomboka chini yake Jalbali la Muziki Marijan Rajab.....

Kuna anayewajua hawa?,na atujuze basi.......
 
Vipi kuhusu Dar International Orchestra wana Super Bomboka chini yake Jalbali la Muziki Marijan Rajab..... Kuna anayewajua hawa?,na atujuze basi.......
Mkuu Mzee Marijani (RIP) alikuwa nio kichwa haswa! Moja ya nyimbo nilizotokea kuzipenda ni Mayasa.

Mayasa mbona wanichana mbavu bibie, Sura yako mbona sasa imekuwa hivyo, Nakuuliza mbona hata kunijibu hutaki, Umenikasirikia kama mimi ndio nilikutuma, Sura yako mbona inatisha mama eh, Sio mimi wazidi kunichana mbavu Mayasa oooh...
 
Mkuu Mzee Marijani (RIP) alikuwa nio kichwa haswa! Moja ya nyimbo nilizotokea kuzipenda ni Mayasa.. Mayasa mbona wanichana mbavu bibie, Sura yako mbona sasa imekuwa hivyo, Nakuuliza mbona hata kunijibu hutaki, Umenikasirikia kama mimi ndio nilikutuma, Sura yako mbona inatisha mama eh, Sio mimi wazidi kunichana mbavu Mayasa oooh...

Huyo ndio Jabali la muziki Marijan Rajab na Dar International mkuu...

Marijan Rajab kabla hajahamia Dar International alikuwa katika bendi ya Safari Trippers ambayo ilisambaratika mwaka 1977......Baada ya Safari Trippers kufa nini kilifuata?.....Mwaka huohuo 1977 mwanamuziki mwingine Nguli chini Abel Barthazar alianzisha bendi ya Dar Internatinal ambayo pamoja naye(Balthazar) pia walikuwepo Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,ALi Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......

Bendi hii ilianza kwa kutoka na vibao kama Nyerere mwanamapinduzi,Rufaa ya kifo,Mwana uoe,Betty,Margreth na Sikitiko,....Vibao hiivi vilitamba hasa na bendi ilianza kushika chati ya juu katika medani za muziki wa Dansi Tanzania.....Bendi hii ilikuwa maarufu ghafla na kwa kupitia Marijan Rajab ilipiga muziki wenye mahadhi kama ya ule muziki uliokuwa ukipigwa na Safari Trippers hivyo kuzidi kumletea umaarufu Marijan Rajab kitu ambacho inadaiwa hakikupendezwa sana na wanamuziki wengine akiwemo Abel Barthazar ambao waliona kwamba watu wanaichukulia Dar International kama Safari Trippers....Walianza kumpiga vita Marijan Rajab ambaye hakupendezwa na hali hiyo hivyo kuamua kujitoa katika bendi hiyo(miezi 9 tu baada ya bendi kuanzishwa).....Mwaka 1978 baada ya Marijan Rajab kujiondoa bendi haikudumu sana kwani ilisambaratika baada ya wanamuziki nane(08) tegemeo wa bendi hiyo Abel Barthzar(aliondoka kabla ya wenzie),King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jef waliondoka na kwenda kuanzisha bendi ya Mlimani Park Orchestra(baadae DDC Mlimani Park Orchestra).....

Baada ya bendi kusambaratika,mmiliki wa Dar International Zachariah Ndebame alimuomba Marijan Rajab arudi kwa ajili ya kuisuka upya bendi hiyo ambapo alikubali na kurudi rasmi kwenye bendi,hapo akakutana na mpiga solo Hamza Kasongo ambaye kwa kushirikiana waliiongoza bendi hiyo kutoa vibao vitamu kama Zuwena,Vick na Mayasa......Vibao hivi viliurudisha umaarufu wa bendi hii kiasi cha kuzitisha bendi ilizozikuta zikitamba wakati huo kama Vijana Jazz,Juwata Jazz,Mlimani Park,Marquiz na Biashara Jazz.....Hali hii ilileta ushindani mkubwa miongoni mwa bendi hizo.....Baadae bendi hii ilipata wanamuziki chipukizi kama Fresh Jumbe ,Tino Masinge 'Arawa', Mohammed Mwinyikondo na wengine na kurekodi vibao vitamu kama Mzee Said,Baba Anna,Masudi amekuwa jambazi,Bwana Mashaka,Pondamali kufa kwaja, Mwajuma, Pendo si kulazimishana, Usimtese Mwana, Chakubanga na nyingine nyingi zilizotamba na kufunika ile mbaya enzi hizo.....

Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Bomboka.......Nyimbo nyingine zilizotamba za bendi hii ni pamoja na Mwanameka, Ukewenza, Sababu ya Mapendo, Usia wa Baba, Aisha Mtoto wa Mwanza, Siwema, Mama Maria, Paulina, Mateso ya ndoa, Ponda Mali Kufa Kwaja, Amekosa Nini Mama, Pesa Sabuni ya Roho, Ukatili Ni Unyama, Siwema No. 2, Mwana Acha Kidomo Domo, Mpenzi Christina, Uzuri wa Asali, Ninamsaka Mbaya Wangu, Emmy, Umevunga Ahadi, Alinacha, Nitajirekebisha, Ndugu Umepotea, Baba Anita, Ndugu umepotea No. 2, Pendo, Pombe si chai, Esther, Baruti, Vicky, Uzuri wa asili, Mapambano yanaendelea, Mwana mpotevu na nyingine nyingi...........

Hao ndio Dar International Orchestra wana Super bomboka chini yake Jabali la muziki Hayati Marijan Rajab(R.I.P)......
 
thanks balantanda, umenikumbusha mbali sana enzi za utoto. especially huo wimbo wa nikitazama milima ya kwetu. i wish ningepata walau audio yake. na wimbo wa kalubandika, huu naweza kuusikiliza kwa repeat mode hata 5 times! sijui nani aliimba ila unanikumbusha nikiwa kinda, naskiliza radio tz,lol
 
Back
Top Bottom