Zijue sababu mbalimbali zilizosababisha watu tunaowajua kujinyonga

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,524
21,998
Leo nimeona niwasogezee Uzi huu iwe kama tahadhari na somo kwetu kutokana na hizi sababu za watu mbalimbali kuamua kujinyonga ( kujiua).
1. Jamaa mmoja alilipotiwa kuchukua uamuzi wa kujinyonga huko iringa kisa Mkewe alimnyima samaki (mboga)
2. Askari mmoja huko Tanga aliamua kujiua Kwa sababu tu mwanamke wake kachukuliwa na askari mwenzake.
3. Mtu mmoja ambaye ni mpiga picha maarufu huko Masumbwe- Geita (Athanas photo ) ameripotiwa kufikia maamuzi ya kujinyonga kisa mkewe alikwenda kukopa mil 20 saccos akiwa na hawala yake Kwa siri..ambapo Mme alikuja kutambua siku ya nyumba yake ilipopigwa mnada akaamua kujinyonga.
4. Huko mtwara jamaa aliyetambulika Kwa jina la JUMA alijinyonga Kwa kamba kisa alikimbiwa na mke wake.
5. Juzi jamaa mwingine kawanyonga watoto na yeye kujiua kwasababu alikuwa kalewa.
6. Binti mmoja huko tanga aliamua kujinyonga kisa kapata division zero.
7. Mwalimu Wa shule ya msingi huko masumbwe aliwahi kujinyonga kisa mke wake kuzaa na mwanaume mwingine wakati yeye akiwa masomoni na aliporudi akakuta mtoto.
8. Mtu mmoja aliamua kujinyonga huko morogoro kisa alikuta shamba lake lote limelishwa mifugo.
9. Mtoto mmoja huko mbeya alijinyonga kisa hakuchaguliwa kujiunga Fomu one!
10. Jamaa mmoja alifikia uamuzi Wa kujinyonga baada ya kufukuzwa kazi na kuandamwa na madeni aliyokopa!
NI TUKIO GANI HAPO JUU AMBALO KAMA LINGEKUKUTA WEWE UNGEJINYONGA?
******************************
ENDAPO KUNA TUKIO UNALOLIJUWA LILILOWAHI KUPEKELEKEA MTU UNAYEMFAHAMU KUJINYONGA LIWEKE HAPA ILI WATU WAJIFUNZE MAKOSA!
 
Depression hurts! Hii ni mood disorder ambayo inamfanya mtu kupata huzuni ya kupita kiasi cha kawaida na hivyo binadamu kutamani kufa kuliko kuishi...
Usiombe ufikie katika hali hiii...
Hata Yesu kristo alishwahi kufikia katika hii akasema, 'Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa'...
Huu ni wakati mgumu sana kwa binadamu aliye hai kuliko nyakati zozote...
Its an emontional state that makes you think that, 'This is the end of the road'... Your face is covered with total blindness such that you dont get a breakthrough. You dont know what next... And you feel that the best thing is to dissappear from the face of the Earth!
 
Depression hurts! Hii ni mood disorder ambayo inamfanya mtu kupata huzuni ya kupita kiasi cha kawaida na hivyo binadamu kutamani kufa kuliko kuishi...
Usiombe ufikie katika hali hiii...
Hata Yesu kristo alishwahi kufikia katika hii akasema, 'Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa'...
Huu ni wakati mgumu sana kwa binadamu aliye hai kuliko nyakati zozote...
Sijakuelewa; inamaana yesu aliwahi kufikiria kujinyonga?
 
Sijakuelewa; inamaana yesu aliwahi kufikiria kujinyonga?
Hapana, hakufikiria kujinyonga. Inawezekana alikuwa anasikia huzuni kubwa sana mpaka akatamani afe. Ni sawa na wewe unaweza ukasikia kuchoka sana ukatamani kulala!
Mathayo 26
37 Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka.
38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
 
Duh
 
Nimejaribu kuwaza maumivu aliyoyapata huyo Namba 3 hapo.
# aliumia Kwa kudhalilishwa.
# aliumia kugegedewa mke wake
# aliumia kudhauliwa na mke wake hadi kutafta mtu mwingine
# aliumia mzigo alionao Kwa watoto
# huenda aliumia na gonjwa aliloletewa na mke wake
# aliumia wapi atapata hela ya kurejesha mkopo
# aliumia Jamii itamfikiliaje
HUYU PEKEE ALISTAHILI KUPEWA CHETI CHA KUJINYONGA ( certificate of self-killing)
 
Back
Top Bottom