Ziara ya Kinana Arumeru Magharibi

Ziara ya Kinana Arumeru Magharibi

security guard

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
799
Reaction score
603
​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Oldonyosambu.

​
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Oldonyosambu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM.

​
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye akisalimia wananchi wa kijiji cha Oldonyo Sambu waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha Chama.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kijiji cha Oldonyosambu ambao walijitokeza kumpokea alipowasili kwenye jimbo la Arumeru Magharibi.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua daraja la Kisongo.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi kwa kupeleka zege kwenye eneo husika wakati wa ujenzi wa daraja la Kisongo.
​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya shina la wakereketwa la Mateves kama ishara ya kufungua rasmi shina hilo.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kata ya Kisongo mara baada ya kushiriki ujenzi wa daraja la Kisongo.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nduruma ambao walikuwa na malalamiko juu ya mradi wa maji wa Nduruma kuonekana kupelekwa mashambani badala ya maeneo wanayoishi watu.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kutoka wilaya ya Arumeru Magharibi Ndugu Mathias Manga wakati wakiwasili kata ya Mlangarini tayari kushiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha kijiji cha Manyire.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege wakati wa ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jengo la kituo cha afya cha Manyire kutoka kwa MNEC Mathias Manga.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wazazi,walimu na wananchi waliojitokeza kumsikiliza alipotembelea shule ya Sekondari ya Sokon II

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi katika shule ya sekondari ya sokoni II.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya wilaya ya Arymeru Magharibi

​
Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Arumeru Magharibi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
​
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni,Arusha.

​
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo alitoa sababu mbali mbali za dalili za kufa kwa upinzani nchini.

​
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa CCM wilaya ya Arumeru Magharibi uliofanyika Ngaramtoni shule ya Msingi ambapo alitoa sifa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa kazi nzuri ya kuimarisha Chama.

​
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ya sasa haitofanya makosa, na kuwahakikishia kila atakayefanya makosa itabidi aubebemsalaba wake.

​

Kinana anazungumzia ccm IPI? Tathminini ya ziara zilizopita ilikuwaje? Waliwajibishwa wangapi? Mbona utendaji mbovu unazidi kushamiri? Mbona watendaji wabovu wanazidi kulindwa? Kinana unaongelea ccm IPI? Labda ya kufikirika labda ya kusadikika labda ya ndotoni...!
Maneno ya kama ' ccm mwaka huu haitafanya makosa tena' yamekifu masikioni mwa wananchi
 
This kinana needs to be refered to Apollo in India.
 
Watu ni wachache sana mpaka aibu

Hapa ni kwenye Jimbo la aliyekuwa mgombea Urais kupitia tiketi ya CHADEMA 2010, Babu Dkt. Slaa.

02.JPG

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Karatu jioni ya leo, 17 Machi 2015.

Kinana ambaye yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, alishuhudia Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na Chadema imekataa kutoa sh. mil 60 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Baray Mbuga Nyekundu kwa sababu Kata hiyo inaongozwa na Diwani wa CCM.
01.JPG

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika ziara ya Mkoa wa Arusha, akihutubia pia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Karatu
 
arumeru hakuna fisi wa kucheza nae???
 
Attachments

  • 1426736769095.jpg
    1426736769095.jpg
    40.7 KB · Views: 96
  • 1426736782388.jpg
    1426736782388.jpg
    47.9 KB · Views: 93
MwanaDiwani

Mwana diwani hizi nyomi zipo popote na wakati wote, hiyo ilipaswa iwe kazi ya upinzani! ccm kama chama tawala inatakiwa ifanye mengine zaidi ya hiyo mikutano ya HADAA, hasa kufanya overhaul kubwa serikalini na kwenye chama, kitu ambacho ni ndoto isiyowezekana

Uvundo umejaa serikalini na kwenye chama nyie badala ya kuusafisha mnauvundika kwa maguo ya mikutano ya hadhara iliyojaa hadaa, mnajichimbia kaburi kubwa niamini
 
Last edited by a moderator:

Ndugu mshana jr

Ninadhani unajenga hoja bila kuelewa msingi wa hoja unayoijengea. Kwa lugha nyingine wanasema, unadandia basi kwa mbele.

Bandiko langu limelileta baada ya huyu mdau kusema hivyi;
Watu ni wachache sana mpaka aibu

Ninakubaliana kiduchu na hoja yako kwa sababu pia mikutano ni sehemu ya kukutana na wananchi nilishawahi kukisema katika thread hii;

Nilisema hivi;
Ndugu,

Hoja zako haziwezi kusimama kwenye ukweli.

Kama maandishi huwezi kuyasoma, hata kuangalia picha nazo unataka msaada.

By the way, Sera ya CCM ni kutenda na siyo kujaza watu kwenye mikutano ili ijipime.

Wananchi wengi hawahitaji kuelezwa Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa sababu wanaziishi.

Tunawaachie hiyo sera kwa sababu CCM ilishajipima kuanzia mwaka 1995 kwenye chaguzi kuu na ndogo.

Hoja ya kujipima kama mnakubalika inawafaa kwa sababu hamna uhakika kama mnakubalika na mtashinda katika chaguzi.
Ziara zetu ni zaidi ya kufanya mikutano ya hadhara, ndiyo maana hatutumii chopa ingawa uwezo wa kufanya hivyo tunao!
 
Ndugu mshana jr

Ninadhani unajenga hoja bila kuelewa msingi wa hoja unayoijengea. Kwa lugha nyingine wanasema, unadandia basi kwa mbele.

Bandiko langu limelileta baada ya huyu mdau kusema hivyi;

Ninakubaliana kiduchu na hoja yako kwa sababu pia mikutano ni sehemu ya kukutana na wananchi nilishawahi kukisema katika thread hii;

Nilisema hivi;

Ziara zetu ni zaidi ya kufanya mikutano ya hadhara, ndiyo maana hatutumii chopa ingawa uwezo wa kufanya hivyo tunao!

Bado nishauri tu kwamba kuna mengi ambayo ccm ikiyafanya yatakuwa na positive impact kubwa sana kuliko hiyo mikutano ya hadhara na picha kama hiziView attachment 235828View attachment 235829View attachment 235830hakuna umakini hapa!
Wananchi wanakusanyika kwa wingi ili kuangalia vituko, wanakuwa na furaha ya muda katikati la lindi la ufukara wa kutisha

ccm ilishajenga chama kimekomaa hakihitaji hizi ziara kwasasa na propaganda tasa kuna mambo yanatakiwa yafanyike kwa vitendo,
-matamko yameshatosha
-mabandiko yameshatosha
-maonyo na makemeo pia
Kama chama tawala kinatakiwa kuchukua hatua sasa kuanzia wakati ule wa kuvua gamba mpaka escrow
 
Mazungumzo yako yoooote yanaonyesha haujui kazi ya siasa, wala hujui tafsir na maana ya uimara wa chama cha siasa.
 
Mazungumzo yako yoooote yanaonyesha haujui kazi ya siasa, wala hujui tafsir na maana ya uimara wa chama cha siasa.

Inategemea una uelewa gani kwenye nini na una mtazamo gani kwenye nini! Siasa haina formula na kama IPO basi ni moja tu SIASA HAITAKI USALITI
 
Mwana diwani hizi nyomi zipo popote na wakati wote, hiyo ilipaswa iwe kazi ya upinzani! ccm kama chama tawala inatakiwa ifanye mengine zaidi ya hiyo mikutano ya HADAA, hasa kufanya overhaul kubwa serikalini na kwenye chama, kitu ambacho ni ndoto isiyowezekana

Uvundo umejaa serikalini na kwenye chama nyie badala ya kuusafisha mnauvundika kwa maguo ya mikutano ya hadhara iliyojaa hadaa, mnajichimbia kaburi kubwa niamini
Mhhh we umeshashindikana, hata haujielewi, ngoja nijiandae kufanya yangu asubuhi hii niachane na haya maujinga.
 
Mhhh we umeshashindikana, hata haujielewi, ngoja nijiandae kufanya yangu asubuhi hii niachane na haya maujinga.

Usijali JS fanya yako ila kumbuka ujinga kwako, elimu kwa wengine! ni mtazamo tu...! Sitaki kukukumbusha mengi utachachuka asubuhiasubuhi
 
Mazungumzo yako yoooote yanaonyesha haujui kazi ya siasa, wala hujui tafsir na maana ya uimara wa chama cha siasa.
Kweli wewe dada hauna aibu ulivyokuwa chadema ulikuwa unatukana ccm kweli unadhani wameisha sahau?wanakuona kwa jicho la tatu huku wakilipiza kwako mf wanakutongoza wote na unawakubali kisha wanakuona kama mdudu.ndio mahana juzi unamlazimisha kinana aongee na mkuu wa kaya ili upewe ukuu wa wilaya.sahau hilo.wewe ni ndumila kuwili haujui ni nini unafanya.be carefully na siasa zako.

swissme
 
Mazungumzo yako yoooote yanaonyesha haujui kazi ya siasa, wala hujui tafsir na maana ya uimara wa chama cha siasa.

ccm ya kina nyerere haikuwa hii juliana! Sisi tumezaliwa na kukulia ccm iliyokuwa ina accept chalenge! Nyerere aliwaambia watanznia waz kuwa nchi imefilisika tangu tutoke vitan tunapaswa kukomaa na kidogo tulichokuwa nacho! Wananch walimuelewa na wakakomaa kwel kwel! Nyie nchi imewashinda inaendeshwa kwa kanun za geto bado tu mnaendelea na hadaa! Hak ya Mungu mkifa nyie makaburi yenu yatachimbwa mita nne zaid kwenda chin! Yaani mtafukiwa mbali sana!
 
Na mimi ni miongoni mwa 'nyomi'hiyo hapo!huwa sikosi mikutano ya ccm kila nipatapo nafasi kwani ni fursa nzuri ya kujipatia kipato cha bwerere.
 
Back
Top Bottom