Malaika wa Misukosuko
JF-Expert Member
- Jul 16, 2021
- 1,744
- 5,071
Moja kati ya makocha ambao nimekuwa nikitazama mechi zao kadhaa za nyuma basi ni huyu kocha Zidane ila kitu nlichogundua ni kwamba huyu jamaa ni kocha wa kawaida mno kimbinu, aliweza kuchukua makombe ya UEFA back to back kwasababu tu ya uwepo wa CR7 akiwa kwenye peak yake na aina wachezaji waliopo madrid,
Na ndomaana mpaka sasa hana timu tangu kaondoka Real madrid hakuna timu iliyompa ofa kwasababu wameangalia aina ya mpira wake ni wa kizamani sana na ni kocha wa mbinu moja tu kitu ambacho modern football haitaki kwa sasa,
Kuna mtu atasema mbona aliweza kubeba makombe ya Uefa back to back akiwa madrid ? Jibu ninalo weza kukupa ni kwamba Madrid ni aina ya Timu ambayo unaweza mchukua hata Peter Msechu tukamvalisha suti na Tai ndefu na kumkabidhi timu na akabeba Makombe kama hana akili nzuri,
Siku zidane akipata kazi nje ya klabu ya madrid mtakumbuka maneno yangu huyu kocha hatokuja kubeba tena kombe la Uefa akifundisha timu nyingne tofauti na Wafalme wa Soka duniani Real madrid.