Zijue sababu zitakazoifanya chadema ishindwe arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zijue sababu zitakazoifanya chadema ishindwe arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mujumba, Mar 30, 2012.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika kuwa chadeam ni chama kikubwa kwasasa lakini hicho sio kigezo cha kukifanya kijione kiko sawa na ccm na kuweza kupambana na ccm ambacho kina mtaji wa mamilioni ya watanzania mjini na vijijini! lakini tukiwa tumebakiza siku chache kabla ya uchaguzi mdogo wa ARUMERU, zifuatazo ni sababu chache za msingi zitakazo iangusha chadema na kuicha ccm ikiibuka kidedea

  1. UDHAIFU WA NASSARI
  Ni ukweli ulio wazi Nassari ni mgombea ambae kiwango chake kipo chini sana katika kujenga hoja na kuzitetea,marafiki zake wa karibu wamepruv hilo, pia hana mvuto wa kisiasa kama mshindani wake wa karibu SIOI! Pia Nassari amekuwa akibebwa zaidi na umaharufu wa viongozi wake wa juu wa chama i.e MBOWE na SLAA ambao wamepiga kambi mjini ARUMERU ili kumpigia kijana wao kampeni, ili la kubebwa na kina Slaa, hata RAIA mwema wamelipruv, nanukuu"Mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari, licha ya uwezo wake binafsi wa kujieleza lakini kwa sehemu kubwa uzito wake jukwaani unahusisha umaarufu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa, ambaye bado hajapoteza mvuto wa kisiasa kwa wakazi wa Arumeru'

  2.WAPIGA KURA VIJANA
  ni jambo lililo wazi kwamba chadema inategemea sana vijana zaidi katika kampeni zake na ndio mtaji mkubwa sana wa chama hicho, sasa vijana wengi waliojiandikisha pale arumeru wengi wako shuleni kwasasa, wengine vyuoni hivyo uwezekano wa kukosa kura ni mkubwa
  pia ukiangalia mahudhurio na aina ya ushabiki wa kampeni za CHADEMA, ni dhahiri kuwa wapiga kura wengi wa chama hicho ni vijana.

  Ni katika mtazamo huo ambamo changamoto inayojitokeza ni kuwa vijana wengi wenyeji wa Arumeru Mashariki hawakujiandikisha kupiga kura katika kata za jimbo hilo.

  Wengi wamejiandikisha katika maeneo wanakoendesha shughuli zao za kujikimu kimaisha, ambazo ni Mererani, kwenye mgodi wa Tanzanite, eneo lililopo Jimbo la Simanjiro, linaloongozwa na Christopher ole Sendeka. Mbali na Mererani, vijana wengi wa jimbo hilo wamejiandikisha kupiga Arusha Mjini, wanakoendesha shughuli zao za kila siku hii kwa kiasi kikubwa itamwangusha bwana NASSARI, sababu ccm imejiwekeza katika kada mbalimbali za watu kuanzia watoto,vijana na wazee ambao kikukweli ndio hazina kubwa ya ccm

  3.NGUVU KUBWA YA CCM ARUMERU
  siamini ni kwa jinsi gani chadema inaweza shinda katika jimbo ambalo viongozi wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya ni ccm, hapa ni kujidanganya! lazima chadema wakubali kuwa pale ARUMERU sio pao,kwa mtaji huu ccm inaweza kucheza both macro and micro politics ilhali kujihakikishia ushindi mkubwa
  4.PROPAGANDA ZA WAZI ZA CHADEMA
  Chadema katika kampeni zake nyingi imekuwa ikimwaga propaganda nyingi sana kuhusu ccm, wananchi wa arumeru wamekuwa na ccm kwa muda mrefu kwahiyo wanajua fika yanayosemwa sio sahii! ingawa hata ccm imekuwa ikitoa propaganda kali na wengie wamesikika wakitoa matusi makali kwa viongozi wa chadema ila kuna msemo wa kiswahili unaosema "zimwi likujualo....."
  kwa uchache hayo ni mambo yatakayoiangusha chadema tarehe 1 april 2012
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... my foot!!!!!!!!!
   
 3. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Sioi ana umaaarufu gani? Huo mvuto alionao ni upi? Acha porojo!
   
 4. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rabbish
   
 5. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  anaitwa SIOI SUMMARI just to remind you my bro! that name itself is popular....
   
 6. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mchawi siyo lazima avae tunguli,Kwa umaarufu gani alionao Sioi kumzidi Joshua,
  Jumatatu uje tena ujinga kama huu,maana utakuwa umeshapata jibu yupi ni maarufu
  na ukweli ni upi.
   
 7. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  hakika cdm ni chama chenye mvuto na kinachotishia matumbo ya watu.nadhani mtasema yote mlonayo mioyoni maana msiposema mtakufa kihoro.ccm mmekaliwa kooni pumzi imewakata network hakuna vichwani mnahangaika kwa kila namna,mbio za sakafuni huishia,,.ukingoni.nawaombea kheri!
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Acha kupiga mayowe subiri 1st April
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuishi Kwa Matumain@MsondoJazzBand!
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Kama ndo hivyo, tusubiri tarehe 01/04/2012.

  Wasiwasi wangu,

  Propaganda za siku ya wajinga duniani na magazeti yanayonunulika na ccm tarehe 01 Aprili 2012
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Pumba Express!!.....
   
 12. P

  Praff Senior Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyeleta post hii ni kada wa sisiem.
   
 13. M

  Malova JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kipindi Slaa anatwa jimbo la Karatu alikuwa na kiongozi yeyote chini yake ambaye ni wa CHADEMA? Kutokuwa na viongozi wa chama chako chini yako haimaanishi kushindwa kuchaguliwa.
   
 14. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  popular kwa vile katoga masikio au?
   
 15. Sihali

  Sihali Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulitaka awe mwananchama wa CHADEMAV? Unadhani utasikia yale unayopenda kuyasikia? Safisheni CHADEMA ndani imeozaaaa
   
 16. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sijafika kwenye kampeni na wala arumeru sipafahamu lakini kwa maelezo yako hakuna la maana zaidi ya unafiki kwa ccm, jiulize huko ambako cdm huwa inashinda hakuna wazee ambao ni mtaji wa ccm? Kumbuka 2010 vijana walikuwa majumbani lakini Mnyika na Mdee walishinda
   
 17. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 2,461
  Trophy Points: 280
  Ni ngumu sana kutoa tathmimi ya kinachojiri arumeru kwa kufuata kile kinachoandikwa magazetini..Niko ARUMERU NNAELEWA kinacho endelea tusubiri tar 1..
   
 18. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ooops, my country Tanzania!!!!!

  Huo umaarufu sasa ni kwa vile baba yake alikuwa naibu waziri au!??? Na huyo waziri alifanya nini kikubwa (mfano Magofuri amejenga barabara, Mwakyemba anapinga ufisadi! nk)? Inasikitisha sana kupandikiza propaganda za namna hii maana uchaguzi unapita lakini Tanzania inaendelea kuwa masikini

   
 19. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nimecoka na sarakasi za Arumeru mashariki nataka mpya
   
 20. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Well analyzed, lakini hii haiwezi ika-apply kwa watu waelewa na waliochagua mabadiriko, CCM ina mtaji mkubwa wa wanachama watu wazima lakini sidhani kama kuna mtu mzima mwenye akili timamu anayeweza kujitokeza ku-surpot sera za akina Lusinde, sidhani kama kuna mtu mzima asiyefaham CCM imemtoa wapi na imemfikisha wapi. hivi unajua CCM imetufikisha mahala Watanzania wana hamu ya kubadiri utawala hata wammpatie mtu asiye fahamika utendaji wake maana kuna uwezekano wa kuwatendea mema kuliko CCM iliyopo madarakani kwa miongo zaidi ya mitano na utendaji wake upo bayana. Japo naamini bado Tz ina watu wenye uwezo wa chini sana kwenye kutafakari waliompigia kura Kikwete kwasababu ni mweupe vivyo hivyo nahisi watampigia Sioi ili kumfuta machozi kwasababu kafiwa na baba yake mzazi lakini kundi la watu wa aina hii linazidi kupungua kwa kasi zishukuliwe shule za kata kwa kila kata kwani zinasaidia kutoa tongotongo
   
Loading...