Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,443
DONDOO:
Ø Je ushawahi kumsikia mtu akisema ‘Na mimi nilikuwa nawaza hivyo hivyo' wakati mtu mwingine anapozungumza jambo fulani?
Ø Je kuna wakati umeshawahi kujisikia kama huna furaha na kuhisi kama kuna jambo ambalo si la kawaida litatokea. Na baadae unakuja kupata taarifa kwamba ndugu yako au rafiki yako ana shida na anahitaji msada wako?
Ø Je umeshawahi kuwa na rafiki ambaye huwa anapatwa na wasiwasi na mashaka mara kwa mara na wewe ukajikuta ukiwa na hali hiyo bila kutegemea?
Ø Je umeshawahi kuota ndoto kuhusu kupata mgeni uliyepoteana naye kwa siku nyingi na kweli siku inayofuata ukafikiwa na mgeni huyo?
Ø Je Umeshawahi kushuhudia mtu uliye karibu naye sana akiwa katika maumivu makali sana na wewe ukajihisi kupata maumivu hayo?
Ø Unadhani ni kwa nini watoto Mapacha mmoja akiumwa na mwingine hujisikia au huhisi kuumwa vile vile?
Hii hali ndiyo inaitwa Telepathy na hututokea pale ambapo mtu ambaye tuko karibu naye kama vile ndugu wa karibu mlioshibana, rafiki wa karibu sana, mpenzi, mama, baba, kaka, dada na hata mtoto ambaye umempenda kuliko wengine anapokuwa katika hali fulani na sisi hupata taarifa kupitia mawazo yetu na hisisa zetu.Tunaweza kusema:
Ø Ni mawasiliano ya moja kwa moja kutoka kwa mtu hadi mwingine bila kutumia njia tano za milango ya fahamu (Kunusa, kugusa, kuonja, kusikia, na kuona.)
Ø Ni uwezo wa kuwasiliana kwa kutumia uwezo wetu wa juu kabisa bila kutumia njia iliyozoeleka ya ishara au kuandika.
Ø Ni njia ambayo ubongo hutumika kwa kiasi kikubwa katika kupokea na kupeleka ujumbe kwa njia ya mawazo
Ø Ni njia ambayo huweza kusafirisha hisia zetu, mawazo yetu na hata maumivu yetu kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine bila ya watu hao kuonana
Utangulizi: Telepathy inatokana na lugha ya Kigiriki ambapo ni muunganiko wa maneno mawili:
Elepathy likiwa na maana ya Distant au kwa Kiswahili Umbali na neno Patheia likiwa na maan ya ‘to be affected by' au kwa Kiswahili tunaweza kusema ‘iliyoathiriwa na'Hii ina maana kwamba ni mawasiliano kati ya nafsi mbili bila kutumia njia tano za milango ya fahamu kwa maana ya ile milango ya fahamu tuliyoizoea: Kunusa, kugusa, kuonja, kusikia, na kuona.
Na hili neno telepathy lilivumbuliwa na msomi mmoja wa kifaransa aitwae Fredric W. H. Myers hapo mnamo mwaka 1882 alipotaka kupata msamiati mpya badala ya msamiati uliokuwa ukitumika hapo awali wa ‘Thought-Transference'
Telepathy ni nini?
Telepathy ni mawasiliano ya moja kwa moja ya kimawazo au hisia kutoka mtu mmoja hadi mwingine bila kutumia milango mitano ya fahamu tuliyoizoea. Haya ni mawasiliano ambayo yapo katika kiwango cha juu cha uwezo tulio nao binadamu ambapo nguvu ya ubongo ndio unaotumika kuratibu mawasiliano hayo.
Tunaambiwa kwamba si binadamu tu pekee wanaotumia njia hii katika mwasiliano peke yao, bali pia wanyama ndege na wadudu wanatumia njia hii kuwasiliana aidha wao kwa wao au wao na binadamu kwa wale waliofunzwa, hapa naweza kuwataja wanyama kama Mbwa, Punda, Farasi, Ng'ombe, Paka nk.
Pamoja na sisi binaadamu kuachana na njia hii ya mwasiliano kutokana na kukua kwa lugha na sayansi na teknolojia kwa upande wa mawasiliano, lakini yapo makabila ambayo bado mpaka sasa wanatumia njia hii katika mawasiliano, hapa naweza kutaja kabila la Aborigines la kule Australia ambapo wenyewe hujiita ‘watu halisi'.
Inaelezwa kwamba hata watoto wenye umri wa kuanzia miaka 6 wa kabila hili wanaweza kutumia njia hii ya mawasiliano. Na hii imetokana na tabia yao ya kutokuwa waongo, wazushi, wasiopenda kupindisha jambo na wala kuzusha jambo. Ni watu ambao ni wakweli wa nafsi zao.Ni vyema ikafahamika kwamba Binadamu wote tunao uwezo wa kutumia nguvu hii ya mawasiliano kama vile tunavyotumia pumzi na hii nguvu haijapotea ndani mwetu, ni kiasi tu cha kuamua kujifunza na kuifanyia mazoezi, na bila shaka tutamudu.
Tunazungumzia jambo hili leo, sio kwamba ni jambo geni sana kwetu, ni jambo ambalo huwa tunalifanya lakini likiwa nje ya urazini(awareness), na hivi sasa watu wengi duniani wameanza kuamka na kulifanyia kazi jambo hili wakitaka kurejea katika uhalisi wao na kupunguza au kuondokana na njia hizi za kisasa za mawasiliano ambazo zina athari kubwa kwetu kutokana na njia hizo kutumia mionzi ambayo ina athari katika ubongo na miili yetu kwa ujumla.
Inaelezwa kwamba kina mama ndio watu ambao hutumia njia hii ya mawasiliano kwa kiasi kikubwa hapa duniani. Kama mjuavyo kina mama hubeba ujauzito kwa miezi tisa, na baada ya hapo huwa na jukumu la malezi kwa watoto hao. Hivyo basi wakati watoto hao hususan wale wachanga au wadogo kwa umri na wasioweza kujieleza wanapokuwa na maumivu au kuumwa, kina mama wanakuwa wepesi sana kung'amua hali za watoto wao. Si hivyo tu hata pale watoto hao wanapokuwa tumboni kina mama wana uwezo mkubwa wa kuwasiliana na watoto hao kwa njia hii na mara nyingi huwatokea kwenye ndoto.
Watoto Mapacha nao wanatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuwasiliana kwa kutumia njia hii, si pale wanapokuwa pamoja tu yaani katika eneo moja, bali pia hata wanapokuwa wametenganishwa kutoka mji mmoja mpaka mwingine au hata kutoka nchi moja mpaka nyingine. Zipo simulizi nyingi sana zinazothibitisha jambo hilo.
Ndoto.
Ndoto nazo zinatajwa kuhusika sana katika njia hii ya mawasiliano. Na hata ukisoma vitabu vya dini mbalimbali, tunaambiwa kwamba hata mungu alikuwa akiwasiliana na manabii kwa njia ya ndoto. Si hivyo tu wazee wetu zamani walikuwa wakizingatia sana kila wanachokiona na walikuwa wanabashiri kwa usahihi kabisa kitakachotokea siku za usoni. Na ndio sababu siku hizi wapo wataalamu wa kufasiri ndoto.
Aina za Tepepathy
Zipo aina tatu za Telepathy:
Ø Kinesics Communication
Ø Emotion(Empathy) Telepathy
Ø Concrete Concept
Kinesics Communication:
Kinesics Communication ni mawasiliano yanayohusisha ishara badala ya kutumia lugha, hapa kinachotumika ni lugha ya mwili, macho au namna ya utazamaji. Wengi wetu tunaijua njia hii vizuri sana na tumekuwa tukiitumia sana. Kwa mfano mume au mke anaweza kuwasiliana na mkewe au mumewe mbele ya watoto na watoto hao wasielewe chochote. Au pale unapowasiliana na rafiki yako katika mkusanyiko wa watu na watu wengine wasielewe kabisa kinachoendelea.
Njia hii inatajwa kuwa ni nzuri na ndiyo inayotumiwa sana na ndugu walio na ukaribu, marafiki, wapenzi, na wanandoa. Lakini wapenzi na wanandoa ndio wanaotumia njia sana.Hata hivyo wapo baadhi ya wataalamu wa Telepathy wanaoamini kwamba, wakati milango hii mitano ya fahamu inapotumiwa (kuona, kusikia, kunusa, kuonja na kugusa) na watu walio na ukaribu, hufikia mahali wakatumia njia ya ishara katika mawasiliano, hivyo hiyo haiwezi kuitwa Telepathy.
Jambo hili linaweza kuwa na ukweli kwa kiasi fulani kwa sababu watu hao hutumia ishara ambazo zinawalazimu wawe wanaonana. Lakini njia hii ya mawasiliano haiwezi kukamilika iwapo watu hawa watakuwa kila mmoja hasomi mawazo ya mwenzake.
Emotion (Empathy) Telepathy
Inawezekana miongoni mwetu imewahi kututokea kulia pale tunaposimuliwa stori yenye kuhuzunisha na kuumiza moyo, au pale tunapoangalia sinema ambapo mhusika uliyempenda sana anatokea kufa mwishoni mwa sinema hiyo. Hisia za maumivu kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ni miongoni mwa aina hii ya Emotion Telepathy.
Kwa mfano wengi tuma-shahidi wa kujisikia maumivu pale ambapo yule tumpendaye au tuliyekaribu naye anapoumia au kupata maumivu. Mara nyingi tumeshuhudia wenzetu tuwapendao wanapoumia nasi hujisikia maumivu sawasawa na wenzetu hao. Wakati sio sisi tulioumia. Ni kama ilivyo pale ambapo mtu tuliye karibu naye anapokuwa na maumivu ya hisia, kuwa na msongo wa mawazo au anapokuwa na furaha kupita kiasi nasi nafsi zetu hujikuta zikipatwa na hali hizo wanazojisikia wenzetu hao.
Concrete Concept
Aina hii inahusisha kusafirisha vitu au alama kwa njia ya mawazo, kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Hii inahitaji watu wawili wanaowasiliana na wawe wamebobea kweli na wawe wamefanyia mazoezi aina hii ya mawasiliano ili kuweza kumudu kuwasiliana kwa njia hii. Njia hii inahitahi urazini wa hali ya juu.njia hii hutumika sana katika kusafirisha kwa njia ya mawazo maumbo, rangi na alama hadi kumfikia mtu aliyekusudiwa.
Matumizi yetu ya telepathy yalianza tangu tulipozaliwa na ni wazazi wetu ndio waliotufundisha namna ya kutumia aina hii ya vipawa tulivyozaliwa navyo. Kumbuka kwamba nilieleza hapo awali kuwa telepathy ni nguvu ya asili ambayo tulizaliwa nayo lakini kutokana na mabadiliko ya dunia katika kuwasiliana, tumejikuta tukiitupa njia hii na kuidharau. Hivyo basi ni jukumu letu kuirejesha kwa kuifanyia mazoezi.
Kama tungemudu kukumbuka enzi za utoto wetu, ni dhahiri tungependa tukumbuke wakati mama au baba alipokuwa akisema na sisi kwa kuigiza sauti zitumiwazo na watoto wachanga huku wakitabasamu na kutuchekea kwa namna ya pekee. Ni wakati huo nasi tulikuwa tukitabasamu kwa Furaha na Amani. Kwa kufanya hivyo wazazi wanakuwa wamewasiliana na watoto wao kwa kutumia njia hii ya Telepathy na hiyo huwafanya watoto kufuatilia kwa hatua kila kitendo kinachofanywa na mzazi ili kuweza kusoma mawazo ya mzazi.
Na hapo ndipo watoto wanapokuwa wamepiga hatua ya kwanza katika kujifunza kutumia uwezo huo ambao wamezaliwa nao.Kama mtakumbuka wakati, tulipokuwa tunahudhuria masomo kwa mara ya kwanza, mtagundua kwamba mambo mengi tuliyojifunza yalitoka kwa wale waliokuwa wakitufundisha na sio kutoka katika kitabu. Wakati mwalimu anapofundisha uelewa wetu unapatikana kupitia njia hii ya telepathy. Walimu pale wanapozungumza au kuelezea kitu, anakuwa na uwezo mkubwa wa kuteka mawazo ya wasikilizaji kwa kiwango cha juu.
Kumudu kujifunza Telepathy unatakiwa uwe na urazini wa hali ya juu katika kuratibu mawazo yako (Ni pale tu utakapojifunza Meditationa ndipo utakapomudu vizuri kudhibiti mawazo yako) na hiyo itarahisisha sana kujifunza na kumudu kwa usahihi kabisa kuwasiliana kwa kutumia telepathy