Ziara ya CCM kwa helkopta ya Polisi!!

Ziara ya CCM kwa helkopta ya Polisi!!

MashaJF

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
246
Reaction score
119
Wajameni hapa sijaelewa kitu naomba msaada kwa wahusika na waandishi wa habari walio kuwepo, huu usafiri mhusika alitoka nao wapi? Na aliukodisha ili na mimi nikakodishe au aliutumia kwa kutumia kigezo gani?

Nimeona hii habari yenye picha kwenye hizo links hapo chini ikisema hivi :

"
(Picha na Dustan Shekidele / GPL, Morogoro)

mamasalma3.JPG


mamasalma6.JPG


Kama ndio hivi basi tuna matatizo makubwa sana katika nchi hii, viongozi wote tulio nao wanashindwa kusimamia misingi ya kazi zao? Au ni njaa kwamba ukisimamia misingi ya kazi na kwa sababu umeteuliwa na bwana mkubwa utapoteza kazi?

Namukuu hapa Mama AnnaTibaijuka (Prof):

"Matumizi ya mali na vyombo vya Serikali sharti yawe na maslahi na manufaa kwa umma. Kwa upande wa ndege za Serikali hutumika na viongozi wa ngazi za juu kabisa serikalini, Rais, Makamu, Waziri Mkuu kuokoa muda wao na hivyo kuleta tija na ufanisi.

Juzijuzi taita letu lilibahatika kushuhudia AirForce One ikitua Tanzania na Mhe Rais Obama. Siyo mbwembwe tu. Ni ulazima kwa kazi yenyewe ilivyo.

Kama ilivyokuwa katika hali ya dharura nilivyoeleza, ndege zinaweza kutumika kwa Waziri au watu wengine kwa ridhaa ya viongozi hao wakuu wenye mamlaka nazo. Ndivyo ilivyokuwa. Ni muhimu kwa WanaJFJ kulielewa hili bila kujali itikadi zetu.

Niseme tu ninamshukuru sana Mhe Rais kuniwezesha kuwaona wapiga kura wangu na kushiriki majukumu ya kimataifa yaliyokuwa yanatungojea. La sivyo ningeshindwa mojawapo.


Kwa hiyo kweli hoja kwamba ningetafuta abiria wengine kupewa lift haipo, ila kama wangelikuwepo ninaamini wangepewa lift.

Na hoja za laana, mimi sioni Wahaya wamelaaniwa kwa lipi? Na sioni mbali na fitna na propaganda, EPA inaingia je katika dharura ya malaria Muleba? Tusichanganye mambo wala tusiwe cynical, tukakata tamaa juu ya nchi yetu na kutawaliwa na hasira juu ya mambo ya msingi. Penye mapungufu tuseme na kutaka marekebisho, lakini kutawaliwa na hasira haisaidii. Unabaki kutoa hukumu bila tafakari sahihi."
 
haaa hii hatari sasa! ndo maana polisi hawaaminiki!
 
mamasalma1.JPG mamasalma3.JPG mamasalma4.JPG

Mama Salma Kikwete ametua mjini Morogoro na Helkopta au Chopa ya POLISI kwa shughuli za kichama (CHAMA CHA MAPINDUZI) Hii imeakaaje wakuu? Maana kipindi cha kampeni aliwahi tumia ndege ya serikali kufanya ziara za kichama aliibuka Kinana haraka haraka na kuonyesha receipt zilizo kuwa zikikinzana kwa wale matomaso mnaweza gonga hapa Je, Wakala wa Ndege za serikali na Ikulu walitenda Rushwa?
 
Kwa msaada wale wenye simu za mchina pia mnaweza kusoma hapa

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"][/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"] [TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Je, Wakala wa Ndege za serikali na Ikulu walitenda Rushwa?
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD]
flight001.jpg

Miezi za mwisho za Uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika mwisho wa October 2010 vyombo vya habari vilisheheni taarifa kuwa viongozi wa juu kabisa wa siasa na serikali ya Tanzania kwamba walikua wanakiuka sheria za nchi na kanuni za uchaguzi kwa kutumia rasilimali za taifa katika kampeni za uchaguzi.
Vyombo vya habari vilitaarifu kile walichokiita kuwa ni ushahidi tosha wa kuthibitisha jinsi chama tawala Chama Cha Mapinduzi-CCM kupitia mgombea wake wa urais bwana Jakaya Kikwete alivyotumia cheo alichonacho kama raisi wa Jamhuri ya muungano kutumia rasilimali za taifa kwenye kampeni zake. (Kamati ya kuangalia uchaguzi Tanzania ‘Tanzania Elections Monitoring Committee-TEMCO' nayo katika tarifa yake ya awali kuhusu mwenendo wa uchaguzi mkuu 2010 nayo iligusia suala hii ya matumizi ya rasilimali za umma wakati wa uchaguzi na viongozi wa serikali)

Vyama vya upinzani vilijitokeza kwenye vyombo vya habari na kulalamikia CCM kufurahia matunda ya Taifa kwa kutumia fedha za walipa kodi.

Waliitaka Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC kuingilia kati na kumsimamisha mgombea wa urais kupitia CCM au kumwondoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa kuvunja sheria ya uchaguzi, maadili ya uchaguzi na sheria ya gharama za uchaguzi. Vifungu hivi vyote vya sheria pamoja na taratibu hizi ninambana mgombea kutotumia rasilimali za Taifa kama vile vyombo vya usafiri na mengineyo kipindi cha uchaguzi.
Haya yote yalianza mwezi Agosti iliporipotiwa kuwa Taifa linatumia fedha za serikali kuandaa vifaa vya uchaguzi kwa ajili ya CCM. Baadaye ripoti ziliandaliwa kwa undani na gazeti la Mwanahalisi kama makala maalumu Agosti 11-17 2010 uk.2 kwamba CCM ilitumia rasilimali za serikali kuchapisha mabango ya kumnadi mgombea wake wa uraisi.
flight002.jpg

Makala hiyo ilieleza kwa undani kuhusu barua pepe iliyokamatwa ya mawasiliano kati ya viongozi wa juu wa ikulu, bwana Salva Rweyemamu ambaye ni mkurugenzi wa habari ikulu, bwana January Makamba ambaye ni mshauri wa kisiasa na mwandishi wa hotuba wa rais, bwana Abdallahaman Kinana ambaye ni mwenyekiti wa kampeni wa CCM pamoja na Ramji mmoja wa wawakilishi wa shirika/kampuni iliyosajiliwa na Canada ya Mediapix International Ltd.
Shirika hilo lenye anwani yake nchini Kanada linalofanya kazi nchini China, liliingia mkataba na CCM wa kuchapisha vitu mbalimbali vya ikiwa ni pamoja na mabango ya rais na vifaa vingine vya kampeni ambavyo viligharimu jumla ya dola za kimarekani milioni 1.5 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania bilioni 2.17. mkataba kati ya CCM na Mediapix International Ltd ulisaainiwa tarehe 22 mwezi Juni mwaka huu 2010 na ulishuhudiwa na mwanasheria mkuu wa shirika hilo la Kanada Jane Barvey Associates of 300 Borough, Toronto-Canada.
Kwa mujibu wa mkataba huo, serikali ilitakiwa kulipa asilimia hamsini ambayo ni sawa na dola 750,000 kufikia mwisho wa mwezi Juni mwaka 2010 na kiasi kilichobaki kingelipwa kufikia tarehe 7 mwezi Julai mwaka 2010. Vocha mbili za malipo hayo zenye nambari MPX/CCN-TZGOV2010/2713 na MPX/CCM-TZGOV2010/2717 zilitumwa kwa serikali na Chama Cha Mapinduzi-CCM tarehe 22 mwezi Juni 2010. Malipo haya yalikua ni kwa ajili ya mabango 600,000 ya rangi kwa ajili ya mgombea wa urais kupitia tiketi ya CCM.
Fedha hiyo ilitakiwa kutumwa kwenye benki ya The Royal Bank of Canada iliyopo kiwanja namba 571 Sandulst Circle, Scarbourg, Ontario MIV 1V2, namba ya simu 416 292-6791. Kodi za malipo hayo pamoja ni miwala mingine ilitakiwa kufanyikia nchini Kanada.
Kufuatana na taarifa za habari pamoja na taarifa kutokana na ankara zilizokamatwa, taarifa zilidaiwa kuwa ni thabiti zilisambaa ndani ya muda mfupi mnamo mwezi Juni mwaka 2010.
Barua pepe moja iliyokamatwa ilionyesha wazi maelekezo kutoka ikulu kwenda Mediapix International Ltd kuhusiana na jinsi malipo yatakavyokuwa na jinsi mabango yavyotakiwa kuonekana na kutumika.
Katika barua pepe hiyo inayodaiwa kuandikwa tarehe 3 ya mwezi Julai 2010 majira ya saa 12.04.46, jioni bwana Salva alinukuliwa akimjibu mmoja wa wawakilishi wa Mediapix-bwana Sarakikya, alisema
" Nimekwisha ongea na mwenyekiti wetu bwana Kinana (mwenyekiti wa timu ya kampeni wa CCM) pamoja na Bwana Ramji kuhusu kuhusu suala lako na mwenyekiti amekubali lakini kwa masharti yafuatayo, utatumia picha za rais kwa ajili ya mabango tu na si kwa shughuli nyingine na mawasiliano yataendelea kua ni ya usiri wa hali ya juu sana". Bwana Salva alikua akijibu barua pepe iliyoandikwa na bwana Sarakikya aliyoituma Ikulu tarehe 3 Julai 2010, majira ya saa 8.20.11 mchana ikielezea ubora wa picha zilizotumwa Mediapix kwa ajili ya uchapishaji wa mabango.
Hadi kufikia uandaji wa makala hii, serikali bado haijatoa maelezo juu ya suala hilo, ikiuachia umma kuamini kuwa huenda serikali ilijihusisha na mambo mabaya ya kisiasa.
Muda mfupi baada ya taarifa hizi, tuhuma nyingine zilibuliwa kuwa mke wa mgombea wa urais kupitia tiketi ya CCM alitumia ndege za serikali pamoja na magari ya kubebea wagonjwa yajulikanayo kama Ambulances kipindi cha safari za kampeni zake. Taarifa zilitolewa zikiambatana na vithibitisho na picha zilizochukuliwa kipindi cha kampeni za urais mkoani Mwanza ambazo zilionyesha gari ya wagonjwa ikiwa imegesha karibu na sehemu ya kampeni. Mahojiano na viongozi wa idara ya Afya wilaya Mwanza walithibitisha kutumia gari hilo wakati wa kampeni ili kukabiliana na dharura yote ambayo ingeweza kutokea wakati wa kampeni.
Chama tawala kiliamua kuvifukuza vyombo vya habari bila sababu ya msingi kwa tuhuma kuwa vilikuwa vinafuatilia bili zake za kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa mujibu wa viongozi wa ngazi za juu za CCM, kisheria chama kilifikia gharama za kampeni za mgombea wake wa urais pamoja na msafara wake.
Katika mahojiano maalumu na kwa nyakati tofauti, katibu mkuu wa CCM bwana Yusufu Makamba na katibu/afisa habari wa CCM bwana John Chiligati walisema kua chama kimejipanga vyema kifedha kwa ajili ya kampeni kupitia njia mbalimbali za chama za ukusanyaji fedha na kwamba chama kinatumia fedha kisheria kutoka kwenye mfuko halali wa chama pamoja na misaada ya wanachama wake.
Katika mkutano wake na vyombo vya habari, mkurugenzi wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi-CCM, bwana Kinana aliwasilisha maelezo ya kina pamoja na stakabadhi ya gharama zilizotumika kugharimia magari pamoja na kukodi ndege ya serikali kusafiria kwa mke wa mgombea wa uraisi pamoja na timu yake ya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini.
Pamoja na hayo, uwasilishwaji wa stakabadhi na ankara katika kusaidia upande wa chama tawala ulizua maswali mengi kuliko majibu. Tangu hapo, watu bado wanahoji na kutaka majibu ya kuridhisha pamoja na maelezo sahihi kuhusu mpango mzima ambao umeonekana kuhusisha shirika la Taifa la ndege na ikulu.
Kwa mujibu wa bwana Kinana, CCM iligharimia kisheria kundi la magari kumtembeza katika sehemu mbalimbali mgombea wake wa uraisi pamoja na msafara wake (ikiwemo Mke wake na wengine wote wafanyao kampeni) kipindi chote cha kampeni. Ili kuwezesha usafiri wa haraka, chama tawala, kisheria kilikodi ndege kutoka shirika la Taifa la ndege liitwalo Tanzania Government Flight Agency-(TGFA) na kwamba kilipa gharama zote zilizohitajika. Bwana Kinana aliwasilisha kwenye mkutano stakabadhi kutoka TGFA kama ushahidi kutetea matumizi ya chama chake.
Maswali ambayo yalisumbua na kuendelea kusumbua vichwa vya wengi mpaka leo ni kwamba, Je, shirika la ndege la Taifa lina mamlaka ya kukodisha ndege kwa mtu binafsi nje ya shughuli za kiserikali?
Kwa mujibu wa bwana Kinana, TGFA imekua ikikodisha ndege za serikali kwa watu binafsi katika matukio mbalimbali na hata kwa CCM haikuwa kitu kigeni. Lakini swali linaloibuka hapo ni je, hii ni njia sahihi kwa mtu binafsi kukodi ndege ya serikali kwa gharama hiyo? Kwanini mtendaji Mkuu (CEO) ama mtumishi husika wa TGFA hakutokea kufafanua taarifa kuhusiana na suala hili?
Je, ni CCM au CEO aliyetakiwa au aliyekua tayari kuwasilisha taarifa kuhusiana na watu wangapi na ni makampuni mangapi yaliweza kukodi ndege ya serikali tangu mwanzo?
Je, ankara zilizowasilishwa katika mkutano wa waandishi wa habari na kusambaa kwa umma mzima zilikuwa za kughushi? Inawezekanaje kwa kwa shirika kubwa la serikali kama TFGA kufanya kosa la wazi katika kuandaa ankara kwa kuonyesha saini ya kutatanisha ya dola na ile ya shilingi mwishoni mwa tarakimu 15,000 katika kumbukumbu moja? (angalia mchoro hapo juu).
Je, gharama ya dola za kimarekani 3000 kwa saa ni gharama sahihi iliyogharimu chama tawala? Na ni dola 15,000 kwa masaa matano inayosemekana kutumiwa na CCM au ni kwamba muda uliotumika kwa ndege ya Serikali ni zaidi ya masaa matano? Je, kuna mtu mmoja wapo alikuwa anafaidika na shughuli hizo kinyume na sheria?
Je, nyaraka hizi zilitengenezwa na vyama vya upinzani vikiwa na lengo la kuchafua kambi ya uchaguzi ya CCM kwa kumchafua mkurugenzi wa kampeni, mgombea wa uraisi, mke wa mgombea wa uraisi kupitia CCM au wapambe na ikulu?
Tangu kipindi hicho, hakuna ofisa yeyote wa Serikali aliyezungumzia jambo hilo na kusababisha umma kujiuliza kama Serikali ilijihusisha na masuala ya rushwa.
Ni kutokana na musukumo kutoka katika jamii na umma iliyopelekea mfumo wa ufuatiliaji wa rushwa (Tanzania Corruption Tracker System-CTS) kurejea, kuchambua na kuhifadhi ripoti au tarifa hizi, ili wadau husika waweze kuzifanyia kazi na kutoa ufananuzi utakaondoa utata uliomo miongoni mwa wanasisa na wananchi kwa ujumla juu ya matumizi ya madaraka ya kisiasa katika rasilimali za umma.
Bila maelezo ya kutosheleza kutoka mamlaka zinazohusika, maoni ya wananchi na umma kwa ujumla ni kwamba baadhi ya maofisa wa serikali pamoja na baadhi ya vitengo vya serikali huenda vinatumia vibaya madaraka yao, kukodisha kizembe vifaa vya Serikali kwa watu binafsi, kughushi au kuandika kinyume kabisa ankara au stakabadhi kwa wateja wao na kuandaa makundi ya mapato ya serikali.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Tutamwambia awe anasafiri na bajaji msitokwe povu humu
 
ngoja mama mwiguru aje ( a.k. juliana wa kufyozwa, a.k.a HAMMY-D, a.k.a Sherui, a.k.a Mingoi)
WATAKWAMBIA NA NEYE NI RAISI, SO ANATIMIZA MAJUKUMU YA SERIKALI YA SISIEMU..
 
Ziara ya 1st lady ulitaka aende na nini air msae yeye na walinzi wake..
 
Tukisema wanasema tuna wivu sasa sijui wanataka hadi watuchome na vijiti machoni ndiyo tuseme!
 
View attachment 101586View attachment 101587View attachment 101588

Mama Salma Kikwete ametua mjini Morogoro na Helkopta au Chopa ya POLISI kwa shughuli za kichama (CHAMA CHA MAPINDUZI) Hii imeakaaje wakuu? Maana kipindi cha kampeni aliwahi tumia ndege ya serikali kufanya ziara za kichama aliibuka Kinana haraka haraka na kuonyesha receipt zilizo kuwa zikikinzana kwa wale matomaso mnaweza gonga hapa Je, Wakala wa Ndege za serikali na Ikulu walitenda Rushwa?
Wapi imeandikwa kuwa anafanya kazi za chama au umetabiri mwenzetu mtabili
 
Makubwaaaaaaa,mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!
 
uzuri wa serikali ya tanzania kwenye safari yoyote huwa haishindikani pesa,usafiri hupatikana haraka sana,tatizo kwenye vitanda,dawa mahospitalini,madawati,vitabu mashuleni huwa pesa hakuna!!!
 
ccm na serikali yake na vyombo invyoviongoza wamejaa ma-mburura. Hakuna hata wa kumshauri mwenzie.
Vinginevyo wameshiba madaraka na kujifanya waflme... kila kitu kwao ni sawa , hakuna wa kuhoji. Useless bums!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom