Charles Mkubya
JF-Expert Member
- Aug 27, 2009
- 206
- 161
Ndugu zangu wana JF, nimewiwa kuwashirikisha katika hili nikiamini naweza pata msaada toka kwa members wa JF. Nimeibiwa simu yangu jumanne ilopita (18 Feb 2014) eneo moja maarufu kwa jina la darajani kuelekea mataa ya chang'ombe mida ya saa moja jioni. Simu iloibiwa ni IPHONE 5 nyeusi na bahati nzuri nilifanikiwa kuwasiliana na APPLE, na kwa sasa iko kwenye Lost Mode hivyo itamuia vigumu mtu yoyote kuitumia kwa namna yoyote ile achilia mbali kuifanyia flashing. Mara ya mwisho imeonekana usiku wa tukio maeneo ya KEKO mtaa wa mapinduzi. Kwa yeyote atakaefanikiwa kuipata kwa namna yeyote ile kuna zawadi ya laki moja taslimu (100,000) sababu najua alieiba atahitaji kuiuza kwa watu au ameshaiuza kwa mtu na anaweza kuwa member wa JF. Ukiiwasha tu utakutana na ujumbe wangu na number yangu ya simu jinsi ya kunipata. Sitohitaji kujua nani kaiba au nani kamuuzia nani na hii itakuwa baina yangu na huyo atakaefanikiwa kunirejeshea. Number yangu ya simu ni 0785690479, natanguliza shukrani zangu kwa JF members nikiwa na imani kuna siku nitatoa mrejesho wa mafanikio, Asanteni sana.
Charles Mkubya.
Charles Mkubya.