Mahmood
JF-Expert Member
- Feb 9, 2008
- 7,908
- 2,480
Baada ya kutimiza sifa za kuwa Muumin. Basi jiangalie, je utakuwa miongoni mwa Muumin aliyefuzu (faulu)?
1) Muumni ambaye ananyenyekea kwenye Swalah yake, iwapo mtu hunyenyekei basi hujafuzu.
2) Ambae anajiepusha na mambo ya upuuzi, iwapo hujiepushi na mambo ya kipuuzi basi utakuwa hujafuzu. Labda mtu atajiuliza suali - mambo ya kipuuzi ni yepi? Tukipata wasaa in shaa Allaah tutakuja kuyaeleza mambo ya kipuuzi ni yepi kutokana na mtizamo wa Kiislamu.
3) Ambaye anatoa Zakaah (charity), iwapo upo kwenye kundi la wenye kuwajibika kutoa Zakaah na ukawa huitoi, basi utakuwa hujafuzu.
4) Ambaye analinda uchi wake isipokuwa tu kwa wake zake, iwapo huilindi wako wako basi utakuwa hujafuzu, na ndie yule anaeitwa mzinifu. Mungu Atuepushe na uzinifu.
5) Ambaye hutimiza amana na ahadi, iwapo ukiwa unaifanyia khiyana amana na huna ahadi, basi hujafuzu.
6) Ambaye Swalah zake anazihifadhi, iwapo huhifadhi Swalah zako basi hujafuzu (hujafanikiwa).
Ikiwa basi unatimiza sifa hizi, basi utakuwa umefuzu (umefanikiwa), na ndio utarithi Pepo iitwayo Firdaws kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam):
Mnapomuomba Mwenyezi Mungu pepo, Muombeni (Pepo) ya Firdaws-kwani (pepo hiyo) ni ya kati na kati na-ndani yake inatiririka mito, juu yake kuna Arshi ya Ar-Rahmaan.