Kamanda, naona hujasoma vizuri bandiko hili, Zenj (Zanzibar) ni wazuri sana katika riadha na hasa katika mbio fupi na michezo mingine. Sio wataalamu wa mbio ndefu kama Kenya ama Arusha ama Singida au Manyara kwa upande wa Tanzania Bara.
Wazenj wameweza kuutumia vema uwanja wao wa Amani katika kujiimarisha katika track and field.. Na wana rekodi ya muda mrefu ya kuwasumbua watz bara katika hili.
Ikubukwe kuwa Tz bara kwa muda mrefu wamekuwa hawana viwanja venye hadhi ya kimataifa the same to Kenya... hadi miaka ya hivi karibuni, ingawa wakenya wapo mbele kwa Watz Bara.
Hongera sana kwa Wazenj kwa kuweza kutamba katika mashindano haya ya Taifa. Zile kejeli za Mbatata za urojo itabidi wajiulize mara mbilimbili..😀