Slas Nature
Member
- Oct 18, 2013
- 36
- 72
Magufuli, Simiyu: Niwaahidi hatutowaangusha, nimekuja kuwashuku na nafikiri shukrani zangu mmezipokea.
-Magufuli, Simiyu: Yale yetu tuliyoyaahidi kwenye ilani ya chama cha mapinduzi tutayatimiza.
-Magufuli: Ukichukua hatua zozote wapo watakaolalamika, sitabadilika, msimamo wangu uko palepale, tunataka kutengeneza Tanzania mpya.
-Magufuli: Bariadi inaongoza kwa kutengeneza pamba, dhahabu zipo, hifadhi kubwa ya taifa, Kwanini Tanzania tuwe maskini?.
-Magufuli: Kila mmoja anapenda maisha mazuri na huduma nzuri, sisi viongozi tuna wajibu wa kutekeleza.
-Magufuli: Haijawahi kutokea Tanzania kupanga bajeti 40% kwenda kwenye maendeleo, lazima kuna watu wamekwazika.
-Magufuli: Mnaosikia wanalalamika walikua wananufaika na hizo fedha, ilifikia mahali hatuna hata ndege.
-Magufuli: Mnaosikia wanalalamika walikua wananufaika na hizo fedha, ilifikia mahali hatuna hata ndege nchi ya watu milioni 50.
-Magufuli: Hakuna nchi yoyote duniani iliyofanikiwa kwenye utalii bila kuwa na shirika lake la ndege, tumeamua kuinua utalii.
-Magufuli: Nilikua naongea na waziri, tuone uwezekano wa kujenga kiwanja cha ndege hapa Bariadi mwaka kesho.
-Magufuli: Katika maendeleo machungu lazima yawepo, niwaombe radhi walioumia lakini ni kwa ajili ya maendeleo ya Simiyu.
-Magufuli: Anaetangaza njaa ni Rais, mie ndio nimepewa jukumu la kuwaongoza watanzania.
-Rais Magufuli: Wataandika lakini sitasikiliza, siasa tuziacha, twende na ukweli.
-Rais Magufuli: Nataka niwaeleze ukweli, nimesomewa ripoti hospitali itatumia bilioni 46, hiki kitu hakiwazekani.
-Rais Magufuli: Nasema haiwezekani, nataka hospitali hiyo ikamilike sio kwa pesa hizo mlizozipanga. Ntaleta bilioni kumi jengo liishe.
-Rais Magufuli: Kama yupo kiongozi wa TBA anaweka estimates kubwa, mfukuze kazi, barabara ikifunguliwa ajali zitaongezeka, hospitali lazima.