Maswali yanayohitaji majibu juu ya kifo cha Afande Greyson Mahembe anayedaiwa kujinyonga mahabusu

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
1. Afande Greyson Mahembe hayupo kwenye orodha ya askari saba wana otuhiwa kumuua kijana Musa Hamis Hamis. Nani aliyeeneza taarifa ya kwamba Greyson ni mmoja wa watuhumiwa saba? Kwa lengo gani? Kwa nia gani?

2. Afande Greyson Mahembe anadaiwa kujinyonga ndani ya mahabusu kwa kutumia tambala la deki. Ni mahabusu gani yenye tambala la deki? Nani aliingiza tambala la deki mahabusu? Hilo tambala la deki lilotumiwa 'kujinyonga' lipo wapi?

3. Mazingira ya kujinyonga yakoje? Kuna mahali alifunga tambala kisha akajifunga na yeye shingoni halafu akaning'inia? Swali hili ni muhimu sana kwa sababu mwanadamu hana uwezo wa kujiua kwa kujinyonga kwa mikono yake mwenyewe. Kisayansi hilo haiwezekani. Ili mtu aweze kujiua kwa kujinyonga, ni lazima aifunge kamba au kitu kitu kama hicho kisha ajining'inize. Je! Afande Mahembe alifunga tambala la deki sehemu gani na kujining'iniza?

4. Taarifa ya uchunguzi wa kimahakama (forensic investigation) inasemaeje juu ya sababu ya kifo chake? Kisheria, vifo vyote vinavyotokea chini ya ulinzi lazima vichunguzwe. Mahabusu ni chini ya ulinzi. Daktari mbobezi wa Forensic Pathology anaweza kuchunguza na kugundua sababu ya kifo ikiwa ni pamoja na kama mtu amejinyonga mwenyewe au amenyongwa.

5. Wakati Afande Mahembe anafanya huo mchakato huko mahabusu alikuwa peke yake? Kwanini awe peke yake? Na kama kulikuwa na watu walichukua hatua gani? Wahojiwe.

5. Nani wa kwanza kutoa taarifa za kujinyonga kwa Afande Mahembe? Ahojiwe.

Hayo ni maswali machache kati ya mengi yanayostahili kuhojiwa.

Mapendekezo yangu ni kuwa serikali iunde tume maalum ya kuchunguza matukio mawili. Moja la mauaji ya kijana Musa Hamis Hamis ambalo watuhumiwa wake wanatajwa kuwa askari saba waliokwisha kamatwa.

Pili, tukio kifo cha Afande Greyson Mahembe anayedaiwa kujinyonga. Mimi nilistuka tangu tulipoambiwa ni mmoja wa watuhumiwa saba wa mauaji ya Musa wakati kwenye orodha ya waliotajwa awali hakuwepo.


FB_IMG_1643648596463.jpg


View attachment 2103103View attachment 2103102View attachment 2103101
 
Namba 1 hapo hivi watu kama wewe huwa mnafatilia habari kwa umakini kabla ya kupost!? mbona taarifa ya PT kupitia afande Misime zinasema marehemu naye alikuwa ni mtuhumiwa na alikiri wewe unasema hakuwa mmojawapo! ni vizuri kufatilia habari kwa umakini kabla ya kupost ili kuepusha uchonganishi na kuleta taharuki katika jamii.

IMG_20220131_203303.jpg
IMG_20220131_203307.jpg
 
namba 1 hapo hivi watu kama wewe huwa mnafatilia habari kwa umakini kabla ya kupost!? mbona taarifa ya PT kupitia afande Misime zinasema marehemu naye alikuwa ni mtuhumiwa na alikiri wewe unasema hakuwa mmojawapo! ni vizuri kufatilia habari kwa umakini kabla ya kupost ili kuepusha uchonganishi na kuleta taharuki katika jamii
View attachment 2103117View attachment 2103118
Mleta mada kupitia source yake pengine imeonekana hakuwepo ktk mpango huo
 
Back
Top Bottom