kwitandula
Member
- May 24, 2020
- 30
- 35
Inaletwa kwako na mkunga,
Habari wanajukwaa, awali ya yote poleni sana na majukumu ya kila siku, leo ningependa niwape mada fupi kuhusu uzazi wa mpango, na uzazi wa mpango ninaowaletea leo ni ule wa kisasa.
Nini maana ya uzazi wa mpango
Ni njia ambazo mke na mume wanaamua kuzitumia ili kuzuia mimba zisizotarajiwa,kuweka nafasi kati ya mtoto na mtoto ambapo kiafya inashauriwa wapishane kuanzia miaka miwili(wa mwanzo atakua ameshafikia umri wa kuacha kunyonya), kumpa muda mama aliyejifungua kuujenga mwili wenye afya njema na kupumzika,uchumi n.k
Aina za njia za mpango
1. Njia za muda mfupi kama; kondomu,vidonge
2. Njia za muda mrefu kama;vipandikizi na lupu
3. Njia za kudumu(kufunga kabisa uzazi kwa mwanamke au mwanaume)
Ufafanuzi
Njia za muda mfupi ni zile ambazo mtumiaji atatakiwa atumie kila siku(vidonge) ili kuzuia mimba bila kukosa na ikitokea umesahau kunywa basi itakupasa utumie kondomu endapo utahitaji kujamiiana
Njia za muda mrefu kama vipandikizi huwekwa kwenye msuli wa mkono, kipo cha miaka mitatu na miaka mitano(vinakua viwili), kwa upande wa lupu hiki ni kijiti chenye muundo wa T-shape ambacho kinaingizwa kupitia uke na kuwekwa kwenye mji wa mimba(uterus) kinafanya kazi hadi miaka kumi na mbili
Njia za kudumu hizi kabla ya kuchagua kutumia inahitaji mwanamke au mwanaume kuamua na kuwa na msimamo na uamuzi na unaochukua kwa sababu ukishafungwa hauwezi kufungua tena na hautakua na uwezo wa kupata mtoto tena.
Note:
Kumekua na dhana potofu katika jamii juu ya utumiaji wa uzazi wa mpango hasa mwanaume anapoambiwa na mwenza wake juu ya matumizi ya njia hizi
1. Njia za uzazi wa mpango hazileti Kansa kama wengi wanavyosema sababu za kansa nyingi hadi sasa haijulikani japo kwa baadhi ya kansa kama cervical cancer(kansa ya shingo ya kizazi inasabishwa na virus-human papiloma virus na ni sexually transmitted)
2. Vipandikizi, lupu kupotelea mwilini sio kweli japo kama utaweka na Mtoa huduma ambae hana ujuzi sana hasa kwa vipandikizi muda wa kuweka anaweza kukiingiza ndani sana ambapo muda wa kutoa itachukua muda kukitoa
Ushauri
•Uzazi wa mpango unapangwa na mke na mume hivyo wote mnapaswa kuhudhuria kliniki ya uzazi wa mpango kwa ajili ya kupata elimu na kuchagua njia itakayowafaa
•mpeleke binti yako ambaye amefikia umri wa kupevuka kliniki ya uzazi wa mpango hasa yule anaeonesha dalili za mapenzi ili kuondoa aibu ya binti yako kupata mimba za utotoni usione aibu!
• huduma za uzazi wa mpango ni bure
Karibuni kwa maoni, nyongeza na maswali na ambapo nimekosea unaweza sahihisha.