GE2025 Ziara ya Dkt. Emmanuel Nchimbi: Kero ya Mikutano ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro

GE2025 Ziara ya Dkt. Emmanuel Nchimbi: Kero ya Mikutano ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
16,029
Reaction score
26,231
CCM inakutana na changamoto kubwa katika kukusanya wanachama kwenye mikutano bila kuzingatia muda wa watu. Kwa mfano, Dr. Emmanuel Nchimbi alipokuwa katika ziara ya mkoa wa Kilimanjaro, wanachama wa CCM walipata tangazo kuwa atawasili Jimbo la Hai saa 2 kamili asubuhi.

Hata hivyo, wanachama walikusanyika uwanjani kuanzia saa 12 asubuhi, na Nchimbi alifika Hai saa 4.45 asubuhi. Hali hii imesababisha malalamiko makubwa miongoni mwa wananchi, kwani inawafanya wahisi kukosa thamani ya muda wao, na hivyo kuichukia mikutano ya CCM.

Kero hii haijakosa kuathiri maeneo mengine pia, kama vile Jimbo la Siha, Vunjo, na Moshi Mjini. Wananchi wamekuwa wakifika uwanjani mapema, hata saa 3 asubuhi, lakini Dr. Nchimbi anawasili kati ya saa 7 hadi saa 10 jioni.

Hali hii inazidisha hasira na kukosekana kwa uvumilivu miongoni mwa wananchi, ambao wanatarajia mikutano iwe na mpangilio mzuri na wa wakati.

Wananchi wanashauri kuwa ikiwa Nchimbi anatarajia kufanya mikutano na kuwataka kufika mapema, basi ni bora angewaambia wafike saa 9 mchana ili wapate fursa ya kula chakula nyumbani kabla ya kuja, badala ya kushinda njaa barabarani.

Hii ingesaidia kuboresha uzoefu wa mikutano na kurudisha imani kwa wananchi.
 
Wanaoenda kwenye hii mikutano ni watu ambao wamekosa cha kufanya, kwa hiyo hata wakishindishwa siku nzima hakuna tatizo.

Ambaye anathamini muda wake, hawezi kwenda kupoteza muda wake kwenye haya maigizo ya kampeni kwajili ya uchaguzi wa maigizo.
 
Wanaoenda kwenye hii mikutano ni watu ambao wamekosa cha kufanya, kwa hiyo hata wakishindishwa siku nzima hakuna tatizo.

Ambaye anathamini muda wake, hawezi kwenda kupoteza muda wake kwenye haya maigizo ya kampeni kwajili ya uchaguzi wa maigizo.
Walioko huko ni wale waliofeli Kila kitu kwenye maisha ila ndio wanatengeneze Dola.
 
Wananchi wanaocha shughuli za muhimu na kuhudhuri mikutano ya ccm, lazima wakubali pia kukabiliana na matokeo ya maamuzi yao.
Katika zama hizi ambazo siasa zimekuwa hivi zilivyo, wenye akili timamu na shughuli muhimu za kufanya hawahudhurii mikutano hiyo.
 
Kwamba nchimbi ni wa muhimu sana anasubiriwa kwa hamu sio acha useng'e bro
 
Back
Top Bottom