Zanzibaris want more powers for Vice-President

Zanzibaris want more powers for Vice-President

..Raisi wa Zenj akiwa ndiyo makamu wa muungano basi itabidi kiongezwe kipengele kwamba asiwe na mamlaka ya kukaimu nafasi ya Raisi, wala kuchukua nafasi hiyo ikiwa Raisi atashindwa kutawala. hoja yangu inatokana na ukweli kwamba kuna uwezekano Raisi wa Muungano na yule wa Zanzibar wakatokana na vyama viwili tofauti.

..vilevile badala ya kuangalia majina ya vyeo, kama makamu wa raisi, labda tujielekeze ktk kubainisha majukumu[porfolio] ya viongozi hao yatahusisha maeneo gani. je, Raisi wa Zanzibar akiwa makamu wa Raisi majukumu yake ktk serikali ya muungano yatahusisha maeneo gani?

..zaidi, tuangalie uhalali wa Raisi wa Zanzibar, ambaye hapigiwi kura na wananchi wa Tanganyika, kupewa wadhifa wa kuwa makamu wa Raisi wa muungano. Raisi wa Zanzibar akiwa makamu wa Raisi, then what do we do kwa hii nafasi ya Makamu wa Raisi iliyoko sasa hivi?
 
Huu muungano usiwe mzigo kwa pande yoyote,uvunjwe tu kwa amani kwani hata hivo tutabakia kama east african union.

Ila kuishi na binadamu kazi jamani,pengine tukiwa kama nchi jirani tutaheshimiana zaidi na kupendana.
 
..Raisi wa Zenj akiwa ndiyo makamu wa muungano basi itabidi kiongezwe kipengele kwamba asiwe na mamlaka ya kukaimu nafasi ya Raisi, wala kuchukua nafasi hiyo ikiwa Raisi atashindwa kutawala. hoja yangu inatokana na ukweli kwamba kuna uwezekano Raisi wa Muungano na yule wa Zanzibar wakatokana na vyama viwili tofauti.

..zaidi, tuangalie uhalali wa Raisi wa Zanzibar, ambaye hapigiwi kura na wananchi wa Tanganyika, kupewa wadhifa wa kuwa makamu wa Raisi wa muungano. Raisi wa Zanzibar akiwa makamu wa Raisi, then what do we do kwa hii nafasi ya Makamu wa Raisi iliyoko sasa hivi?


Mkuu.
Hapa ndio ile mantiki ya serikali ndogo ya Muungano inapoonekana umuhimu wake,pia bunge dogo lenye wawakilishi au wabunge wachache kama system ya EAC...serikali Tatu...Ya Tanganyika, Ya Zanzibar na serikali ya mambo ya Muungano au mambo ya pamoja.

Lakini kwa vile Kenya ,Uganda, Rwanda na Burundi hawakuvutika kujiunga na Muungano huu wa TZ,(kwa vile haueleweki ) ni vyema zaidi uvunjwe ili nchi mbili, Tanganyika na ile ya Zanzibar zijiunge na EAC kama nchi huru ili kufanya ndoto ya kuelekea umoja wa Afrika kuwa rahisi na kuondosha layers, ugumu, kero na misuguano ambayo haina ulazima. Pia itakuwa ndio ukomo wa usanii wa Muungano wa TZ.
 
Back
Top Bottom