Ziara ya Kyombo kata ya Kassambya jimbo la Nkenge mkoani Kagera

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
740
479
Mbunge wa Jimbo la Nkenge, tarehe 09 Agosti, 2023 ameendelea na ziara yake ya Jimbo katika Kata ya Kassambya iliyopo Wilayani Missenyi, Kagera.

Katika ziara yake amehudhuria Kikao cha ndani CCM Kata ya Kassambya, amewapongeza viongozi wa CCM wa Kata hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kukisaidia Chama Cha Mapinduzi na Serikali kuwaongoza Wananchi. Katika Kikao hicho Mhe. Mbunge wamewakabidhi viongozi vitendea kazi ikiwemo Bendera za Chama, Sare za Chama (T-shirt), Karatasi (Ream papers), Kalamu, Mipira kwa ajili ya Michezo, Runinga Kwa ajili ya Wazee wa Bunazi

Pia Mbunge Kyombo amefanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Kassambya na kusikiliza kero zao. Mbunge Kyombo amewaeleza Wananchi waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani chama hicho kina dira na Mipango mizuri ya Kuleta Maendeleo kwa Taifa la Tanzania.

Wananchi wa Kata ya Kassambya wamemshukuru Mhe. Mbunge Kwa kazi kubwa ya Uwakilishi anayofanya Bungeni na kuhaidi kutoa ushirikiano wao kila wakati kwa Maslahi mapana ya Taifa. Pia, Wananchi hao wamemkabidhi Mhe. Mbunge Zawadi ya Mbuzi ikiwa ni ishara ya kuendeleza Umoja na Ushirikiano.

Mbunge Florent Kyombo amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya Kuleta Maendeleo katika Nchi yetu.View attachment 2714393View attachment 2714394View attachment 2714397View attachment 2714395View attachment 2714396View attachment 2714398View attachment 2714399View attachment 2714400
255754274709_status_f9a987ce2998428aa8f28e97cd555c10.jpg
255754274709_status_9f44d1270e0c4157abf4420f1a65a4e1.jpg
255754274709_status_624e85cf17854f5fbecb5b47a8e14129.jpg
255754274709_status_ca1411c46bb04d669f11e1118fa9fdff.jpg
255754274709_status_d5859168cb4a46f68038cb6d425a1af5.jpg
255754274709_status_aacb3aaf2e16452aa62a9a7a412e1619.jpg
255754274709_status_8b5177978176447b8ca2d07cfbfe3349.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom