kama ulikuwepo vile... Mimi nilichogundua niliporudi tz ni kuwa madereva wa Tanzania wana roho mbaya sana. Akikuona unakatisha bara bara yeye ndio anaongeza speed ya gari ili akuwahi . Wana roho ya kinyama sana.
Baada ya miaka mingi, nilirudi bongo juzi and I must say nilinusurika kugongwa na magari mara mbili wakati navuka barabara kwenye zebra crossing. Baada ya siku kadhaa na kulizoea jiji nikagundua kwamba hizo crossings zipo tu kama mapambo na hakuna dereva anayeziheshimu. Ukitaka kuvuka barabara ni lazima usubiri hadi kuwe hakuna magari ndo uvuke hata kama uko kwenye zebra! Hii ina maana kwamba hakukuwa na haja ya kupoteza hela kuweka hii michoro na you might as well vukia barabara popote tu ambapo unaona ni safe.
Ikumbukwe kwamba kwenye zebra crossing ni sehemu salama ambayo mwenda kwa miguu ana haki ya kuvuka barabara na dereva anapaswa kusimama kama kuna watu wanaosubiri kuvuka. Kama wanaosimamia sheria za barabarani wameshindwa kuwabana madereva waheshimu alama za barabarani na kuhatarisha maisha ya waendao kwa miguu, ni bora kabisa waondoe hizi alama barabarani manake zinaweza zikaku mislead ukajikuta umegongwa......
Kana-Ka-Nsungu
NN heshima yako mkubwa, long time man.
Kweli hiyo ya traffic light nayo niliishuhudia mara nyingi tu, yani kama ulivosema hata kama ngoma ni green kwako una proceed with caution. Lakini kwenye round about mimi nilivofunzwa na muingereza hapa (na najua nyumbani tunatumia system zao hawa jamaa) ni kuwa unampa priority mtu aliyeko kulia kwako and am sure hii ni kitu ambayo madereva wengi hawaijui. Tatizo jingine kubwa pia ni matumizi ya honi yasiyo lazima, yani ni kama vile watu wanaendeshea honi, mtu akiwa ana overtake honiii, foleni ikiwa haisogei kila mtu anapiga honi, mtu akimuona msichana mzuri anapita pembeni anatwanga honii tu, kero tupu
Asilimia 80 ya madereva wa tanzania hawana leseni au kama wanazo wamezipata kwa deal, hawajazisotea kama ambavyo unasomea ukiwa nchi za wenzetu. Ndio maana ajali bongo haziishi coz watu wamelewa wanaendesha magari tena ya abiria au waendesha pipipiki wamejifunzia mafichoni so alama za barabarani kama zebra, stpo nk. kwao ni mabango tu hayana maana yoyote.