Zijue nchi zenye watu wanaoishi umri mkubwa zaidi duniani na sababu zake

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
aaa.jpg

JUKWAA la Uchumi Duniani (WEF) limetoa utafiti wa nchi ambazo watu wake wanaishi umri mkubwa zaidi. Utafiti huo haukutia maanani tu nguvu ya kifedha ya nchi husika bali afya ya watu katika nchi hizo.

Utafiti huo umelinganishwa dhidi ya takwimu za nchi za umoja wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi (OECD) kujua ni kwa nini watu huishi umri huo mrefu.

Nchi hizo na nafasi zake, umri na sababu zake ni:

13. Sweden — miaka 82. Sababu kuu ni maji safi.

12. Iceland — 82.1. Chakula bora kinachopunguza hatari ya magonjwa ya kisukari na moyo.

11. Jamhuri ya Korea (Kusini) — 82.2 kustawi kwa uchumi na kuboreshwa kwa maisha licha ya kiwango cha uchafuzi wa mazingira kuwa juu.

10. Luxembourg — 82.2. Idadi ndogo ya watu na kipato cha juu, mambo yanayowapa chakula bora na matibabu bora.

9. Israel — 82.2. Wanaume ndiyo huishi umri mrefu zaidi licha ya kulazimika kulitumikia jeshi.

8. Australia — 82.3. Huduma nzuri ya afya.

7. France — 82.4. Idadi ndogo ya watu wenye vitambi.

6. Singapore — 82.6. Matibabu mema na kinga za magonjwa.

5. Italy — 82.7. Tiba njema, kipato kikubwa kinachowawezesha kula na kuishi maisha mazuri.

4. Switzerland — 82.8. Tiba na chakula bora.

3. Spain — 83.1. Chakula bora hasa mboga, samaki na vyakula vya mafuta..

2. Japan — 83.6. Chakula bora.

1. Hong Kong — 84. Chakula bora chenye kukaushwa na unywaji wa chai.
 
dada ake wa bibi yangu ana miaka zaidi ya 100 na mpaka leo ukimzingua anakuvunja,ana kaa kijijini hajawah kwenda mjini halafu ndo kwanza utafikiri ana miaka 60
 
Hawa waongo babu na bibi Yangu wazaa babu tunawaanika kila asubuhi huko kijijini wana zaidi ya 120
 
Anakula Chakula Gani ?
KANDE ZA MAHINDI MAKAVU AMBAZO HAZIJAKOBOLEWA+MAHARAGE+NJEGERE+MBOGA MABOGA+ULANZI+VIAZI MVIRINGO AMBAVYO HAVIJA MENYWA BUT VIMECHEMSHWA HATUMII MAFUTA YA KUPIKIA ANATUMIA TETERE KUUNGA CHOCHOTE, NK
 
Back
Top Bottom