Zifahamu Biashara zinazolipa sana mitandaoni

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Zifahamu Biashara Zinazolipa Zaidi Mtandaoni.

Biashara hizi pia zinakuja na changamoto zake hivyo ni vizuri kuchagua unayoiweza
Linapokuja swala la biashara mtandaoni ni wazi kuwa kila mtu ana upeo wake pamoja na uzoefu unaomsaidia kupata pesa mtandaoni, lakini pia kufanya biashara mtandaoni hasa ukiwa Tanzania unahitaji kuangalia aina fulani za biashara ambazo hizo pengine zinaweza kukusaidia zaidi kupata pesa mtandaoni hasa ukiwa afrika na Tanzania kwa ujumla.

1. Anzisha Tovuti au Blog
Ukweli ni kwamba, Google bado inauhitaji wa tovuti hasa tovuti za kiswahili. Lakini hapa sina maana kuwa na tovuti zisizo na maana hapana, bali hapa nina maana tovuti zenye kuleta maana na kutoa mchango wa thamani kwa wasomaji kila siku na sio kuangazia maswala ya kipato pekee. Lakini wazo hili la biashara mtandaoni limekuwa ni la mwisho kwa sababu kuwa na tovuti pekee sio chanzo cha mapato bali unahitaji kuwa na vyanzo vya ziada kuweza kuhakiksha tovuti hiyo inakuingizia faida.

2. Anzisha YouTube Channel
Sambamba na kuanzisha tovuti unaweza pia ukaanzisha YouTube channel lakini ni muhimu kuwa na picha pana ya unapokwenda kwani watu wengi wamekuwa wakianzisha channel bila kuwa na muelekeo wakiwaza kwamba unaweza kuwa tajiri kwa haraka kwa kuchapisha habari au video zisizokuwa na maana. Ukweli ni kwamba kuwa na channel hasa hapa Tanzania unahitaji kutengeneza ubora wa video zako pamoja na mada zako ziwe na mchango lakini pia unatakiwa kujua unapokwenda kwani asikudanganye mtu yoyote matangazo ya Google Pekee hayatoshi.

3. Kutafuta Masoko Kwa Niaba ya Makampuni (Affiliate Marketing)
Ukweli ni kwamba hakuna kampuni ambayo haina kitengo cha kutafuta masoko, kama kwa namna yoyote umefanikiwa kutengeneza jina mtandaoni au unaweza kutoa ushawishi mtandaoni basi unaweza kufanya biashara ya affilate marketing. Lakini kama zilivyo biashara nyingine kwenye listi hii pia nayo hii inakuja na changamoto zake. Kama unafanya kazi hii kwa hapa Tanzania ni lazima kuwa na jina kubwa sana ndipo uweze kufanikiwa kwani watu wanahitaji mtu muaminifu na uaminifu hauji kwa maneno bali kazi na muda mrefu wa kujituma bila kuwaza faida.

Vilevile kama unafanya kazi hii na kampuni za nje ya Tanzania bado kuna changamoto kubwa sana ya njia za malipo hasa kwa wanunuaji pamoja na njia za kuweza kupokea fedha zako baada ya kutengeneza faida.

4. Ushawishi Kwenye Mitandao ya Kijamii (Social media influencer)
Kwa sasa kama umekuwa ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram lazima unajua kuwa kuna baadhi ya watu wanafanya matangazo ya makampuni fulani kupitia akaunti zao hii ndio inaitwa social media influencer, hapa sisemi matangazo ya vipodozi au matangazo madogo madogo bali mara nyingi watu hawa hupewa bidhaa na makampuni makubwa kuweza kujaribu au kutumia na baadae kutangaza kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii. Lakini biashara hii kama zilivyo biashara nyingine nayo pia inakuja na changamoto.

Ili kuweza kufanya biashara hii unahitaji kuwa na wafuasi wengi na pia unahitaji kuhakikisha wewe mwenyewe unajiweka kwenye mazingira bora ya kushawishi kampuni kuweza kufanya kazi na wewe, akaunti yako isiwe yenye kuvunja sheria za nchi au kukiuka maadili kwa namna moja amba nyingine lakini kikubwa kabisa unatakiwa kuwa na ushawishi mkubwa kupitia mitandao yako hiyo.

5. Kuwanunulia Wateja Bidhaa Kutoka Mtandaoni (Drop shipping)
Kama wewe ni mpenzi wa biashara mtandaoni basi lazima utakuwa kwa namna moja ama nyingine umeshawahi kuwaza kununua kitu kutoka mtandaoni, lakini kutokana na sababu kama njia rahisi za malipo pamoja na njia za kufanya mzigo kukufikia kwa urahisi basi unakuta hatua hii ya kununua kitu inakuwa ni ngumu sana.

Ndio maana biashara ya kununulia watu vitu kutoka mtandaoni ni moja ya biashara bora sana kwa sasa hapa Tanzania. Biashara hii inahusisha kununua bidhaa kwenye tovuti kubwa kama vile Amazon, Ebay na nyingine kama hizo na kusafirisha bidhaa hizo moja kwa moja kwa mteja bila mteja kuwa na mawasiliano na kampuni husika, mteja hukulipa wewe kiasi fulani cha pesa ambacho hichi hutosha kulipia gharama zote pamoja na wewe kupata faida kwa kiasi fulani.

Mara tu mzigo unapofika mteja huja kuchukua kwenye ofisi zako au huletewa na kampuni za usafirishaji ambazo unakuwa unafanya nazo kazi, uzuri wa biashara hii unaweza kufanya bila hata ya kuwa na ofisi lakini unahitaji kuwa na uaminifu mkubwa ambao huu unapatikana kwa kuwa na jina kubwa pamoja na kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu kidogo..

Nimeandika hayo nikiwa na uzoefu wa baadhi ya vipengele na ninasimama kama moja ya Blogger na YouTuber
 
Pole sana mkuu Kumbe na huko wamejaa matapeli
Najuta kuagiza saa mtandaoni, hasa Kikuu, niliziona saa nzuri Sana kwa Bei poa, nikasema zikija bonge ntapiga hela. Zilipokuja aiseee, yaani hata kuuza 2000 huwezi, nikazigawa kwa watoto wa primary school
 
Back
Top Bottom