Ziara ya Prof Muhongo kusini

kumusoma

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
566
890
ZIARA YA PROFESA MUHONGO KUSINI

Waziri wa Mishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amehitimisha ziara yake ya Kusini kwa kutembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Somangafungu cha wilayani Kilwa.

Waziri Muhongo amesema katika ziara hiyo amegundua yafuatayo:

🔹Mitambo ya Mtwara na ya Somanga Fungu inao umeme wa ziada ambao aliagiza kuangaliwe namna ya kupeleka ziada hiyo kwenye gridi. Hadi kufikia Februari mwakani mipango iwe tayari.

🔹Uzembe wa matengenezo ya mitambo kwa mfano mtambo mmoja wa Somangafungu umeharibika tangu 2012 hadi hii leo service haijaanza japo ilielezwa kuwa itaanza mwakani Januari kwani vipuri vimeagizwa.

🔹Ameagiza mazungumzo na Kilwa Energy ambao watajenga mitambo ya kuzalisha megawati 320 hapo Somangafungu yakamilike kufikia Februari mwakani.

🔹Aligundua kuwa kiwanda cha Dangote kimefikia hatua ya kununua makaa ya mawe nje ya nchi wakati Tanzania pia yanapatikana kwa wingi.

🔹Ameagiza wiki ijayo Wizara, Tanesco, TPDC na Stamico wakutane na Dangote kuzungumzia suala la kumuuzia Gesi Asilia na makaa ya mawe kwa ajili ya kuzalisha umeme

🔹Amehitimisha kwamba Tanesco wabadilike na wawe wabunifu na pia wasiwadanganye wananchi kwa taarifa za mabwawa wakati kuna mitambo mingine ipo tu na haitumiwi.

🔹Amesema hadi kufikia Februari mwakani kwa wafanyakazi wa Tanesco ambao itaonekana wameshindwa kutatua kero mbalimbali kama alivyoagiza itabidi waondoke.

🔹Alimalizia kwa kusema yeye binafsi kama ilivyo kwa Watanzania wengine haiamini Tanesco ndio sababu ameamua kufanya ziara kwenye mitambo yote ya kuzalisha umeme ili kujionea hali halisi.

Waziri Muhongo alifika Mtwara leo asubuhi na kutembelea Kituo cha kuzalisha Umeme cha Mtwara baada ya hapo alielekea katika kituo cha kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kisha akatembelea Kiwanda cha Saruji cha Dangote na kumalizia katika Kituo cha kuzalisha umeme cha Somanga Fungu.
 
Kwani professor Muhongo ameacha kuwa professor muongo?
CC Dr.Kingwangala
 
Hivi professor kazi anayoifanya mbona ni acceptable, kulikoni ITV?
Au kale kamsala na TOP wa ITV kanaendelea?
Yaishe Tujenge nchi.
Au kosa professor to talk the truth about local investors on gassing project?
He was right!
 
Professor anafanya kazi kwa nia anagundua na ambayo tulikua hatuyafaham
Mungu mpe afya na muongezee umri
 
Mambo mengi njamaa za wanufaika na mgao wa umeme.

Sitashangaa kusikia orodha ya watu hao itakayomuaucha kila mtu hoi.

Wamekuwa wakisingizia maji wakati hatusikii hayo Zambia, Zimbabwe na Msumbiji ambao pia wanategemea Hydro Power
 
Safi sana Prof Muhongo, piga kazi baba hakuna kulala
 
"Amehitimisha kwamba Tanesco wabadilike na wawe wabunifu na pia wasiwadanganye wananchi kwa taarifa za mabwawa wakati kuna mitambo mingine ipo tu na haitumiwi."

Kwanini viongozi wengi wa tanzani ni waongo?. Magufuli kashasema msema kweli ni mpenzi wa mungu. Inabidi tujifunze kuwa wakweli. (
Afadhali kuwa na jirani mchawi kuliko mwongo)
 
kungekuwa na viongozi 20 kama prof muhongo hakika tanzania ingekua kama china economically.
 
Mimi aliniudhi aliposema watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gasi, wanaweza kuwekeza kwenye juisi na maji1 kujidharau hata kama ni msomi kiasi gani! inferiority complex!
 
Mimi aliniudhi aliposema watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gasi, wanaweza kuwekeza kwenye juisi na maji1 kujidharau hata kama ni msomi kiasi gani! inferiority complex!

Hii kauli ilipotoshwa alichotoa ni ushaur tu kwani gesi ni very risk na kwa mitaji yetu ukiikosa wakati umekopa matrilion lazima uruke kichaa. Hata mabenki nchini hayana hicho kiasi cha pesa kukopesha wazawa kuinvest huko, na ndiyo maana haya TPDC wameishia kuwa wamiliki wa leseni za vitalu vya na teknolojia wamewaachia makampuni ya nje, na mgao wanaupata kwa kuwa leseni zote za vitalu ni zao. Sasa kama watu wanabisha hii kauli ya muhongo waende hapo TPDC kutaka kitalu waone kama watanyimwa, maana watu wanalalamika weee zabuni zikitangawa hatujitokezi. PROF was right.
 
Back
Top Bottom