Ziko wapi bustani za wazi Dar?

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,016
2,194
upload_2016-1-20_11-43-3.png


Kwa ufupi
Mbali na kupamba mji, bustani za wazi zinafanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa sehemu ya mapumziko kwa watu mbalimbali wenye msongo wa mawazo na wageni wanaoingia katika mji fulani kwa shughuli zao.
=====

Moja ya vitu vinavyopamba mji ni pamoja na bustani za wazi ambazo mtu yeyote anaweza kwenda kwa ajili ya kupumzika au kuburudika kwenye mandhari nzuri ambayo imetengenezwa katika mji husika.

Mbali na kupamba mji, bustani za wazi zinafanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa sehemu ya mapumziko kwa watu mbalimbali wenye msongo wa mawazo na wageni wanaoingia katika mji fulani kwa shughuli zao.

Pia, shughuli nyingine za kijamii kama vile mikutano au makongamano yanaweza kufanyika katika bustani hizo bila kuathiri watu wengine waliokwenda kwa madhumuni yao. Bustani hizo zimekuwa kitu kizuri katika jamii iliyostaarabika na ambayo inajali ustawi wa watu wake.

Kwa bahati mbaya, Jiji la Dar es Salaam halina bustani ambayo watu wake na wageni wanaoingia kila siku wanaweza wakajivunia. Jiji hilo ndilo sura ya nchi hii. Serikali iko hapa na mataifa mengine yanautazama mji huo kama kielelezo cha Watanzania.

Pamoja na umuhimu wake, mji huo umekosa mambo muhimu kwa ustawi wa watu wake ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bustani za aina hii zinazoweza kuwahudumia wakazi wa jiji wapatao takriban milioni tano sasa.

Kukosekana kwa bustani hizo kunaelezwa kumetokana na mipango miji mibovu pamoja na mwamko mdogo wa viongozi katika kutambua umuhimu wa bustani hizi. Mambo yamekuwa yakiendeshwa hovyo bila kufuata weledi.

Viwanja vya wazi vilivyotengwa kwa ajili ya michezo vimeuzwa vyote na kujengwa majumba ya biashara. Rushwa imetawala katika umilikishaji wa ardhi, matajiri wanatumia fedha zao kununua viwanja vya umma bila hofu yoyote.

Baadhi ya halmashauri nchini zimejitahidi katika kutengeneza bustani kwa ajili ya wakazi wa maeneo hayo. Mfano mzuri ni manispaa ya Dodoma. Wao wana bustani ya wazi inayojulikana kama Nyerere Square.

Eneo hilo limekuwa kama alama ya mji wa Dododma na ukienda utakuta watu mbalimbali hasa wageni wamekaa na kufurahia mandhari ya bustani hiyo. Wanafunzi wa vyuo vikuu pia wanakwenda katika bustani hiyo kwa ajili ya kufanya mijadala yao.

Vilevile, Zanzibar imefanya vizuri katika kutengeneza bustani ya wazi. Bustani hiyo inatumiwa na mtu yeyote, lakini mara nyingi utakuta wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (Suza) wakifanya majadiliano yao juu ya masomo ya darasani.

Tanzania tunaweza kujifunza kutoka kwa jirani zetu wa Kenya ambao wana bustani kubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Kenya ilitengeneza bustani ya Uhuru (Uhuru Park) mwaka 1969 wakati wa utawala wa Rais Jomo Kenyatta.

Bustani hiyo ina ukubwa wa hekta 12.9 na imewekewa vitu vingi ndani yake ambavyo ni vya kuburudisha na kuwafanya watu wapumzike vema. Bustani hiyo ni ya wazi na watu hawatozwi pesa kuingia katika bustani hiyo isipokuwa kutumia baadhi ya viburudisho vinavyopatikana humo ikiwamo bembea za watoto, kupanda ngamia au kuendesha boti katika bwawa lililotengenezwa humo.

Pamoja na ukubwa wa bustani hiyo, zipo nyingine ndogondogo ambazo nazo zilijengwa muda mrefu kwa malengo hayohayo. Kwa mfano, bustani ya Jeevanjee iliyopo pia katika mji wa Nairobi nchini humo.

Kutokana na mifano hii michache, Serikali inaweza kujifunza na kuandaa mpango wa kulipa hadhi jiji la Dar es Salaam ili lifanane na miji mingine duniani iliyojengwa kwa ustadi wa aina yake.

Tayari Serikali imeanza kubomoa nyumba zilizojengwa katika maeneo ya wazi. Ninashauri Serikali iandae mpango wa kujenga bustani kubwa. Haitoshi kuwa na viwanja vya mpira wa miguu pekee wakati watu wengine si wapenzi wa mchezo huo.

Bomoa bomoa inayofanywa na Serikali ilete matokeo mazuri ili wananchi waone kitu ambacho Serikali imekusudia kukifanya.

Itakuwa haina maana kama nyumba zitabomolewa bila kufanya kitu ambacho kitakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Ninampongeza Rais John Magufuli kwa kuzuia ubinafsishaji wa baadhi ya fukwe katika bahari ya Hindi hasa ambazo zilikuwa zinatumiwa na wananchi kwa ajili ya kuburudika. Ameonyesha kwamba anatambua umuhimu wa kuwa na maeneo ambayo mtu yeyote anaweza kufika na kujipumzisha.

Utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa bustani za wazi unategemea utashi na utayari wa viongozi waliopo madarakani katika kusimamia suala hili kikamilifu.

Iwapo watafanikiwa kutengenezwa kwa bustani hizo, watawasaidia wananchi ambao hukosa kabisa sehemu ya kupumzika katikati ya jiji hasa wakatii wa jua kali.

Wananchi tutoe ushirikiano pale tutakapohitajika ili kurahisisha utekelezaji wa suala hili lenye manufaa kwetu sote.

Peter Elias ni mwandishi wa gazeti hili (Mwananchi) - 0763891422.
 

Attachments

  • upload_2016-1-20_11-43-5.png
    upload_2016-1-20_11-43-5.png
    88.1 KB · Views: 60
MBONA KUNA BOTANIC GARDEN PALE POSTA KARIBU NA IFM..??


ANYWAY BONDE LA MTO MSIMBAZI NASHAURI BAADA YA BOMOA BOMOA MSIMBAZI WAJENGE CENTRAL PARK KAMA YA PALE NEW YORK

MAANA HAKUNA NAMNA


800px-Central_Park_from_Rock.jpg
 
MBONA KUNA BOTANIC GARDEN PALE POSTA KARIBU NA IFM..??


ANYWAY BONDE LA MTO MSIMBAZI NASHAURI BAADA YA BOMOA BOMOA MSIMBAZI WAJENGE CENTRAL PARK KAMA YA PALE NEW YORK

MAANA HAKUNA NAMNA


800px-Central_Park_from_Rock.jpg
dah! central park. naipenda sana
 
Nchi hii watu hawana haya nakumbuka kama sio mwishoni mwa miaka ya 90 basi mwanzoni mwa elfu mbili watu wa ardhi waliuza mnazimmoja pale mtu akazungusha mabati mwenye kumbukumbu nzuri atalikumbuka tukio lile.
 
Serikali ya kutafuta utukufu binafsi, ya ukanda kkukomoawwengine, ya mipasho, yammbwembwe, ya hovyo hapaddunianikkwassasa yyammafisadi yyakkujifanyammiunguwwatu yyaddhihaka yyakkilaghai yyakkibabe yya ya KIDIKTETA. Serikali hii ya
 
Huu uzi ulikuwa wa maana sana lakini haukupata wachangiaji!
Katika vitu vinasikitisha nchi hii ni kukosa bustani za kubwa za watu kukutana, kupumzika, n.k. Bustani chache tulizo nazo hazina uwezo wa kuaccomodate watu kutokana na udogo wake. Naamini viongozi wetu sasa wanaweza kulifanyia kazi.
 
Nilipofika moshi kwa mara ya kwanza nilitafuta park nikajua IPO kila mkoa kwa uzoefu niliokuwanao kutoka Dom na Musoma (bustanini) !!

Nilishangaa nafika tu uhuru park naulizwa kinywaji gani!!

This country is so rotten !!
 
Back
Top Bottom