Zifahamu sababu za kusitisha ajira

Zifahamu sababu za kusitisha ajira

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
"...ni jukumu la kila mwajiri, kutoa mkataba wa ajira, kulipa mshahara na masilahi mengine stahiki kwa wakati, kuandikisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi ya Mifuko ya Jamii Na. 8 ya Mwaka 2008 kifungu cha 30.Kinatoa jukumu kwa waajiri kwenye sekta rasmi kuhakikisha wafanyakazi wao wanasajiliwa na mifuko ya hifadhi ya jamii".



*Sababu ambazo zinakubalika kusitisha ajira ya mtu ambazo ni pamoja na;-

Moja, mwenendo mbaya unaweza kuwa ni sababu inayokubalika kusitisha ajira endapo utafuata utaratibu na sababu kuwa halali. Kwa mujibu wa kanuni ya 11 ya kanuni za ajira ya mwaka 2004, inatakiwa kuweka kuweka utaratibu wa mwenendo kazini unaofahamika na kutumika siku zote.
Uhalali wa sababu ni kuwa sheria imeweka baadhi ya matendo kuwa itakuwa ni mwenendo mbaya kazini (misconduct) kama udanganyifu mkubwa, uharibifu wa mali kwa makusudi, kuhatarisha usalama wa wengine mahala pa kazi, uzembe mkubwa, kumshambulia mwajiri, wafanyakazi wenzako au wateja na dharau kubwa.
Mahakama itaangalia ukubwa wa kosa na adhabu yake, mazingira na usalama mahala pa kazi, pia mahakama itaangalia rekodi za nyuma za makosa ya muajiriwa lakini pia kosa la kwanza halitahalalisha kumfukuza mtu kazi labda liwekuwa kubwa sana.
Kukosa uwezo (incapacity) inaweza kusababishwa na ugonjwa, kuumia au utendaji mbovu, hivyo inaweza kusababisha kusitisha ajira ya mhusika hii kwa mujibu wa kanuni ya 15 ya kanuni za ajira za mwaka 2004.
Ugonjwa, mtu anaweza kuugua sana kiasi kwamba akawa hawezi kuendelea na kazi ajira yake inaweza kusitishwa kwa kufuata utaratibu wa kisheria ikiwapo na kupata vithibitisho kutoka kwa daktari. Pia mtu mwingine anaweza kuumia kiasi kwamba akashindwa kuendelea na ajira basi utaratibu ufuatwe ikiwa ni pamoja na kumpa ajira mbadala.
Utendaji mbovu ni sababu inayokubalika kusitisha ajira ya mtu, inatakiwa kuwapo na viwango vya utendaji vinavyokubalika kwa pande zote na mmekubaliana. Mwajiri atatumia viwango hivyo kupima utendaji na pia mtu anatakiwa apewe fursa ya kujieleza kwanini yuko chini ya kiwango kabla ya kusitishwa ajira yake.
Pia kutohitajika inaweza kuwa sababu (incompatibility) hapa mwajiriwa kutoendana na mwajiriwa wake au wafanyakazi wenzake au wateja yani huendani na wenzako kitabia au ni mtu wa ugomvi sana, unatukana wateja, hiyo pia ikithibitika inawezakuwa sababu ya kusitisha ajira ya mfanyakazi. Hii inatokana na tabia ya mfanyakazi au silika yake, lakini ninasisitiza zaidi katika kufuata utaratibu.
Pia ajira ya mfanyakazi au wafanyakazi inaweza kusitishwa endapo kampuni husika au mwajiri hawezi tena kuwatumia watu hao (operation requirement), kwa mfano kampuni inafungwa, sheria inaruhusu watu hawa kusitishwa ajira yao lakini utaratibu ufuatwe ikiwa ni pamoja na kupewa stahiki zao.



Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom