Ziara ya Rais Magufuli mkoa wa Mara, tafrani tupu kwa viongozi wa mkoa, wanasiasa na wananchi

Addis Ababas

JF-Expert Member
Aug 5, 2018
351
353
Mkoa wa Mara hauko sawa kiuchumi, unahitaji mkakati mpya wa kuchochea uchumi.

Kwa kulijua hilo CCM wakaja na mradi wa chuo kikuu, Mwl Nyerere University of Agriculture and Technology, wa tsh 770 billion.

Mradi huu kama ilivyo kwa miradi mingine ya mkoa huu una miaka zaidi ya 10 bila kutekelezwa. Uchaguzi wa 2015 ulipokaribia, wakateuliwa viongozi na wakaajriwa watumishi...lakn hakuna wanafunzi hadi sasa, hawa wamekaa bila kazi...

Inasikitisha kuona, Rais kaenda Mara hakuna aliyeulizia mradi huu kwa Rais. Mradi huu n wa mkoa kwani kwa mjibu wa Draft charter ya chuo, chuo kitakuwa na matawi ktk wilaya zote za mkoa... Tazama pp 76, 77 za charter.

Nyerere anasifiwa, lakn hakuna chochote cha maana kinachofanyika. Hospital ya mkoa ina miaka 40bila kukamilikka, barabara ya Arusha - Musoma miaka 55 bila kukamilika, mama Maria anaoga maji ya kopo, hata kaburi la Nyerere ni Mandela ndo aliyetoa hela za kulijenga, mwl Nyerere Foundation hawana hata senti ya kufanya kazi zake. Aibu!
 

Attachments

  • charter-mjnuat_2016.pdf
    448.4 KB · Views: 52
Kaburi la Nyerere lilijengwa kwa hela zilizotolewa na Mandela? Serious?
 
Inasikitisha kuona, Rais kaenda Mara hakuna aliyeulizia mradi huu kwa Rais. Mradi huu n wa mkoa kwani kwa mjibu wa Draft charter ya chuo, chuo kitakuwa na matawi ktk wilaya zote za mkoa... Tazama pp 76, 77 za c
Inashangaza Rais anatoa fursa ya kuuliza kero za jumla za kimkoa huonekani,hata kutums sms kwa mtu akuulizie umeshindwa unakimbilia jf
 
Inashangaza Rais anatoa fursa ya kuuliza kero za jumla za kimkoa huonekani,hata kutums sms kwa mtu akuulizie umeshindwa unakimbilia jf
Wale wanaouliza maswali tayari wameshapangiwa cha kuuliza nenda wewe utanyoosha mkono hadi upinde hupewi mic kuzungumza

Wale wenye GPA ya 32 ndio watakao uliza maswali
King comedian
 
Ndo hivyo... Mandela alitembelea Butiama Nyerere akiwa keshafariki, akakuta kaburi n "tuta". Alisikitika, lakn hakusema chochote... Baada ya kurudi South Africa ndo akatuma hela, kaburi likajengwa...
Aisee ccm wana dhambi hadi zisizofikirika.
 
ukweli wachawi wa mkoa wa mara ni watu wa mara wenyewe kwani wakishaondoka hawana tabia ya kukumbuka kwao wote wanajifanya kumuiga Nyerere kutopeleka maendeleo kwao tutabaki tukilaumu serikali lakini ukweli ndio huo
 
Inashangaza Rais anatoa fursa ya kuuliza kero za jumla za kimkoa huonekani,hata kutums sms kwa mtu akuulizie umeshindwa unakimbilia jf
Kwani ndiyo kusema kichaa hayajui haya hadi aulizwe ? Kichaa a.k.a jiwe anafanya usanii tu.
 
Back
Top Bottom