Ziara ya Rais Kikwete Hazina na 'Long Room' (leo)

Kumbe anakumbuka kufanya ziara nchini?? mi nilifikiri yupo Ughaibuni anakula gud tym.
Big up Kikwete kwa kuanza kufanya ziara nchini!
Hii siyo ziara. Kutoka ofisi yake Ikulu kwenda Hazina ni kama mita 300 hivi. Kwenda TRA/Long Room ni kama nusu kilometa. Hata bila yeye kwenda huko angeweza kuwaita wahusika wakaenda ofisini kwake na taarifa alizozitaka. Ni zuga zake za kila siku.
 
Ziara uchwara tu hizi .Hazina manufaa makubwa kwa Watanzania. Amehisi reputation yake imepotea kidogo akaamua ajitokeze ili vyombo vya habari viandike watu wajue yupo.
Hebu tujiulize ile ziara alifanya bandarini kwaka jana kama sio juzi, je ina mafanikio???????????? Jibu ni hapana. Zile zilikuwa nguvu za soda tu. Maana ukifika bandarini utajionea jinsi usumbufu wa kutoa mizigo bandarini ulivyo! Pia fuatilia Miundo mbinu mingine kwishny!
 

Nakubaliana na wewe mkuu. Kama mapato yameongezeka kwa mara mbili kwanini huduma za jamii ndo zinazidi kuwa mbovu? Umeme, maji, hospitali, shule za kata n.k. Watuambie hizo pesa zetu zinakwenda wapi?
 
Anatafuta cavarage katika magazeti , TV na radios baada ya kuona ''Babu'' kafunika
 
JK anapaswa kutowasikiliza wakuu wa idara tu bali ashuke kwa akina kayumba wampe physical data za yanayojiri kwa wateule wake kiutendaji na UOZO uliopo.
 
Kwa hali ya Tanzania ilivyo hivi sasa Rais anatakiwa awe sites muda wote, sio anasubiri wakati ambao hana safari za kwenda nje ya nchi tu ndio anakwenda kukagua.

Hivi mkuu wa kampuni kama atakuwa muda mwingi anafuatilia mambo ya nje ya kampuni na kuacha ya ndani si kampuni itakufa kabisa. Hii ni hivyo hivyo na rais wa nchi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…