tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Vyombo vya habari na waandishi wa habari wameshauriwa kuepuka kutumia lugha za chuki, uchochezi au zinazoweza kugawa jamii kwa misingi ya ukabila, dini au itikadi katika kipindi hiki cha kuelekea kampeni za uchaguzi.
Soma pia: ZEC: Vyama Visivyosaini Maadili ya Uchaguzi Havitaruhusiwa Kufanya Kampeni
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi, alitoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wahariri wa vyombo vya habari, waandishi, wapiga picha pamoja na wachukuaji wa maudhui ya mitandao ya kijamii yaliyofanyika katika ofisi za tume hiyo, Maisara.
Amesisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi taarifa za upotoshaji zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii, hivyo waandishi wanapaswa kuhakikisha wanathibitisha ukweli wa taarifa zote kabla ya kuzipa nafasi kwenye vyombo vya habari au mitandaoni.