Zao la ubaguzi sasa tujifunze kuishi,kama watanzania tusibaguane kwa misingi ya siasa au dini!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Wana,Bodi,Asalm,
Nirudi katika kichwa cha Habari na nitajikita katika historia.
Nakumbuka mwaka 1996 wakati wa chama kikuu cha upinzani NCCR Mageuzi watu walipigwa sana pale Kisutu.
Watu waliokuwa wapinzani walinyanyaswa...siku moja pale kitonga alipita Mjumbe wa kamati kuu ya CCM,(CC,NEC) na Waziri Mkuu wa kipindi hicho alisema maneno mengi na kuwambia viongozi wapale kumshughulikia mwenye Hotel ya Comfort kisa ni mpinzani! Nakweli alishughulikiwa na bendera akaishusha ilikuwa ya CHADEMA kila siku serikali mlangoni kwake! Na si huyo tu!!Ni utamaduni uliojengeka katika mfumo wetu wa siasa na waanzirilishi wapo wanaona!.
Mfano leo Frederick T.Summaye analia kunyang'anywa shamba amesahau kuwa huu ni mfumo waliuanzisha wao??Atulie asubiri zamu yake ya utawala aje awanyang'anye viongozi wa CCM waliojilimbikizia mashamba!
Mwenzake Lowassa ni mjanja yupo Kimya siyo kuwa hapitii katika tanuri anapita anajikaza kwakuwa anajua ni mfumo!!
Ndiyo maana Mwalimu Nyerere alisha sema ukila nyama ya mtu huwezi kuacha kamwe hili ndilo zao la ubaguzi.
Tamati.
 
Back
Top Bottom