Kiasi cha wiki mbili tu zilizopita endapo pangetoea wa kuniuliza nawafahamu waigizaji wangapi wa Kihindi, jibu lingekuwa mmoja tu, Amitabh Bachchan! Na kama angeendelea kunitaka nitaje japo filamu moja aliyocheza Amitabh, it's definitely nisingekuwa na jibu! Katika maisha yangu yote, sijapata kuzipenda filamu za Kihindi, pamoja na mambo mengine, ni ile staili ya mlio wa magumi wanayopiga!
Wakati hayo yakiendelea, jumapili ya 15.03.2015 nikiwa ghetto nimetulia, vidole vikicheza kwenye remote, nikajishitukia tu naishia kwenye Zee World! Hii ni moja ya Channel ambazo endapo service provider angenipa option ya kuondoa channel yoyote na ili iwe replaced na yoyote hata kama ni Clouds TV, basi sina shaka ninge-opt waiondoe Zee World! Hapo kabla, sikuwahi kuiangalia hata siku moja... mara zote nilikuwa naipita tu !
Bila kutarajia, nikajikuta nimetuliza macho hapo Zee World... sina hakika ni nini kilinivutia, labda huenda nilivutiwa na binti wa Kihindi mwenye ngozi nyeusi! I think her innocence appearance ndiyo ilinivutia kutuliza macho hapo! Bila kutarajia, nikajikuta nimepoteza karibu dakika 15 na hatimae kuiweka remote pembeni... kuonesha ni kama nimefika! Punde si punde, nikagundua naangalia tamthilia iitwayo SALONI na huyo Binti wa Kihindi mwenye ngozi nyeusi ndie Saloni mwenyewe!!!
Niishie tu kusema kwamba, bila kukusudia, nikajikuta nimefuatilia episodes zote tano ambazo ni marudio ya wiki mzima!!! Wiki iliyofuata, nikajikuta siku mbili za awali (jtatu na jnne) naangalia marudio ya Saloni siku ya pili yake lakini hapa ninaposema, nimekosa kabisa ujasiri wa kusubiria marudio bali naangalia siku hiyo hiyo ya kwanza!!!
Wakati ya SALONI yakiwa hayo, Jumapili(au jumamosi, sikumbuki vizuri) iliyopita nikajikuta tena nimenaswa kwa staili ile ile ya jumapili iliyotangulia! Hata hivyo, siku hiyo nafahamu ni nini kilinivuta! Nikiwa nachezesha remote nikajikuta tena natua Zee World na hapo hapo nikakuta binti mwingine mdogo wa Kihindi mwenye umri wa takribani miaka 17-19. Kama ilivyokuwa kwa Saloni, Binti huyu nae alikuwa amejawa na innocence look lakini akionesha kuwa kwenye maswahibu makubwa zaidi kuliko alivyokuwa anaonekana Saloni! Kitu ambacho kilinivuta (sio kunivutia) ni kuona Binti huyu amepigishwa magoti huku mikono yake ikiwa imeegemezwa kwenye meza na jamaa mwenye jambia akiwa pembeni yake! Ilionesha dalili zote kwamba Binti yule alikuwa kwenye hukumu ya kukatwa mikono! Nikajikuta nataka kufahamu maswaibu yaliyomkuta binti wa watu!
Mikono ya binti yule haikukatwa lakini kama ilivyokuwa kwa Saloni, nikajikuta nimemaliza dakika 15 kama masihara na haikuchukua muda kubaini kwamba naangalia tamthilia ya LAALI na huyo binti aliyetaka kukatwa vidole ndie Naali mwenyewe! This's Laali, omg! Is the one of strongest characterization ever seen!!!
Kilichonikuta kwa Saloni, ndicho kimenikuta kwa Naali kiasi kwamba hivi sasa naogopa hata kuangalia matangazo ya tamthilia nyingine ninazoona wanazitangaza hapo Zee World kwa hofu ya kuwa mtumwa wa Zee World!!!
Swali ni kwamba, je humu jamvini kuna anayeziangalia hizi tamthilia? Kama yupo, ni kwamba ni uboya wangu ndio umenifanya hizi tamthilia zinibambe au kuna wengine ambao nao pia zimewabamba kwahiyo kama ni uboya basi tupo wengi?