Licha ya ratiba ya uchukuaji wa fomu za uteuzi wa nafasi za urais, uwakilishi na madiwani kuanza leo, lakini kwa nafasi ya urais vyama vya siasa vimeandika barua za kuomba kuchukua fomu kuanzia Agosti 30, 2025.
Wakati mchakato huo ukiendelea, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), inatarajia kutumia Sh12 bilioni katika shughuli zote za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
Akizungumza leo Agosti 28, 2025 Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar, Thabit Idarous Faina amesema dimba la uchukuaji fomu litafunguliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho mtiania wake wa urais atachukua fomu Agosti 30, saa 4: 00 asubuhi katika ofisi za Tume hiyo
Siku hiyohiyo pia Chama cha National League for Democracy (NLD) kitachukua fomu saa 5:00 asubuhi, Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP) kitachukua fomu saa 6:00 mchana na Chama cha Wananchi (CUF) kitachukua fomu saa 7:00 mchana na saa 8:00 mchana kitachukua Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) huku saa 9:00 alasiri watafunga siku hiyo kwa kutoa fomu kwa chama cha NRA
Kwa mujibu wa Faina, Agosti 31, 2025 wataanza na chama cha NCCR Mageuzi saa 3:00 asubuhi, saa 4:00 asubuhi itakuwa ni Chama cha ACT Wazalendo huku saa 5:00 asubuhi watakuwa na chama cha Kijamii CCK, kikifuatiwa na Chama cha DP ambacho kitachukua fomu saa 6:00 mchana
Amesema katika uchukuaji wa fomu lazima mwombaji apate namba maalumu ya malipo (control number) kwa ajili ya kulipia na tayari vyama vyote 17 vimeshachukua namba ya malipo kwa ajili ya fomu hizo
Chanzo: Mwananchi_official