Uchaguzi 2020 Zile kampeni za kupokea wanachama wapya na kuchoma kadi zimeishia wapi?

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Kampeni za mwaka huu zina utofauti mkubwa sana na kampeni za vipindi vilivyopita.

Zamani muda kama huu tungekuwa tukishuhidia wanachama toka vyama mbalimbali wakijiunga na vyama vipya kwa kurudisha kadi upande wa pili ili kunogesha mikutano ya viongozi na wagombea.

Lakini mwaka huu mambo yamebadilika sana. Kila kona tungeshuhudia vituko vya kila aina lakini mpaka sasa hakuna vituko.
Hata vyombo vya usalama hasa hasa Polisi nao wamekuwa na weledi uliopitiliza kwani sijasokia mabomu ya machozi kuunguruma kokote ama mikutano na maandamano kutawanywa.

Ama kweli mwaka huu ni uchaguzi wa tofauti kabisa. Miaka ya nyuma wakati kama huu akina comrade Mwigulu Chemba, Nape Nauye Mzee Kinana, Mangula,Makmba Jr na Sr wote wangekuwa wakichachafya kona za nchi hii. Cha kushangaza kama kazi hii kaachiwa Polepole peke yaku huku katibu mkuu Bashiru Ally akiingia kwa ku beep.
Hata mawaziri wasio na majimbo ya kugombea kama akina Angela Kairuki nao siwaoni kabisa. Mzee Bulembo nae sijui kastaafu siasa hata sijui. Aliyekuwa mbunge wa Sengerema bwana Ngeleja nae kapotea, Sumaye simwoni. Kuna vionjo kwenye uchagizi wa mwaka huu tumevikosa
 
Back
Top Bottom