barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Leo Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amefanya ziara ktk Mkoa wa Iringa,lengo ikiwa ni kuwatembelea wananchi wa Tarafa ya Pawaga baada ya kupatwa na mafuriko.Waziri Mkuu alitua katika uwanja wa Nduli na baadae akapelekwa kuwatembelea wahanga hao katika eneo la bonde la mto Ruaha na Tarafa ya Pawaga
Ziara hiyo imewakutanisha Mh.Mbunge wa Jimbo la Iringa ndugu Peter Msigwa na DC Kasesera ambao siku za hivi karibuni walionekana ktk video mtandaoni wakitofautina.Mafuriko hayo yameacha watu wengi bila makazi,chakula na pia kusababisha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.Tarafa ya Pawaga ipo ktk Jimbo la Isimani la Mh.William Lukuvi.
Baada ya mafuriko hayo kutokea,ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Ofisi wa Waziri Mkuu waliamua kuchukua vijana wa JKT-Mafinga ili kuja kutengeneza makazi ya muda kwa wahanga wa mafuriko hayo.Kambi ya wahanga wa mafuriko hayo ipo katika Kijiji cha Kisanga,kitongoji cha Kilala ktk Tarafa ya Pawaga.Misaada mbalimbali imeendelea kutolewa na serikali na watu binafsi.