Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 976
Wanabodi,
Mahudhurio ya wananchi kwenye Mikutano ya Kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu (2020) haiwezi kuwa sababu ya moja kwa moja ya ushindi Ila angalau yanatoa picha ya mambo yatakavyokuwa.
Siasa za duniani kote, hata Marekani, idadi ya watu wanaohudhuria Mikutano ya Kampeni huchukuliwa kuwa moja ya kigezo cha kukubalika kwa chama cha siasa na mgombea/wagombea wake.
Katika kampeni zinazoendelea, tumeshuhudia mahudhurio machache kwa vyama vya upinzani ukilinganisha na mwaka 2015. Pamoja na kuwa sio kigezo cha moja kwa moja Kama nilivyotangulia kuandika hapo juu, lakini kuna uhusiano chanya. Mfano halisi tunauona kwenye motokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Motokeo yaliendana na mafuriko, hivyo kigezo hicho ni muhimu na kamwe hakiwezi kuepukwa.
Nilipata kusema mahali fulani kuwa "siasa ni sayansi na wanasayansiasa wazuri hufanikiwa sana". Ninawashangaa sana wapinzani wanaposema kuwa "mafuriko ya watu kwenye kampeni za CCM wanafuata wasanii". Hili halikupaswa kuongewa na watu wanaojua siasa. Lazima unogeshe mkutano kwa vionjo mbalimbali. Hivi hawajifunzi kwenye mikutano ya injili ambapo kunakuwa na "sebene la Yesu"?. Kuna wale wanakuja kufuata sebene, wanawake na kuibia wahudhuriaji. Wakifika pale wanakutana na faya. Vivo hivyo, mwananchi anaweza kwenda kwenye kampeni za CCM kuona wasanii lakini akifika pale anapata yote, burudani na kusikiliza sera. Hii imetusaidia sana.
Mtu asipofika kwenye mkutano wako, atafanyaje maamuzi ya kukuchagua? Kijana anasikia nini kimepangwa kwa ajili yake, vivo hivyo kwa akina mama wazee, walemavu na makundi mengine.
Ukiacha ukubwa wa chama, umaarufu wa mgombea nao una nafasi kubwa sana. Umaarufu wa Lowassa haufanani hata kiduchu na umaarufu wa Lissu au Membe. Lowassa wa 2015 alikuwa Ni "man and a half". Lissu anatumia vibaya shambulio lake kutaka kura za huruma. Kipekee, nalaani kushambuliwa kwake lakini kupigwa risasi haiwezi kuwa kigezo cha kuchaguliwa. CHADEMA kwa hapa mmekosea sana. Watanzania wanataka maji, umeme, huduma bora za afya, elimu na miundombinu bora.
Mahudhurio machache ya wananchi ni salamu kwenu. Hiyo ni rasharasha, masika inakuja. Sasa mnaanza kutumia picha za mafuriko ya Lowassa mkizani hatujui. Watanzania wa leo "HAWADANGANYIKI". Wamemuelewa Dr John Magufuli, wameilewa CCM.
Tukutane oktoba ishirini na nane
Amani Msumari
Tanga