Zifahamu aina nne za mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zifahamu aina nne za mapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by somba kankara, Aug 24, 2012.

 1. somba kankara

  somba kankara Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ya muda huu wana JM ninayo furaha kubwa kuwa nanyi ktk kubadilishana mawazo na kusaidiana pale tunapopata muda katika pitapita yangu nimekutana na hiki kitu hebu kiiangalie na ujiulize wewe upo ktk aina ipi kati ya hizo.

  AINA KUU NNE ZA MAPENZI DUNIANI

  "Vipi dada/ kaka, huyu ni mpenzi wako?" Wengi kati ya niliowauliza hawakupoteza hata nusu sekunde kujibu ‘NDIYO'.

  Lakini watu hao hao nilipowauliza kwa mara nyingine "Unampenda kwa sababu gani?" Majibu ya wengi yalikuwa na sababu ambazo si za msingi na wengine walinyamaza au kuambulia kucheka.

  Hebu wakati tunaendelea na mada hii, jiulize wewe mwenyewe ambaye una mke/mume swali kama hilo unampendea nini huyo mpenzi wako? Baada ya hapo sababu zinaweza kuwa ni kama zifuatazo " Nampenda kwa sababu ni mzuri wa sura, tabia, umbo, na kusema kweli ananivutia" la kama hizo hazitakuwa sababu sina shaka nawe utanyamaza au utacheka.

  Watalaam wa elimu nafsi na hasa Bw. Robert Stenberg walijitahidi sana kufanyia utafiti wa mapenzi na kuibuka na aina kuu kiasi cha nne ambazo wanazitaja kuwa ni PENZI LA UTIIFU, PENZI LA KUJALIANA, PENZI LA UIGIZAJI NA PENZI TIMILIFU.

  PENZI LA UTIIFU

  Penzi la utiifu au kama wengi wanavyolifahamu hujulikana kama ‘penzi la mahaba'. Katika aina hii ya penzi, wanaopendana hujali sana na kuendekeza zaidi miito ya kimwili. Mapenzi ya kiwango cha juu kabisa miongoni mwao hupatikana pale wanaposhiriki tendo la ndoa. Pia wanaopendana hupenda kuwa pamoja au karibu kwa muda mwingi.

  Lakini kwa bahati mbaya penzi la aina hii linakosa sifa moja ambayo ni kujitolea. Wapenzi kwenye penzi hili huonekana na pengine hujiona kuwa wanapendana, lakini unapofika wakati ambapo kujitolea kunahitajika, penzi lililoonekana kushamiri hupukutika ghafla.

  Kujitolea kunaweza kuwa na maana ya kuumia kwa ajili ya mwingine, kutoyumbishwa na watu wa pembeni na kuwa tayari kulinda penzi hilo kwa gharama yoyote. Kwa mfano ukiona mpenzi wako hayuko tayari kukusaidia unapoumwa, unapokuwa na matatizo, hakuhurumii unapokuwa taabuni ujue kuwa mapenzi yenu ni ya utiifu ambayo uhai wake ni mdogo.

  Jambo la kufanya hapa ni kwa wapenzi wenyewe kujitambua na kuchukua hatua za kukamilisha pengo la kujaliana ili kutowapa nafasi wambea na shida za dunia kuyumbisha meli ya penzi ambayo wanasafiria, ikishindikana watu hawa wanashauriwa kutokuwa wepesi wa kuoana kwani uwezekano wa ndoa yao kutodumu ni mkubwa.

  PENZI LA KUJALIANA

  Penzi la kujaliana ni lile ambalo wanaopendana wanakuwa karibu mara zote na kushiriki mambo mengi pamoja. Wapenzi wa kundi hili huwa na hali ya kujitolea tofauti na penzi la utiifu ambalo tumeliangalia, lakini kasoro yao kubwa huwa kwenye miito ya mwili. Jambo la kufurahisha hapa ni kwamba wapenzi wa kundi hili wako makini kwa kila sehemu na mara nyingi huwa hawakubali kuingiliwa maamuzi ya mapenzi yao.

  Lakini linapokuja suala la tando la ndoa hujitokeza kasoro nyingi za kutofikishana kileleni au kutofurahishana na hivyo anguko lao huletwa na muwasho wa mwili ambao huwasukuma wapendanao hao kutoka ndani ya uhusiano wao na kufanya usaliti.

  Sasa ili kulifanya penzi la aina hii liwe imara lazima wapenzi waulizane kuhusu kutimiziana haja za mwili wanapokuwa faragha. Kama kuna kasoro kati yao si busara kufichana wanatakiwa kuwaona wataalamu wa mapenzi na kupata ushauri utakaosaidia kuondoa tatizo hilo. Hawa pia wanashauriwa kutooana haraka.

  PENZI LA UIGIZAJI

  Penzi la aina ya tatu linalotajwa na watafiti ni lile lijulikanalo kama penzi la Uigizaji. Hili ni lile penzi ambalo wanaopendana hukutana asubuhi na ikifika jioni tayari ni wapenzi kamili, ambapo hugandamana kama ruba, utadhani waigizaji wako kwenye matayarisho ya filamu. Ukiwatazama wanakuwa kama vichaa na msukumo wao wa kutimiza hisia za mwili huwa ni mkubwa kiasi cha kufikia kufanya mapenzi hata barabarani au kwenye sehemu za wazi.

  Wapenzi wa aina hii huchukua muda mfupi sana kutangaziana mambo ya ndoa na pengine kuoana bila kufahamiana zaidi kitabia. Wanajuana asubuhi na jioni mwanamke/mwanaume keshahamia kwa mwenzake na maisha yanaanza, hapo hakuna ushauri wala muongozo wa watu wengine.

  Tatizo kubwa ambalo hujitokeza katika penzi la aina hii ni wapenzi kuchokana mapema na hamu ya kufanya tendo la ndoa kupotea. "Yaani nikiwa na mume wangu sijisikii kabisa kufanya naye mapenzi, lakini kwa wengine nakuwa na hamu sana" hizi ni kauli za wapenzi wa penzi la kisinema sinema.

  Mbali na hilo wapenzi wa aina hii ni rahisi kuporwa na kuanzisha uhusiano mpya, hivyo inashauriwa kuwa kwa wale ambao wanaona kuwa wako kwenye kundi hili, wajitahidi kujizuia na kupeana nafasi za kujuana zaidi kupitia ushauri wa watu wengine. Si vema kushiriki tendo la ndoa kila mara kwa staili na sehemu zile zile na pia haifai kukurupuka kuoana bila kuchunguzana tabia, ndoa za hivi hazidumu.


  PENZI TIMILIFU

  Aina ya mwisho ya penzi kama inavyoelezwa na mtaalamu Sternberq ni ile ya penzi timilifu. Aina hii ya mapenzi inakuwa na sifa zote tatu, yaani TENDO LA NDOA. Kwamba wapendanao huwa hawana kasoro katika eneo hili, unapofika muda wa kupeana raha hufikishana mahali pa juu. UKARIBU kwamba muda wote huwa karibu na kila mmoja hakai na kiu ya kutokumuona mwenzake kiasi cha kupoteza hisia na kushawishika kufanya usaliti.

  Sifa ya mwisho ni KUJITOLEA. Ni mahodari kusaidiana, kufarijiana na hawako tayari kupokea mambo kutoka pembeni yanayohusu uhusiano wao, hivyo huwa si rahisi kwao kuyumba kwa sababu za umbea. Kumbuka katika penzi hili tendo la ndoa huwa si sehemu muhimu sana kwa wapenzi, yaani kwao penzi ni rohoni zaidi kuliko mwilini hata wakikaa muda wa miezi mitano bila kufanya tendo la ndoa upendo wao haupungui.

  Hata hivyo, penzi la aina hii kwa mujibu wa wataalamu ni vigumu kupatikana na ni vigumu pia kulilinda, lakini linatajwa kuwa ni aina ya penzi bora ambalo ni muafaka kwa maisha ya baadaye ya ndoa kwa wanaopendana. Watu wengi kwa kutotambua aina hii ya mapenzi wamejikuta wakiliharibu kwa kufikiri tu kwamba wapenzi wao wamefika na hivyo kufanya makusudi ya kuharibu misingi ya penzi.

  "Nimeshamshika atakwenda wapi, nikikohoa tu anaitika" Kauli kama hizi ni hatari sana katika penzi hili, hivyo inashauriwa ukiona unapendwa na mpenzi wako katika aina hii ya penzi ni vema ukawa macho ili kutolivunja kwa uzembe wako na kudhani unababaikiwa kumbe unapendwa kwa dhati.
   
 2. somba kankara

  somba kankara Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya wana JM wewe umempendea nini huyo na kutokana na aina hizo wewe upo katika aina ipi na nini ufanye ili kulekebisha mapenzi yenu
   
 3. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi nipo hapo PENZI LA UIGIZJI, penzi hili ni tamu sana na halina usumbufu kwangu, mnakutana hasubui, jioni kimeeleweka, asubuhi yake mbio kutafuta maisha huku mawazo yakiwa kwenye kazi badala ya kumuwaza mwanamke, penzi hili halina stress, na unapokuwa stress free anaweza kuyafanya mambo yako kwa ustadi zaidi na unakuwa na furaha ya maisha.
   
 4. P

  Pedeshee kiraka Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani mie cjifamu nipo kwenye aina ipi?
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Somo zuri, ila sina jibu la swali ulilouliza.
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 160
  knowledge nayo ikizidi inaharibu.
  Sasa hivi nina digirii ya hiari ya mapenzi kinadharia.
   
 7. k

  kabye JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 355
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pouwa pouwa
   
 8. somba kankara

  somba kankara Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pedesheee acha utani wewe
   
 9. somba kankara

  somba kankara Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi nipo hapo PENZI LA UIGIZJI, penzi hili ni tamu sana na halina usumbufu kwangu, mnakutana hasubui, jioni kimeeleweka, asubuhi yake mbio kutafuta maisha huku mawazo yakiwa kwenye kazi badala ya kumuwaza mwanamke, penzi hili halina stress, na unapokuwa stress free anaweza kuyafanya mambo yako kwa ustadi zaidi na unakuwa na furaha ya maisha.

  so hauoni kuwa unakuwa ktk hatari kubwa ya kupata maambukizi maana mkeo au mchumba ni lahisi kuporwa
   
 10. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Well said. Nimetafakari mahusiano yangu na mchumba wangu nikagundua tumepitia stages kadhaa katika hizo aina za mapenzi.

  Na sasa tunaelekea kwenye TIMILIFU!
   
 11. MMDAU

  MMDAU Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndugu naoana kama kuana aina nyingine hapa zimekosekana kwani mm mbona sijioni kama vile kila sehemu nipo kidogo kidogo so nikijumlisha napata kuwa nipo ktk penzi la aina za mapenzi
   
 12. L

  Lindongo Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mada yako ni nzuri na imenifungua, maana nilikuwa sifahamu aina hizi za mapenzi na jinsi ya kuboresha penzi.
   
 13. Krait

  Krait JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2014
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 1,408
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mi nipo single
   
 14. I

  ISIMBA Senior Member

  #14
  Mar 25, 2014
  Joined: Feb 7, 2013
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bonge ya somo chaliangu, naitamani sana hyo aina ya nne, hili nlilonalo sijui ni aina gani kati ya hzo ila sio la Maigizo...
   
 15. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,888
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  team Bravo.. no reason to love.

  but to pass by for the next hit..
   
 16. ngungwangungwa

  ngungwangungwa JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2014
  Joined: Jul 23, 2013
  Messages: 522
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Dah,me hata sijui npo wapi! Ngoja nimwambie mke wangu tusome wote then tujadili wote na tujue tupo kundi gani!!
   
 17. MankaM

  MankaM JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2014
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 9,493
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Tunashukuru
   
Loading...