JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Mwekezaji anayetaka kuuza hisa atafuata taratibu zifuatazo:
Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kuuza hisa
Kabidhi hati yako ya umiliki wa hisa kwa dalali. Dalali atahakiki umiliki wa hisa hizo kabla ya kuuza
Kama hisa haziko kwenye hifadhi ya hisa, dalali ataziweka kwenye hifadhi kabla ya kuuza
Dalali ataweka oda yako ya kuuza hisa kwenye mfumo wa kompyuta wa soko la hisa akitumia namba maalum ya mteja.
Iwapo bei unayotaka kuuzia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kununua, basi atakuwa amekuuzia hisa hizo na mwekezaji atalipwa.