Ziara ya rais na sare za CCM

Ziara ya rais na sare za CCM

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,250
Reaction score
893
waziri+wa+kilimo+christopher+chizza+akielezea+mipango+kabambe+ya+kilimo.JPG
Hapa ndipo nakubaliana na watu wengi wanaotaka tume ya Taifa ya uchaguzi ( NEC) isiichie tu katika uchaguzi, inatakiwa iratibu pia programu za Elimu ya uraia kuwafundisha watu maana ya mfumo wa Vyama vingi na Demokrasia Tanzania.Hii inajidhihirisha katika ziara za kiserikali za Viongozi wa Kitaifa kuonekana kama mkutano wa CCM, ambapo mbwembe za kichama zikiwamo sare, na midundiko hutawala hali inayoashiria kuwa watu hawatofautishi shughuli za kichama na za Kiserikali. Utakuta ofisi za Chama zina hekaheka, kuandaa maandamano ya bodaboda, sare n.k vitu ambavyo vinapunguza utaifa wetu. CCM wafundishe watu wenu na vyama vingine pia, kuwa shughuli za kiserikali hazitakiwi kuwa na sura ya Kichama.
waziri-wa-nishati-na-madini-profesa-sospeter-muhongo-akieleza-mikakati.jpg
 
Kwa jinsi walivyo jipanga, Labda hawa ni greengurd wa ukeli sio wale watekaji
 
mkuu unakurupuka tu bila kutuambia ilikuwa ni ziara ya rais wapi!!!mimi naona ilikuwa ziara ya kichama until you convince me otherwise..tuambie ilikuwa wapi mkuu.
 
Obama alimweleza Vasco da Gama bila kuuma maneno kuwa "demokrasia ni zaidi ya uchaguzi" lakini yeye bado hajaelewa. Na ndio maana anawashawishi wananchi fukara wavae manguo ya green njano.
 
Back
Top Bottom