warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,273
- 18,422
Kufuatia madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa na katabia ka’ kujiweka kimahaba kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa Sauzi, madai yametua mezani mwa gazeti hili kuwa, kimenuka kati ya Zari na Kajala.
Chanzo chetu makini ambacho kimeomba jina lake lisitajwe gazetini kimedai kuwa, hivi karibuni baada ya Zari kupata ubuyu huo wa kuchovyewa penzi lake, alitafuta simu ya Kajala kisha kumpigia na kumpa makavu kuwa, asimuingilie kwenye himaya yake.
“Siku moja nilikuwa na Kajala, mara ikaingia simu ambapo alipopokea akasikia sauti ya Zari, basi unaambiwa akamsema sana juu ya kuingilia penzi lake, Kajala akawa kimyaa, wala hajajibu lolote, inavyoonekana alipewa makavu,” alidai mtoa habari huyo.
Baada ya kupata habari hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kajala ili kuzungumzia madai hayo ambapo alipokea simu na kupewa mkanda mzima, alishangaa na kuuliza: “Nyie nani kawaletea hizo habari, jamani watu wambeya sana.” Alipobanwa zaidi akasema hawezi kuongelea hayo mambo.
Zari hakuweza kupatikana mara moja ila Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kupitia simu yake ambapo mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Ijumaa: Ebwana kuna habari kuwa Zari alimpiga mkwara Kajala juu ya tuhuma za kutoka na wewe kimapenzi sijui hilo likoje kwa upande wako?
Diamond: Hahahaa, sema nini mwanangu, hapa sikusikii vizuri nipo njiani naelekea Sweden.
Ijumaa: We nijibu tu, imekuwaje?
Diamond: Dah! Kweli mimi hata nakosa hata la kusema hapo maana mambo ya wanawake ni ngumu kuyaingilia kwa namna yoyote ile ila sijui nini hapo.
Ijumaa: Oke poa.
Kipindi cha nyuma ilidaiwa kuwa, Kajala alikuwa na uhusiano wa siri na Diamond mpaka ikafikia hatua baadhi ya watu kuhisi hata ile mimba aliyokuwa nayo Kajala ilikuwa ya msanii huyo anayefanya poa kwa sasa kwenye muziki.